Tanzania bado hatujaweza kufanikiwa vizuri katika Agriculture revolution.
Industrial revolution iko kwenye mchakato kwa mskumo wa Kisiasa.
Kenya wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika swala Zima la Industrial revolution.
Inchi zenye uchumi wa aina hii zina policy inayozuia finished products toka nje.
Kenya wako tayari kuagiza mahindi hata kutoka Brazili, Zambia, South Africa au popote lakini si kuagiza unga toka Inchi za Nje.
Inchi kama Brazili wameendelea kuliko Tanzania lakini kama kuna Inchi inataka mahindi hawawezi kuwapa masharti kwa sababu wao wanataka pesa.
Tanzania tukubali kuuza ziada ya mahindi yetu Kenya kwa manufaa ya shilingi yetu ukilinganisha na shilingi ya Kenya na kwa manufaa ya wakulima wetu kwa sababu watapata soko na bei zitakuwa juu.