Website ya JATU naona picha kubwa ya Mzee Pinda na Waziri Mhagama

Website ya JATU naona picha kubwa ya Mzee Pinda na Waziri Mhagama

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ilikuja Q-NET tukaona Waziri Kigwangala akihusika ufunguzi wa ofisi

Ukienda Website ya JATU unakutana na picha kubwa ya Mzee Pinda na Waziri Mhagama.

Lakini mwisho wa siku ni wananchi kulia kutapeliwa pesa zao. Hawa viongozi wametumika kujenga imani za wananchi kutoa pesa zao.

Bado najiuliza tuna viongozi wa aina gani nchi hii ambapo watu wakubwa wanasapoti mambo ambayo mwisho wa siku yanatumika kutapeli watu.

Tunahitaji mwongozo katika maadili ya viongozi, mtu akishiriki katika jambo ambalo baadae linakuwa la utapeli akiwa kiongozi na kiongozi huyo achukuliwe hatua maana status zao ni vigezo vinavyotumika kushawishi watu kutoa pesa.

Naomba kuwasilisha
 
Viongozi wamealikwa kwenye taasisi zilizosajiliwa hawana makosa tatizo ni usalama wa taifa
 
Viongozi wamealikwa kwenye taasisi zilizosajiliwa hawana makosa tatizo ni usalama wa taifa
Sasa huoni mtu anaweza kuandaa ka upatu, hana business plan yoyote ilimradi akusanye pesa za watu na ili upige pesa vizuri unaalika viongozi.

Huoni hapa kuna shida

watu wanafanya colabo na viongozi ili kuwavuta wananchi vizuri.

na masikini mwananchi akiona waziri au mtu mkubwa kama Pinda anajua hawa ni waaminifu.
 
Back
Top Bottom