Weka siasa pembeni, tafakari "credibility" ya Mamlaka za Serikali katika sakata la CHADEMA

Weka siasa pembeni, tafakari "credibility" ya Mamlaka za Serikali katika sakata la CHADEMA

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Mnyika anasema...

Uhakika nilio nao, hao 19 walioenda kuapa, walishirikiana na ofisi za NEC, pamoja na Bunge kughushi nyaraka za chama, kujiteua bila kikao na kujipeleka kwenda kuapa. Huu ni USALITI mkubwa. Wote 19 wanafahamu orodha haiwezi kwenda NEC bila kupitishwa na Kamati Kuu ikiwa na saini ya Katibu Mkuu na mihuri ya chama. Na mimi sijasaini wala Manaibu wangu. Sasa NEC watueleze hiyo orodha waliyopewa ina saini ya nani?

Kughushi ni jinai. Na ni jambo la aibu kama Ofisi ya Bunge na Tume ya Uchaguzi wanaweza kushirikiana na watu wachache ndani ya chama kufanya jinai ya kughushi kwa maslahi yao wenyewe. Naomba wanachama wa CHADEMA, mtoe maoni yenu ni hatua gani zichukuliwe dhidi ya akina Halima Mdee na wenzake. Maoni hayo yawasilishwe kabla ya kikao cha kamati kuu Novemba 27.

Ieleweke hawa sio wabunge wa CHADEMA. Ni wanachama wa CHADEMA walioamua kutumia mwavuli wa Chama kunajisi heshima zao na heshima ya chama chao. CHADEMA hatuwatambui. Ni wabunge wa Viti Maalum kwa matakwa ya CCM, ni Wabunge wa NEC na ni Wabunge wa Spika Ndugai. Kwa ujumla CCM imeamua kujiundia kambi yake ya upinzani Bungeni ili kuokoa Trilioni 2 za wafadhili zisipotee."

Moja ya mambo ya msingi katika nchi huru kujenga taasisi imara ambazo hazitegemei mtu bali mifumo imara itakayofanya taasisi isimame hata asipokuwepo fulani.

NEC, DPP, Bunge n.k wanahusishwa katika jinai. Tafakari kama Tanzania ina taasisi na mifumo au kitu gani?
 
Serikali inazalisha na kufundisha Wanasiasa na Raia kuwa sio wazalendo. Taifa letu la kesho halitakua na viongozi wazalendo.

Serikali inavyotengeneza sinema za kununua (Kwa rushwa) wapinzani na kwa vitisho, inafundisha na kutuaminisha kwamba siasa ni kujali tumbo lako pia vita dhidi ya Rushwa haishindikani.

Vyombo vya dola (hasa vya usalama) vime lawitiwa na viongozi wachache baada ya kujitoa kwenye mfumo wa vyombo vya Usalama na kua vyombo vya siasa, credibility imekufa, division of power/delegated legislation hakuna, havina hadhi tena kama vyombo vya usalama, na hakuna raia anaeviamini kwasasa hivi.

Imefikia hatua raia wanashindwa kutofautisha kati ya kuwa Askari polisi na vibaraka wa CCM raia wanaona askari ni kibaraka na sio mtu wa kumwamini. Kwasababu jeshi la polisi limekubali kutumika kisiasa.

NB tumeshudia OCD wakiimba mapambio ya CCM. Na hakuna hatua za kinidhamu walichukuliwa.

Hii, tunajenga uadui ndani ya Taifa. na hakuna vita mbaya kama kujenga uadui wa ndani (Katika familia, ni rahisi kupambana na adui wa nje ya familia, kuliko kupigana na adui wa ndani ya familia).

Uadui wa ndani ya taifa ni njia rahisi ya kuruhusu maadui wa nje ya taifa.

Serikali isilalamike kama inavyopenda kulalamika "Kuna baadhi ya watu sio Wazalendo wa Nchi yetu" Yenyewe ndio inazalisha hao watu, yenyewe ndio inaharibu uzalendo kwa raia, yenyewe ndio inajenga chuki na kuvunja uaminifu kwa raia.

