Umesoma kila kitu nilichoandika, tatizo unajifanya hamnazo tu. Hivi nikuulize swali, tukiruhusu kuuza mahindi kwa yeyote anayetaka, unadhani kuna nchi itakayoagiza unga?, kwasababu ukiagiza mahindi mahindi unapata kwa bei ya chini kuliko Unga, na hayo mahindi sio tu yatatengeneza ajira katika viwanda vyao, lakini pia yatapunguza ajira zetu na kupunguza upatikanaji wa Mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyetu.
Kila nchi lazima iwe na Sera ya kulinda viwanda vyake, hivi unadhani kwanini wakenya hapa JF wanapinga kununua unga badala yake wanalazimisha mahindi?, lengo ni kutaka kuhakikisha viwanda vyao vinapata Mali ghafi ya kutosha.
Wewe una wasiwasi gani?, kama umemsikia vizuri huyo mkenya ktk hiyo clip anasema kwamba wamekuja kuwahi kwasababu nchi zote zilizotuzunguka Nina upungufu wa mahindi isipokua TZ, kwahiyo wakikataa unga, tutawauzia watakaokubaliana na terms zetu.