Wanajamvi,
Mara zote mataifa ya wenzetu, hata yale wafadhili mfano wachina na wamarekani, huwa wanatafuta rais ambaye yuko vizuri kwenye hitaji lao kuu la Taifa ambalo wananchi walio wengi wanakubaliana na lengo hilo na hivyo kumpata kiongozi atakayewafikisha kwenye malengo yao ya kitaifa.
Ni kweli tunahitaji sana viwanda ili tuweze kuwa na uchumi wa kati. Sera ambayo Rais aliyepo, ndugu Maghufuli, aliinadi kwa kupitia chama chake ccm. Hadi sasa hivi sioni tukielekea huko. Hatahivyo lengo kama sikosei ni kuwa Taifa lenye uchumi wa kati ifikapo 2025! Miaka chini ya sita kutoka sasa! Kiuhalisia, sidhani hata kama tumeshaweka hata misingi...
Kwa hali ilivyo ambapo ni vigumu kuhoji na hata kupata ripoti sahihi za wapi tumefikia kwenye agenda yetu hiyo! Ukiuliza, unaweza kuitwa msaliti au siyo mzalendo nk.
Lakini wananchi walio wengi, malalamiko yaliyopo ni kuhusu ukiukwaji wa wazi wazi kabisa wa sheria za nchi pamoja na haki zinazowalinda wananchi! Hakuna kipindi ambacho watanzania wamelilia utawala wa kisheria na mara nyingi katiba mpya kama ilivyo sasa. Matamanio hayo, yanaweza kuwafanya wakataka kuwa na rais ambaye atarudisha haki na sheria, kuwa nguzo kuu inapokuja kwenye uongozi. Kwamba anaweza kusimamia tukapata katiba ya wananchi kwa ajili ya wananchi na siyo katiba ya mtu mmoja ambaye anakuwa hahojiwi lolote mahali popote na yoyote yule! Ni kama Mungu mtu kabisa!
Hata mikataba mingi tunaingia hovyo hovyo na kuivunja hovyo hovyo, imesababishwa na hayo! Hakuna mfumo wa accountability ama uwajibikaji! jambo ambalo limetusababishia hasara kubwa chini ya tawala za ccm haswa uongozi huu uliopo.
Kuiweka kando kwanza idea ya viwanda, ni wazo la busara, tujipange, wenzetu ndivyo walivyofanya na si vurugu mechi! Ni muhimu ili nchi inyooshwe inavyotakiwa, ili tuweze kupata viongozi ambao watawajibika kwa wananchi waliomchaguwa na si vinginevyo!
Kwa namna ambavyo ccm imetuingiza ama imeliingizia Taifa hasara kubwa na hivyo kuendelea kuwa masikini, ni wazi kwamba ufisadi mkubwa uliokubuhu, chanzo chake ni mazoea ya kutokuwa watu wenye kufuata sheria za nchi kwasababu ya katiba mbovu inayomlinda mwenyekiti wa chama cha mafisadi ambapo anatokea kuwa na majukumu ya kuongoza wananchi wake wote bila ubaguzi wowote hata ule wa vyama!
Endapo “law and order” itakuwa ndiyo one of the main agendas uchaguzi ujao, basi honorary Lissu “is a good fit”
In matters of truth and justice, there is no difference between large and small problems, for issues concerning the treatment of people are all the same.
Albert Einstein
“We must maintain law and order at the highest level or we will cease to have a country”-Donald J Trump.