WCB watembelewa na Waziri wa mambo ya ndani

WCB watembelewa na Waziri wa mambo ya ndani

Diamond siyo artist peke yake, bali ni mwajiri aliyeajiri vijana zaidi ya hamsini, na katika vijana hao wapo wenye watoto, wake na wengine ndio tegemeo katika familia zao. Anawalipia mafao hao vijana, na zaidi analipa kodi zaidi ya milioni 40 kwa mwaka. Sasa nijuze ni kijana gani msanii ambaye anafanya kazi zaidi ya Diamond? Ukifikiria hapo, basi utaelewa kwa nini wanasiasa na viongozi wanakwenda kutembelea WCB kila mara. Wana mambo mengi ya kujifunza kutoka WCB ili wakaweze kushare hayo mambo na vijana wengine wanaohangaika kujikwamua kimaisha. Ukiwa kiongozi, na ukawa na nia ya kusaidia wasaniii au jamii fulani, basi ni lazima ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa na ujifunze kutoka kwa waliofeli ili kusudi upate njia sahihi ya kuwasaidia wanaokwama.
Umeongea kwa busara sana bila kuweka utimu shukran mkuu
 
Hivi wale wengine wa mikataba ya sony hua hawana ofice, ili viongozi wao wawatembelee

Kila siku naona wcb wakitembelea tu

Bado mukulu magu nae atembelee ofice, za wcb
Wenye mikataba ya sony ni akina nani
magu he is too busy with government issues hawez kuja
 
Diamond siyo artist peke yake, bali ni mwajiri aliyeajiri vijana zaidi ya hamsini, na katika vijana hao wapo wenye watoto, wake na wengine ndio tegemeo katika familia zao. Anawalipia mafao hao vijana, na zaidi analipa kodi zaidi ya milioni 40 kwa mwaka. Sasa nijuze ni kijana gani msanii ambaye anafanya kazi zaidi ya Diamond? Ukifikiria hapo, basi utaelewa kwa nini wanasiasa na viongozi wanakwenda kutembelea WCB kila mara. Wana mambo mengi ya kujifunza kutoka WCB ili wakaweze kushare hayo mambo na vijana wengine wanaohangaika kujikwamua kimaisha. Ukiwa kiongozi, na ukawa na nia ya kusaidia wasaniii au jamii fulani, basi ni lazima ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa na ujifunze kutoka kwa waliofeli ili kusudi upate njia sahihi ya kuwasaidia wanaokwama.
I disagree.... kuna watanzania wengi sana wameajiri zaidi ya watu 500 na hii haiko recognized

I feel sorry for our president, vijana wake hawana objectives kabisa... kumtembelea uimbaji mmoja na kuifanya agenda leaves a lot to be desired

[HASHTAG]#TatizoNiSisi[/HASHTAG].....
 
Ben na majibu ya miili 7 kule Ruvu yamepatikana???
Yaani viongozi wa Afrika na hasa Tz. ni waajabu sana kufanya inappropriate duties and repsponsibilities with every thn is politics.
kwenye maisha muda wote ukichukulia mambo too serious utakufa mapema.....
 
I disagree.... kuna watanzania wengi sana wameajiri zaidi ya watu 500 na hii haiko recognized

I feel sorry for our president, vijana wake hawana objectives kabisa... kumtembelea uimbaji mmoja na kuifanya agenda leaves a lot to be desired

[HASHTAG]#TatizoNiSisi[/HASHTAG].....
Mkuu hapa tunazungumzia mziki na sanaa. Hakuna mwanamziki au msanii yoyote katika tanzania hii alieajiri vijana wengi zaidi ya Diamond. Na hii ni kwa sababu wasanii wengi hawakuchukulia kama vipaji vyao vya sanaa vinaweza kuwa ajira rasmi, au labda walikosa maarifa ya kuifanya sanaa kama ajira kuu ya kujiingizia kipato. Hao 500 unaowasema wewe ni katika sekta zingine ambazo zipo zilizoajiri hata wafanyakazi zaidi ya elfu. Halafu unapoangalia fursa usiangalie fursa moja ukaona ndio ina umuhimu mkubwa kuliko zingine. Haiwezekani watanzania wote tukawa kama Bakheresa au tukafanya biashara anayofanya Bakharesa. Ni lazima kuangalia katika pande zote ili kuweza kuwawezesha vijana. Muziki na sanaa ni sehemu ambayo inapaswa pia kutupiwa jicho hasa ukizingatia vijana wengi wanajitosa huko na wapo ambao wameanza kuonyesha kwamba kuna mafanikio yanaweza kupatika kupitia shughuli hiyo. Unapokuwa kiongozi hupaswi kudharau kazi eti kisa tu unaona haina mchango mkubwa au umuhimu mkubwa.
 
Wanasemaga fuvu sijui ina maanisha nini vilee...halafu kama naliona hapo mezani kwa mkubwa mondi.....
 
Back
Top Bottom