Kiongozi anaeuwa sekta binafsi hawezi kuwa kiongozi bora daima, Siuoni ushujaa wa JPM kwakuwa aliua sekta binafsi ambazo ndio chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi.
Kiongozi yeyote ambae atarudia sera za kuua azasi atakuwa anawachimbia kaburi watanzania, mtu aliefanya mamilion ya watanzania wakose ajira kwa kuuwa sekta binafsi hawezi kuwa shujaa, kwenye mizani kikwete yupo far sana kuwa shujaa kuliko jiwe.
Kama ushujaa wake ni kutumbua watendaji wa serikali hapo sawa, Kwangu shujaa ni kiongozo anaepigania ustawi wa wananchi kwa kuzalisha ajira za kutosha kwa kuzipa ustawi bora sekta binafsi na sio kuziua.
Watanzania tulio wengi si kwamba kipindi cha Jiwe tulikuwa na maisha mazuri bali tulikuwa tunafurahia kwa wenye unafuu wa maisha jinsi walivyokuwa wanateseka na ndio hulka ya masikini kuwa na furaha kipindi tajiri anapoteseka.
Kwangu Jiwe hawezi kuwa shujaa hata siku moja.