Weka hapa uchambuzi wa kitaalamu kuhusu ligi yetu.

Weka hapa uchambuzi wa kitaalamu kuhusu ligi yetu.

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Nimeona Kuna haja wakati mwingine kuweka ushabiki pembeni na tuichambue ligi yetu kiweledi na kitaalam.

Kwa mfano mara nyingi ni watu wachache sana hutueleza ni Kwa nini wanasema timu Fulani ni dhaifu ama imara.

Wachambuzi kama Ramadhani mbwaduke huleta ladha ya uchambuzi Kwa kuwa hutumia takwimu.

Hapa JF nimegundua tunao watu wa kutosha wenye uwezo wa kuichambua ligi yetu kiweledi na kitaalam lakini wamepofushwa na ushabiki wa Simba na Yanga.

Thread hii utumike kuchambua ligi yetu Kitaalam na kiweledi ili tusio na ufahamu mpana wa Mpira wa miguu na sisi tufaidike.

Kwa mfano jee kila mchezaji anayetoka nje ya nchi yetu ni bora zaidi kuliko wachezaji wetu? Kabla ya kusajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania vilabu vyetu vitumie vigezo gani ili kupata wachezaji wanaostahili kusajiliwa?

Mifumo ya uendeshaji wa vilabu vyetu unaweka mazingira ya uendelevu?

Kwa nini waamuzi toka kwenye ligi yetu huwa hawachezeshi mashindano ya kimataifa?

Na mambo mengine mengi yahusuyo ligi yetu.
 
Yanga Bingwa.
 
Simba na Azam wanashinda kiuwezo na wanashindwa kwa kuzidiwa

Kuna timu ya kuitwa Yanga Game nyinginzinazoonekana ni ngumu kwao jamaa wanashinda kwa utata mkubwa hasa kwa kubebwa na waamuzi au kwakutoa rushwa kwa wacheza hasa mabekinna makipa
 
Ligi ya Nbcpl inakuwa ukilinganisha na miaka ya nyuma kutok na uwekezaji wa wadhamini wa ligi,uwekezaji huu bado hauzinufaishi timu zingine za madaraja ya chini kwenye ligi ukizitoa Simba,Yanga na Azam kidogo ya hiyo Singida inayouzwauzwa.

Ligi bado ipo mikononi mwa Simba na Yanga kutokana na mapenzi makubwa na nguvu ya mashabiki wake...uwekezaji wao unazifanya timu zisizo na uwezo wa kifedha kubaki kama washiriki na sio washindani,TFF wana kazi ya kuifanya ligi iwe shindani hata kwa timu 10 tu,maana kuna mechi unaona Timu kongwe zina uhakika wa kushinda karibu kila mechi ispokuwa wanapokutana wao kwa wao sasa hii haileti ladha ligi kuwa ya timu mbili tu......ningependa siku moja timu zisizopewa nafasi kufanya vizuri na kubeba ubingwa kama walivyofanya Mtibwa.
 
Nilikuwa nawaangalia Pacome, Chama na Mohamed Hussein wakifanya mazoezi ya Gym wakisimamiwa na Mwalimu wao Denzel, imeniwazisha Sana.

Je ni timu Gani nje ya Azam, Yanga na Simba ambao wachezaji wake wana fursa kama hizo?

Wachezaji wa timu hizo nyingine zinazoshiriki ligi kuu ambao hawana waalimu wa Gym au hata hizo Gym hawana, wanapokutana na kimisuli (Physically) na wachezaji wanaoshinda Gym, watatoshana?
 
LIGI INAKUA TENA INAKUWA KWA KASI SANA.... ILA NASIKITIKA TU TIMU ZINAZOKUWA SAMBAMBA NA KUKUA KWA LIGI NI MBILI TU BASI.

Leo hii wachezaji wengi wa kiafrika wanatamani kwa huu ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara, kama sio Afrika kusini basi ni kuchezea hapa kwenye ligi yetu, haya ulizia timu zipi wanazotamani kuchezea? Hakuna timu nyingine zaidi ya mapacha wa Kariakoo na kwa mbali labda Azam......!! Hii maanisha kwamba timu zetu zingine hazina thamani kabisa ya kuwavutia hao wachezaji wanaotamani kucheza kwenye ligi yetu.

Halii ni tofauti kabisa na ligi ya afrika kusini, ambapo wachezaji wengi wanaotamani kuchezea kule wako tayari kuchezea hata kwenye timu za madaraja ya kati kama Chipa united,Amazulu,Royal AM n.k, hii ni kwa sababu vilabu vinavyoshiriki ligi ya afrik kusini vinathamani sawa na ligi yao, na hii kazi inafanywa hasa na shirikisho lao la mpira.

Kwetu sisi hapa TFF wako kwa ajili ya kuangalia na kuboresha maslahi ya mapacha wa kariakoo tu basi na ndio maana ndio timu pekee zinapanda thamani kila kukicha, na wala hawana habari kabisa na timu zingine 14 zilizobaki... hawana mikakati yoyote ya maana kuweka mazingira mazuri yatakayoinufaisha kila timu inayoshiriki ligi kuu.

Na kutokana na incompetence hii iliyopo Tff tutaendelea kuwa na ligi dhaifu hivi hivi huku tukiamini kwamba ni bora na wakati ubora wake umeelemea kwenye timu mbili.
 
Muhimbu kama ni hivyo, jee timu nje ya Simba na Yanga zifanyaje kuvutia wawekezaji?

Maana hizi timu mbili ni kama vile mfumo unakataa zisifungwe na timu zingine. Sasa mwekezaji anawezaje kuwekeza kwenye timu isiyo na mafanikio?

Au mwekezaji gani ndani ya Tanzania ambaye hana uchembechembe wa U-simba na U-yanga?

Nakumbuka Alex Kajumulo alijaribu kuwekeza...
 
Back
Top Bottom