We miss you JPM, where are you!!?

We miss you JPM, where are you!!?

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,057
Reaction score
7,611
Tunaweza kusema Pasi Na Shaka yoyote kwamba Kwa Sasa Huu unaweza kuwa ni wimbo ambao unaimbwa Sana Na wale tunaoikumbuka Kazi ya Shujaa huyu wa Afrika.

Na hili halijifichi Hasa unapowazungumzia wale wote wenye kuitumia Barabara ya Morogoro kipande kutoka maili Moja Kibaha mpaka kuitafuta mlandizi, hakika maumivu Ni makubwa Sana Na si masihara. Naamini walio wengi wanaamini Na ndo ukweli wenyewe kwamba kama si ushenzi wa wachumia tumbo Wachache wa kumuondoa huyu Mwamba basi zile Barabara njia 8 kama Za kimara- Kibaha basi hivi Leo zingelikuwa zimefika mlandizi kama si Chalinze kabisa.

Na Mie naungana nao katika vilio hivo vya wengi, sahivi kutoka mbezi kuitafuta Chalinze si Chini ya masaa 3 Na Zaidi Hasa nyakati Za jioni. Kweli tumepigwa Na kitu Kizito Na Kazi tunaiona kizimkazi.

Ndio maana Na sie hatuna budi kuungana Na wale weusi wa kwa Mzee Madiba Enzi zile, tunauliza "JPM where are you??" Barabara ya ndoto Zako imefia pale pale ulikoiacha. Na leo kwenda Morogoro ni shuruba isiyo kifani, Ni rahisi Sana ukasafiri kwenda Tanga Na ukafika Mapema lakini si kwenda Morogoro. Zile hesabu Zako Za kuokoa masaa katika uchumi wa nchi ulizokuwa unazipiga ukijenga ma flyovers zimeingiliwa Na wahuni watekaji
 
Usijali,

Yuaja mlawi JG kuimalizia KAZI aliyoianza Magu.
 
Si Barabara tu!

Yule mwamba hata mawe yatatoa mlio

Pumbavu zao sana hao wauza ngada na mafisadi, bila kuwasahau hao wapinzani ambao wimbo wao kwenye nchi yetu ni wao kuleta maendeleo ya kweli, cha ajabu wao ndio walikuwa wa kwanza kumpiga mawe mpinzani mwenzao JPM ambaye kwa dhati ya moyo wake alojitoa mhanga kuiletea maendeleo ya kweli nchi yetu
 
Zile hesabu Zako Za kuokoa masaa katika uchumi wa nchi ulizokuwa unazipiga ukijenga ma flyovers zimeingiliwa Na wahuni watekaji
Duh,
Halafu utekaji haupo huku Zanzibar, ni Tanganyika tu
 
Tunaweza kusema Pasi Na Shaka yoyote kwamba Kwa Sasa Huu unaweza kuwa wimbo ambao unaimbwa Sana Na wale tunaoikumbuka Kazi ya Shujaa huyu wa Afrika.

Na hili halijifichi Hasa unapowazungumzia wale wote wenye kuitumia Barabara ya Morogoro kipande kutoka maili Moja Kibaha mpaka kuitafuta mlandizi, hakika maumivu makubwa Sana Na si masihara. Naamini walio wengi wanaamini Na ndo ukweli wenyewe kwamba kama si ushenzi wa wachumia tumbo Wachache wa kumuondoa huyu Mwamba basi zile Barabara njia 8 kama Za kimara- Kibaha basi hivi Leo zingelikuwa zimefika mlandizi kama si Chalinze kabisa.

Na Mie naungana nao katika vilio hivo vya wengi, sahivi kutoka mbezi kuitafuta Chalinze si Chini ya masaa 3 Na Zaidi Hasa nyakati Za jioni. Kweli tumepigwa Na kitu Kizito Na Kazi tunaiona kizimkazi.

Na sie tunaungana Na wale wa kwa Madiba Enzi zile, tunauliza JPM where are you?? Barabara ya ndoto Zako imefia pale pale ulikoiacha Na kwenda Morogoro Leo Ni rahisi kusafiri kwenda
Tanga Na ukafika Mapema lakini si kwenda Morogoro. Zile hesabu Zako Za kuokoa masaa katika uchumi wa nchi ulizokuwa unazipiga ukijenga ma flyovers zimeingiliwa Na wahuni watekaji
Wabongo wengi kama wewe hata kama ni wa umri mkubwa, fikra zao ni kama za watoto.

Wanapenda kufanyiwa mambo na wengine.

Hawataki kukubali kwamba wao wana wajibu, hawataki kukubali kwamba nchi inajengwa na taasisi imara, watu, hata wakiwa imara vipi, wanapita tu.

Ndiyo maana ni rahsi kusikia watu wanamlikia Magufuli lakini ni vigumu kusikia watu wanajenga taasisi za kuisimamia serikali itekeleze kazi yake inavyotakiwa.
 
Kiongozi anaeuwa sekta binafsi hawezi kuwa kiongozi bora daima, Siuoni ushujaa wa JPM kwakuwa aliua sekta binafsi ambazo ndio chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi.

Kiongozi yeyote ambae atarudia sera za kuua azasi atakuwa anawachimbia kaburi watanzania, mtu aliefanya mamilion ya watanzania wakose ajira kwa kuuwa sekta binafsi hawezi kuwa shujaa, kwenye mizani kikwete yupo far sana kuwa shujaa kuliko jiwe.

Kama ushujaa wake ni kutumbua watendaji wa serikali hapo sawa, Kwangu shujaa ni kiongozo anaepigania ustawi wa wananchi kwa kuzalisha ajira za kutosha kwa kuzipa ustawi bora sekta binafsi na sio kuziua.

Watanzania tulio wengi si kwamba kipindi cha Jiwe tulikuwa na maisha mazuri bali tulikuwa tunafurahia kwa wenye unafuu wa maisha jinsi walivyokuwa wanateseka na ndio hulka ya masikini kuwa na furaha kipindi tajiri anapoteseka.

Kwangu Jiwe hawezi kuwa shujaa hata siku moja.
 
Magufuli alikuwa katili kwenye utawala wa Sheria na democracy Ila out of that he was a wise man

Kosa lililomgalimu na angekuwepo mpaka Leo ni kutaka kuwa rais wa milele kilikuwa kosa kubwa Sana !!

Samia yupo anakodoa tu na kulembua kupaka lipsticks😀😀😀😀
Nilinusa harufu ya hii kitu. Mbaya zaidi alikua anaipeleka less sana
 
Back
Top Bottom