Weka picha ya gari namba 'E' kuonesha utajiri wa Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mimi nimeishia la saba B, hivyo siwezi bishana na mwenye PhD. Leo nilikuwa natembea nikaona gari kadhaa za namba E, nimezipiga picha. Kwa wengine kama mkiyaona yapigeni picha kuonesha utajiri wa watu wa nchi hii.

Pia kama ukipita bar au club piga picha nyomi tuone utajiri wa nchi.
 
Ukisikia namba E ujuwe kapiga mihogo na Maji yaani ni mlo wa Kuungaunga siku ipite

Kaya nyingi mjini ni kulegezea kwa Namba E ili mradi KUKUCHE

Mtu akikuambia niko namba E ujuwe hali tete mfukoni....new code ya KITAA
 
Eeh!!! Ina maana jamiiforum ina watu wajinga kiasi hiki???
Amekuambia yeye ni la saba B na hawezi kushindana na mwenye PhD. Ukitafakari alichoandika utagundua yeye sio mjinga bali ametumia lugha flani hivi ya kuwakilisha.

Ukimjua huyu mwenye PhD alisema nini kuhusu gari namba E nadhani ndo uta-conclude kama mleta uzi ni mjinga au mwerevu
 
Ukiacha siasa alichosema Mwigulu alikuwa sahihi, watu hawawezi nunua gari kwa fujo hiv kama hakuna pesa mtaani,
Tazama jinsi namba E inavyokwenda speed, tena sio gari za ovyo, ni Subaru, dualis, outlander, Mazda C5 na nyingine za hivyo
 
Fujo umeiona wapi hiyo ya kununua magari mzee mbona Njombe hapa hakuna hata duka la hayo magari
 
Unaishi wapi mkuu? Huko ulipo ni chache sana? Huku nilipo Namba E ni nyingi sana nikianza kuzipiga picha kila nayokutana nayo inabidi nisifanye kazi yoyote
 
Kwakweli Tanzania tuko uchumi wa Kati huku kwetu namba E nyingine tayari zipo Garage zimetelekezwa nadhani wanunuzi wanasubiri namba F tuingie uchumi wa Juu!!
 
Ukiacha siasa alichosema Mwigulu alikuwa sahihi, watu hawawezi nunua gari kwa fujo hiv kama hakuna pesa mtaani,
Tazama jinsi namba E inavyokwenda speed, tena sio gari za ovyo, ni Subaru, dualis, outlander, Mazda C5 na nyingine za hivyo
Ameongea utumbo mtupu...ukiangalia walionunua hizo ulizozitaja apo hizo zote kama sio used cars basi robo tatu ni used cars..huwezi pata zote ni mpya,ukiona unapenda gari na bado huna uwezo wa kununua brand new basi jua bado upo kwenye kundi la umaskini
 
kupiga picha bila ridhaa ya mpigwaji ni kosa kisheria...
Tii sheria bila shuruti πŸ’
 
Ikifika namba z mnijulishe huku hakuna magari tuna mikokoteni ya kuvutwa na punda na ng'ombe
 
Kabaka mada huyo, mleta Uzi ana akili kama mchwa!
 
Fujo umeiona wapi hiyo ya kununua magari mzee mbona Njombe hapa hakuna hata duka la hayo magari

Mzee, usituaibishe watu wa Njombe kiasi hiki, please πŸ™πŸ™πŸ™ nakuomba sana, hayo maduka hata Dar tu yanafungwa, watu wanafanya kuagiza online, hakuna haja ya maduka ya physical
 
Sasa mzee kwa uchumi wa Tz hata hizo hizo used za 15-30M zinaponunuliwa sana zinaonyesha uchumi umepanda, no way waTz from no where tukaanza agiza chuma za 0km kwa 200M +
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…