Yaliofanyika jana ni kashfa kubwa kitaifa na duniani. TISS, Polisi, TAKUKURU wanatakiwa watoe majibu ya kuridhisha kwa Wanancu na Dunia"Kukaa kimya, raia na dunia tutaamini wamehusika katika uvunjifu wa Sheria na Katiba ya Nchi.

Cha kujiuliza:

Uchafu huu wote pamoja na kuliangamiza taifa, unafanyika kwasababu gani?

Jibu, kwaajili ya viongozi wachache wa CCM (Wasiojali wala kuogopa amani ya nchi kuvunjika, raia kufa, taifa kuangamia) wenye tamaa ya kushika madaraka kwa miaka 5 ijayo.
 
OKW BOBAN SUNZU,

Acha vitisho huelewi chochote kwenye siasa na huna uwezo wowote wa kushawishi kisheria kutengua

Nilitaraji utamsema vibaya mwenyekiti wa chama maana ndiye aliyetajwa kubariki wabunge hao kwenda bungeni lakini unarukaruka tu eti ni usaliti, saini ya nani ipo kwenye nyaraka, mara NEC, DPP wamekula njama, you are just barking like local dog which when intimadated by the master he draws the tail under the belly.
 
Absolutely!
 
Serikali inazalisha na kufundisha "WANASIASA NA RAIA" kuwa sio wazalendo. Taifa letu la kesho halitakua na viongozi wazalendo.

Serikali inavyotengeneza sinema za kununua wapinzani, inafundisha na kutuaminisha kwamba siasa ni "KUJALI TUMBO LAKO".

Vyombo vya dola (hasa vya usalama) vime lawitiwa na viongozi wachache baada ya kujitoa kwenye mfumo wa "VYOMBO VYA USALAMA" na kua "VYOMBO VYA SIASA", credibility imekufa, havina hadhi tena kama vyombo vya usalama, na hakuna raia anaeviamini kwasasa hivi.
point
 
OKW BOBAN SUNZU,

Acha vitisho huelewi chochote kwenye siasa na huna uwezo wowote wa kushawishi kisheria kutengua

Nilitaraji utamsema vibaya mwenyekiti wa chama maana ndiye aliyetajwa kubariki wabunge hao kwenda bungeni lakini unarukaruka tu eti ni usaliti, saini ya nani ipo kwenye nyaraka, mara NEC, DPP wamekula njama, you are just barking like local dog which when intimadated by the master he draws the tail under the belly.
Labda uniambie nisubiri serikali ijibu (majibu yasiyo na mashaka na ushaidi) Kuhusu Mbowe kutajwa sio hoja kwani hata wewe hapo ulipo unaweza kumtaja bila madhara yeyote. Niamini vipi wakati katibu wake ametamka kwamba hausiki na ameitisha kikao kuwajadili waliomtaja?
Tujadili kwa hoja mkuu
 
OKW BOBAN SUNZU,

Acha vitisho huelewi chochote kwenye siasa na huna uwezo wowote wa kushawishi kisheria kutengua

Nilitaraji utamsema vibaya mwenyekiti wa chama maana ndiye aliyetajwa kubariki wabunge hao kwenda bungeni lakini unarukaruka tu eti ni usaliti, saini ya nani ipo kwenye nyaraka, mara NEC, DPP wamekula njama, you are just barking like local dog which when intimadated by the master he draws the tail under the belly.
Kauli za wababe
 
Ukweli mmekwama,vijambio vyenu havisafishiki
Subiri kauli ya kamati kuu,ili muwatete kama mlivyofanya kwa silinde na lijua likali
Hapo mtakuwa mmejipaka siyo tope bali mavi usoni.
 
Usirushe mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo siku akina mama wakiamua kujibu sinema za CDM zinavyotengenezwa akutokalika au wakiamua kumu expose Lissu for what he is.

Mwisho wa siku wao ndio wako mstari wa mbele kupokea virungu na kulala jela. Fatma Karume, Kigogo na Maria Sarungi wao wako Twitter waingie ulingoni kama wenzao halafu ndio waongee.

Alichokifanya Mdee na makamanda wenzake wao ndio wanajua uchungu wa sauti zao kuminywa sio nyie keyboard warriors.
 
Back
Top Bottom