Wakuu, kama kichwa Cha habari kinavyojieleza, this weekend nitakuwa Kilwa(Lindi) nataka nitembelee hii miji mikongwe ya kilwa yaan kilwa Masoko na Kilwa Kivinje..
Naomba kufahamishwa maeneo ya kutembea na kubarizi bila kusahau Lodge nzuri za kupumzikia/kulala.
Utalii wa ndani kidogo...
Nchi yetu hii nzuri sana ila Kuna mafisadi wachache ndio wanaiharibu.
Maeneo ya kubarizi kilwa ni
1. Kilwa kisiwani, utaenda na boti za kukodi tokea bandari ya kilwa masoko.
2. Kilwa songomnara, pia huko utaenda na boti kutokea bandari ya kilwa masoko.
3. Kuna mawe maarufu ambayo kihistoria zilikua meli za uvamizi ila zilizogeuzwa mawe baada ya maombi ya Wana kilwa.
Pia huko utaenda kwa kukodi boti.
4. Kilwa kivinje huko Kuna bandari, pia Kuna makaburi ya ma chief waliouwawa wakipigania ardhi zao.
5. Kilwa kivinje Kuna mnara wa majina ya watu waliopigana vita vya maji maji, watu wengi hawajui kwamba vita vya maji maji vilianzia kilwa na kuishia songea.
kwenda huko utahitaji kuwa na gari binafsi.
6. Kuna mapango makubwa yaliyotumika kuficha watoto na kina mama kipindi Cha vita za wazawa na wavamizi
7. Kuna bandari kubwa maalumu kwa ajili ya uvuvi katika bahari ya Hindi.
Mambo ni mengi ila Nina hakika hayo yanakutosha.
Kuhusu hotel zipo za kitalii baharini ambao wastani gharama ni laki moja na kuendelea,
Pia Kuna lodge za kawaida zilizopo kilwa masoko stend na kilwa kivinje gharama kuanzia elfu 15 na kuendelea.