Ni kweli kabisa lakini amini usamini bado wapenzi wengi wa Simba bado hawajaona tatizo kwenye kiungo mkabaji na beki wa kati pamoja na kuangalia mechi ya Azam wao wanaangalia ubao wa matokeo basi wanaridhika. Yule Chilunda angekuwa na uzoefu kidogo tu ilikuwa majanga na sijui kwanini Azam hawakuwaanzisha Chirwa, Ngoma na Nado/Chilunda kwa pamoja maana mechi ingekuwa ngumu sana. Simba tukatae tukubali kosa kubwa limefanyika kumwacha Kotei aondoke na pia hatukutafuta beki wa kati wa kimataifa anayelijua soka la Afrika. Anyway tusubiri labda hao wabrazili wakipata moto labda watasaidia vinginevyo unakutana na Esperance, TP Mazembe, Al haly huku kiungo mkabaji Mkude na beki wa kati Wawa hiyo zile tano tano ndio mwanzo wake. Huyo Wawa kwenye ligi ya bongo bado fresh tu. Ila Uchebe naye acheze kamari kwa akina Kennedy na Mlipili wapate uzoefu wanaweza kuja kumsaidia huko mbele ya safari.upo sawa mkuu wote ni washabik wa simba tusijifarij saana kwamba tuna timu nzur bado ukuta wetu ni janga kubwa. pale nyuma tungekuwa na combineshen kama ya yokub na agrey wa azam na tungepata mtu kama bwalya angalau tungesema tuna uhakika hata wa kufikia record ya mwaka jana. Kwa simba hii na uchebe jins alivyokariri wachezaj tutafika makund kwa vile droo imetubeba kiaina. Replacrment ya wawa na bocco ni inevitable. Afu na sisi tunapenda sana vya bure huwez tegemea kupata jembe la maana kwa kusubir wachezaj waliomaliza mikataba ndo uwasajil. Watu wanavunja bank, Kwa simba level yetu kubwa itakuwa kwenye makundi
Ila kwa ligi ya bongo nazionea tu huruma timu pinzani kwa kweli kuna timu dhahama kama sio gharika litawakuta.