Wekeni akiba ya maneno. Miaka 100 ijayo mawazo yenu yatachekwa sana

Wekeni akiba ya maneno. Miaka 100 ijayo mawazo yenu yatachekwa sana

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Wanajamii,

Leo nafanya kuwakumbusha tu, siku hazigandi huku mbeleni miaka mia ijao kizazi cha wakati huo kitakuwa na fikra tofauti sana na zetu. Hivyo basi nyie watu ambao akili zenu mmezifanya mgando, hazishauriki na kubadilika ili kwenda na wakati. mtachekwa sana. Maana kwa wakati huo history itawakumbuka kwa jinsi mlivyokuwa watu wenye mawazo ya kale.

Ipo hivi, kama ambavyo baathi yetu tunavyoona uduni wa kimawazo kwa wazee ambao walikuwa hawataki mwanamke asome, afanye kazi, awe na pesa zake, ndivyo hivyo hivyo tutakavyoonekana kwenye maswala kama dini, msimamo kuhusu mapenzi, ukabila.

Huko mbeleni hizi data tunazoziacha mtandaoni kutakuwa na watu kazi yao special ni kuzisoma kuzifwatilia na kuzidadavua. Hivyo kuna baathi ya watu mtakuwa case study kama ambavyo Hilter na wengine wanavyosomwa nanyi mtakuwa hivyo hivyo.

Shida kubwa tuliyonayo wanadamu hatuwezi kujua mambo yote kwa wakati mmoja hivyo mara nyingi tunakuwa. Tumeshapitwa na wakati pasipo kujua.
 
Kila zama na kitabu chake,huwezi kua na mawazo ya mwaka 2023 ili kuja kumfanya mtu atakayekuja baada ya miaka 100 akubaliane na wewe,New generation itachukua itakachoona kina manufaa kwao kwa wakati huo,na wao pia watakuja kuchekwa baada ya miaka 100,Dunia inazunguka ni vitu huendana na muda husika.
 
Back
Top Bottom