Wekeza Milioni 7 upate Milioni 20 ndani ya miezi 6

Babavos

Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
93
Reaction score
242
Salamaleko,

Shalom. Kama tunavojua kipindi hiki kwa maeneo ya vijijini ni kipindi cha kuvuna mazao na kuna niliko mimi kwa sasa debe la mahindi lina 7000 na debe la mpunga lina 5000. Maana yake gunia la debe sita la mpunga ni 30000. Na gunia la mahindi la debe sita linasoma 42,000.

Kama una mtaji wa kununua mpunga kwa kipindi cha mavuno basi una uhakika wa kuingiza mil 20 kwa mtaji wa mil 6 kwa muda wa miezi 5 (UHAKIKA)

MCHANGANUO
Gunia la mpunga 30,000 unanunua gunia 200 jumla inakuja 6,000,000 kwenye million 7 inakua imebaki million 1 kwa ajili ya kukava gharama za ukusanyaji na mambo mengine madogo madogo.

Huu tupo mwezi wa 5 ikifika mwezi wa 10/11/12 gunia la mpunga linafika 100,000l= kutoka 30k ya sasa.

Sasa una gunia 200 stoo zidisha 100,000 kwa kila gunia mzigo utasoma 20,000,000/= ukitoa mil 7 uliyowekeza UNABAKI NA 13,000,000/=KAMA FAIDA KWA MIEZI SITA (6) WOOW

NB: Ni bora kununua mpunga kuliko mahindi sababu mpunga hauna gharama sana kwenye kutunza kama mahindi

UKITAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI UKU NILIKO KUNA FURSA NJOO TUWEKEZE

Ushauri maoni kurekebishana ruksa, nawakaribisha.
 
Ok
 
Ni wapi huko?
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]. Sie ndo biashara yetu hiyo kwa miaka 6 sasa na sijawahi pata hiyo faida[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]. Eti ununue mpunga 30k uje uuze 100K. Ni fix juu ya fix. Hujui kitu kaka kuhus biashara. Hii biashara inategemea na vitu vingi sana nikianza kuvisema tutakesha.

Faida pekee niliyowahi ku enjoy ni kuwekeza 5m na kupata 8m tena ni zali tu. Jua linakuja baada ya muda mwingi kupita tena bila kujua. Inshort ni biashara ya ups and downs nyingi. Nikikwambia changamoto zake utabaki mdomo wazi
 
Kununua gunia tupu 500/=
Kupima na kushona 200/=
Kutoa mzigo porini kuleta stoo 10,000/=+
Ushuru njiani 2000/=
Wapakiaji 300/=
Kushusha na Kupanga stoo 500/=
Hifadhi ya stoo 10,000/=
Kijana wa kukusanya 1000/=
Uhalibifu 500/=
Cost ya kila gunia Jumla Tsh. 25,0000/=+ 30,000 ya manunuzi ,= 55,000/=

Hapa bado gharama za kukaa kijijini kula na kulala.
Bado vibali/leseni ya Mazao kama laki 7 au 6.
Bado tips za madalali na viongozi wa Vijiji kwa kifupi hii kazi usiichukulie poa Field ina wenyewe.
 
Ingekuwa rahisi kila mtu angefanya na matajiri wangekuwa wengi. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Gunia la mpunga elf 30?
Utakua upo usingizini unaota wewe
 
Na wenyewe ndo tupo kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…