Hello rafiki. Uzito uliokithiri umekua challenge katika kizazi chetu cha leo. Kumekuwa na njia mbalimbali za kupunguza uzito zingine kwa fad diets na zingine za long term plans.
Mojawapo ya njia mashuhuri ambayo imetamba hivi karibuni inaitwa intermittent fasting (IF), ambayo ni kula na kuacha kula kwa masaa kadhaa. IF ziko za aina nyingi ila ntazitaja baadhi.
Kuna moja ya 16/8 ambayo mtu unatakiwa kula ndani ya masaa nane na kuacha kula ndani ya masaa 16 kwa siku. Chakula hicho kinatakiwa kiwe cha afya tafadhali. Pia ni muhimu kuzingatia wingi wa chakula au portion.
Kuna nyingine ya 18/6, 20/4, na 23/1 zote hizo ni kula na kuacha kula kwa masaa yaliyo mengi zaidi.
Leo nitaongelea hii ya 23/1 ambayo inaitwa One Meal A Day. Hii inahusu kula ndani ya lisaa limoja na kuacha kula ndani ya masaa 23. Hivyo kwa siku moja unakula mara moja. Ni njia mojawapo nzuri sana ya kupunguza uzito uliokithiri lakini pia ina faida nyingi ikiwemo clear mind, improving attitude, raising self esteem na kadhalika.
Yeyote atakaependa kujiunga hapa ili tuifanye pamoja lengo likiwa kuitengeneza miili yetu kwa faida zetu na wanaotutegemea. Tutakuwa tunaupdate wapi tumefika kila baada ya mwezi mmoja ili kuinspire wengine. Kwa maoni na ushauri mnakaribishwa tuelezane.
Come one come all. Welcome
29 june: 108kgz
31 july: 103.5kgz