Wee Bocco una mpira gani unaokupa jeuri ya kunyamazisha watu wasiongee?

Wee Bocco una mpira gani unaokupa jeuri ya kunyamazisha watu wasiongee?

Goli la Leo la offside limembeba Boko na kuibeba kolowizard mbumbumbu fc! Bila hivyo mechi ingeisha kivingine, prison wanapaswa kulalamika! Timu zingine zikicheza na Simba ziwe macho na marefa wa mchongo! Zisikubali red cards, magoli ya offside na penati za bahasha!
Hii imeonesha Kuna mkakati maalum Yanga isibebe kombe msimu huu!
Huyu Mr Karai hafai kuongoza soka la bongo!
Chomoa taratibu utaumia
 
Bloo wangu siku hizi unazingua sana kwa vitendo vyako vya kujifanya kunyamazisha watu kisa umefunga tugoli, tena tugoli twenyewe twa offside na twingine beki kajifunga. Ukweli ni kuwa hakuna cha maana unachofanya uwanjani siku hizi, kazi kuwapiga vichwa na vikumbo wachezaji wenzio.

Nakushangaa sana, haujiulizi ulipokuwa hauchezi kwa nini watu walikuwa hawakulilii? U captain wenyewe sijui umepewa na Mangungu au Salim ndiyo unaokupa jeuri hiyo? Captain gani hana namba kwenye timu yake, yaani unaweza kwenda game 10 uko tu benchi na hakuna mtu yuko na time na wewe.

Ona Phiri tunayeamini kakuzidi kila kitu, mnafanya tu uswahili kumpiga pini ila kaingia tu dakika 2 kasaidia timu kupata goli. Hizi ni ishara za Mungu kuwazodoa wale wenye roho za korosho hapo Simba.

Mwenzio Kibu alipofanya ishara ya kunyamazisha mashabiki baada ya kumtungua Diarra, Baleke aliwahi kumzuia, wewe inaonyesha ni kama kamwinyi hapo Simba, hakuna wa kukukemea. Captain gani unakuwa na tabia mbofu?

NB: Siku hizi nimeamua kupumzika na mambo ya mpira naana kuna upuuzi mwingi ambao nimeshindwa kuendelea kuuvumilia.

Upunguza chuki Kaka
 
IMG_6524.jpg
 
Kwa mujibu wa kocha mkuu wa Simba Sc, Robertinho amesema mshambuliaji John Bocco pekee amekuwa akifanikiwa kucheza kwa maelekezo yake kwa kutumia muda mwingi kukaa ndani ya eneo la wapinzani faida ambayo imewapa nafasi ya timu hiyo kufunga mabao.

Kocha huyo amesema “Sikiliza, ni kweli naiona hiyo hali, mashabiki waje uwanjani kuangalia Simba inacheza mpira vizuri, Kwangu Bocco bado ni mshambuliaji mzuri kwani anakwenda kufanya kile ninachokitaka afanye,” amesema Robertinho na kuongeza;

“Hata katika mechi dhidi ya Power Dynamos aliingia akafanya nilichotaka tukapata bao lililosaidia kutuvusha makundi na juzi nimempa nafasi ya kuanza amefunga tena, lakini akawafanya mabeki wa Prisons kwa muda mwingi kubaki nyuma, nataka mshambuliaji wa aina hii anayekaa muda mrefu eneo la hatari la wapinzani na hili ndicho anafanya Bocco huyu bado ni bora kwangu.”

Kocha huyo amesema anayo washambuliaji wengine kama Jean Baleke na Moses Phiri ambao nao ni wazuri kwa kukimbia pembeni lakini wamekuwa hawajaweza kucheza kwa nidhamu kama anavyofanya Bocco.
.
“Simba tunajivunia kuwa na washambuliaji wengi wazuri, kwa Baleke na Phiri angalieni tu, muda mwingi wanataka kukimbia pembeni hili linatufanya kushindwa kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza tunaendelea kuwaongezea ubora huo na wao ili wacheze kama Bocco.
.
“Nimezungumza na Bocco nimemwambia aachane na mambo ya mashabiki anisikilize mimi kama kocha wake, mashabiki wanataka ushindi hesabu zetu ndio zitakazowapa furaha, unaona amefunga wamenyamaza nataka aendelee kufanya hivyo hivyo kila mara kwani nitaendelea kumtumia,” amesisitiza Robertinho aliyefikisha jumla ya mechi 15 bila kupoteza katika ligi kuu ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom