Wekeni Resume (CV) za J Makamba, J Mnyika, Z Kabwe na L Nyarandu

Wekeni Resume (CV) za J Makamba, J Mnyika, Z Kabwe na L Nyarandu

Going forward you better not complain about any mwanasiasa....

I actually, siezi ku-complain kuhusu wanasiasa, najua wengi wao ni waganga njaa au wajasiriamali. Watu kaa wewe mnaowatumainia wanasiasa ndio wa kubeba lawama.

Nimeona hapo kuna thread inasema mgombea urais asitumie zaidi ya bilioni 1. Nimesikia hata uvivu kufungua kuona yaliyomo. Hivi ktk hali ya kawaida mtu ata-splash 1 billion Tsh bila kula faida huko mbeleni?
Hiyio nawaachieni nyie mnaodhani siasa itajenga nchi.
 
Basi hata wewe unapiga kasia kwenye nchi kavu..What are doing hapa JF..you might as well ishia kwa michuzi kuanangalia picha...
What do you mean by "kazi ya kitaalauma"...hawa ni watu ambao kwa kura yako unawapa ajira....kama wewe ni muajiri kwa nini usijue resume ya mtu.

nadhani mtu anayeangalia habari za ze fulanaz na ze mikonozz kwa Br. Michu ana nafuu zaidi kuliko mtu anayetegema kuvuna madafu kwa kupanda chelewa.

btw, kazi za kitaaluma maanake kazi mtu alizo-specialize. ulikua na hili mbado? yaani anaeza kusimama akahesabiwa ktk wataalamu wa fani husika yenye mchango kwa humanity.
 
Kwa staili hiyo ni ngumu kuendelea.

Politks ni kazi inayoendana na cv, otherwise tutabaki kama tulivyo. Politks si uwezo wa kupiga propaganda.Politks ni uwezo wa kubuni, kuuwezesha ubunifu na hatimaye kuupitisha ktk nyoyo za wananchi.Hivyo kazi hii inahitaji kwenda sambamba na cv.

mmhh..naona wewe hasa ndio mwenye mawazo ya kutoendelea. hivi mwanasiasa anaeza kuwa mbunifu kuliko wenye kusomea hayo mambo kwa undani? kaa ndo hivo tunavofikiri kuwa wanasiasa wana theory of everything no wonder tunaenda backward badala ya forward, na ndo maana kipenzi chenu Vasco Da Gama alishawahi kusema hajui chanzo cha umaskini wa waTz halafu mnamshangaa..
 
MkapaP,

Embu elimisha hawa wenye mawazo mgando maana hawaeleni nini maana ya cv na umuhimu wake....

Wewe ndo hujui maana ya CV. Ukisoma maana ya CV ni kwamba ni kifupi cha historia ya mtu ktk fani fulani, na unashauriwa unapoforward CV yako iendane na malengo ya kuituma hiyo CV...yaani relevant expertise na experience. sasa usizidi kujivua nguo hapa tafwadhal.
 
kuna mtu ana CV nzuri kama ya Chenge? CV ya Kikwete inakubalika, na sawasawa na ya Marmo.. kwa vile mnataka kupiga pita kwa kuangalia uzuri na kilichojazwa kwenye CV muangalie sana mnaweza kujikuta mnachagua Wanigeria!
 
Well.....Chenge has "resigned from cabinet" on his CV now. Atakae mchagua bila kujiuliza kwa nini alijiuzuru ni mjinga. Pia JK ana "rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Siku akitaka nafasi nyingine una angalia track record yake kama raisi.
 
Naona wananchi wanataka kufanya 'vetting' kupitia CV. Ushauri wa bure: tuwapime kupitia matendo yao na uzalendo wao kwa nchi hii na hasa katika miaka 5 iliyopita.
 
Naona wananchi wanataka kufanya 'vetting' kupitia CV. Ushauri wa bure: tuwapime kupitia matendo yao na uzalendo wao kwa nchi hii na hasa katika miaka 5 iliyopita.

Naona watu wana shindwa kuelewa CV ni nini. Sasa hayo matendo yake ktk miaka mitano ni nini? Ubunge si tayari CV hiyo? CV itasema alikuwa mbunge from yr X until yr Y. Hapo mwananchi unaangalia kafanya nini katika ubunge wake. Au jamani tuanza kuulizana CV ni nini na mantiki yake ni nini?
 
Tunahitaji kuweka CVs(resumes) za January Makamba,Lazaro Nyalandu,Zitto Kabwe na vijana wengine wote watakao kuwa wanagombania public office ili tufanye upembuzi yakinifu..na kuwaeleza nini tunahitaji toka kwao....
toa boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako!! na hiyo CV yako tunaitaka ili tujue huyo mpembuzi yakinifu ana uwezo gani!!!
 
Siku zote watanzania tumekuwa wa kwanza kupoint fingers!! tunakua wa kwanza kutarajia fulani awe responsible kwa jambo fulani, post ya mstahiki imejionyesha au inanifanya kuamini kwamba yeye ameshajipa right ya ku-review hizo CV akitegemea kuna mawgiji wenine humu watajoin kumsaidia... narudia tena, tunatarajia sana wengine watufanyie au wafanye kwa niaba

its a very bad disease na mbaya zaidi ni chronic!!

Back to mada!! nadhani kuna threads nyingi sana zimeshaweka wazi hawa watu na wengi wa wanasiasa wetu, wazuri kwa wabaya... nijuavyo mimi CV ni wasifu ulioandikwa kitaalama ina as specific format kufit purpose fulani, na kama ni hivyo basi CV zao zimeshwekwa wazi kufit purpose yetu

sioni umuhimu wa kuweka CV, labda mtoa mada atufanyie majumuisho ya wasifu za hawa wanasiasa na kuziweka hapa... hiii pia itatusaidia kuweza kumpa credits zake za kupembua kiyakinifu uwezo wa baadhi ya wanasiasa

bila hivyo tutakua kulekule kwenye siasa za maji taka, kwisha!!
 
Mi namshangaa ati..

Kaa ananafasi ya kazi ya kitaalauma anataka kuwapa awatafute huko kwa muda wake wampe hizo CV, otherwise hapa anachofanya ni kupiga kasia kwenye nchi kavu.
Cv zao ndo zisaidie nini?
Wapo Dkt Benjamin Mkapa
Dkt Jakaya Kikwete
Prof Kapuya
Dokta Mahanga
Prof. Magembe
Dkt Nchimbi
Dkt Kawambwa
Dkt. so so so and so so so........+ Professa so soso

Wamechangia nini hao kwenye maendeleo ya taifa letu kupitia SI-HASA?
 
I actually, siezi ku-complain kuhusu wanasiasa, najua wengi wao ni waganga njaa au wajasiriamali. Watu kaa wewe mnaowatumainia wanasiasa ndio wa kubeba lawama..

Sounds like sizitaki mbichi hizi.....

Nimeona hapo kuna thread inasema mgombea urais asitumie zaidi ya bilioni 1. Nimesikia hata uvivu kufungua kuona yaliyomo. Hivi ktk hali ya kawaida mtu ata-splash 1 billion Tsh bila kula faida huko mbeleni?

Kaka umewahi kufanya utafiti kuhusu gharama za kufanya shughuli za uchaguzi pamoja na kampeni? Yaani utafiti wagharama halali kabisa bila ya rushwa ama takrima? Kama tumekubali demokrasia ya ushindani (wanaita demokrasia ya vyama vingi) ni lazima uwe tayari kugharamia mahitaji yanayotokana nayo. Kulalama kuwa shilingi bilioni moja ni kiwango kikubwa kwa kampeni ya urais kunaonyesha jinsi gani watanzania wasivyokuwa na imani na viongozi wao, wanasiasa, asasi za uongozi na utawala na hata wao wenyewe. Na hali kama hii ni sumu kubwa kuliko hata sumu inayosambazwa na ufisadi, udini, ukabila, umasikini,ujinga na hata magonjwa......

omarilyas
 
Sounds like sizitaki mbichi hizi.....

Kivipi?

Ok, binafsi sikuelewi unakoelekea..

sasa unataka nitafiti gharama za uchaguzi ili iweje?

hivi ni wapi nimelalama kuhusu hizo 1 bilioni? hoja yangu haiko kwenye gharama per se...ipo kwenye dhana nzima ya siasa na chaguzi. najaribu kubainisha kichwani kwangu hii inaezekanaje mtu aingie gharama lukuki bila ya kuwa na prospects za kurudisha fedha zake huko mbeleni. for what really? a matter of simple maths.

pia una ongea kwa ku-assume nasapoti hizi sarakasi zenu mnazoita uchaguzi+siasa(?) kwa kifupi sielewi unakoelekea au unataka kusemeje, maana maelezo yako yanaishia hewani.
 
Wasf unatosha kwa mwanasiasa..CV nadhani ina maana na matumizi tofauti..ingawa inaweza kuwa sehemu ya wasf

Tazama definition hii ya wikipedia

A résumé is a document that contains a summary of relevant job experience and education for specific employment search. The résumé is typically the first item that a potential employer encounters regarding the job seeker and is typically used to screen applicants, often followed by an interview, when seeking employment. The résumé is comparable to a curriculum vitae in many countries, although in Canada and United States it is substantially different

Sasa sijui tunataka CV za hawa wakubwa za nini...
 
mimi naona kama tunaenda mbele na kurudi nyuma....wengi wa watu hawa uliowataja hapo kwenye headin ya thread ni kwamba tayari wanajulikana na mtu kama lazaro na kabwe lazima cv zao zipo kwenye website ya bunge, mtu kama January na Mnyika wamekuwa wakisikika na taarifa zao zipo na pia wamejadiliwa sana hapa na hata kwenye blog nyingine...
sipingi suala la kupata CV zao kwani CV inaweza ikakupa picha ya mtu kabla hujampa nafasi yeyote iwe kazi madaraka nk, kwahiyo kuliko kuendeleza mjadala wa maana ya cv basi zingeletwa tu kama zipo maana najua baadhi ya walengwa watafurahi pia katika namna ya kujiuza....
 
kuna mtu ana CV nzuri kama ya Chenge? CV ya Kikwete inakubalika, na sawasawa na ya Marmo.. kwa vile mnataka kupiga pita kwa kuangalia uzuri na kilichojazwa kwenye CV muangalie sana mnaweza kujikuta mnachagua Wanigeria!

Bado nafikiri hatuelewi maana ya CV ama mie sielewi ndio maana tuko hapa kuelimishana.

CV sio tu kuandika nimesoma havard na nimekuwa mwanasheria mkuu, ok ukiandika hayo ili CV ikamilike inabidi ueleze archviements zako kwa kipindi hicho.

Mtu anaweza fanya kazi miaka miwili akawa na archvievements kubwa kuliko wa miaka 30. Unawekewa tick kila kipengele na inatafutwa average.

Chenge na viongozi wengi ukiipa maksi CV yao nafikiri ita kuwa kati ya minus na 1. Binafsi nitashangaa kama mkisema Chenge ana cv nzuri.
 
hivi ni wapi nimelalama kuhusu hizo 1 bilioni? hoja yangu haiko kwenye gharama per se...ipo kwenye dhana nzima ya siasa na chaguzi. najaribu kubainisha kichwani kwangu hii inaezekanaje mtu aingie gharama lukuki bila ya kuwa na prospects za kurudisha fedha zake huko mbeleni. for what really? a matter of simple maths.
Mwanasiasa halisi(i mean halisi) haangalii faida ya pesa kurudi mfukoni mwake anaagalia maendeleo ya wananchi wake kama barabara, hospitali, shule nk
 
Nafikiri wengi hapa hatujui maana ya CV au resume wataalamu wanasema CV nzuri isizidi 2 pages A4 paper maana CV haiajiri mtu inasaidia kushort list applicants kinachoajiri ni interview inategemea jinsi utakavyojieleza unaweza ukawa na CV nzuri lakini ukafeli interview

Sasa kwenye CV ya page 2 sitegemei kama utaeleza achievemets zako zote za miaka 20 vinginevyo kitakuwa kitabu na ukiweka maelezo mengi kwenye CV interviewers wengi huwa hawasomi wanatupilia mbali
 
Mwanasiasa halisi(i mean halisi) haangalii faida ya pesa kurudi mfukoni mwake anaagalia maendeleo ya wananchi wake kama barabara, hospitali, shule nk

aah wapi..bahti mbaya mie sio mdanganyika..endeleeni kudanganyana na siasa zenu.
 
Back
Top Bottom