AGROPRODUCT
JF-Expert Member
- Apr 2, 2023
- 290
- 952
Inawezikana kabisa mfano ipo mingi sana, Mwaka huu hiyo 7Milioni unaweza kupata 20+ Milioni ,hawa watoto wa 2000 yaan wanachukulia maisha ni note book kuna umuhimu sasa wa kua na filter maada za msingi , uhalisia na Makadirio kuwekwa wazi
uko mbali ungekua karibu ningekuchalaza bakora 6M = 20M kwa miezi 6M
Mahindi Gunia Moja Leo ni Tshs 35000 , ukinunua Mahindi Gunia 200 za Mahindi unaweza kabisa kuuza mwezi Desimba Kwa Tsh Laki Moja na Zaidi Kwa Gunia Moja, Sababu kwanini Mahindi yatapanda Bei ni maljirani zetu wengi Wana njaa na ukame mwaka huu Zambia. , Malawi, Angola, Zimbabwe na Msumbiji Kwa Upande wa mikoa ya kusini magharibi na nyanda za juu kusini. Mahindi Yao yatavuka sana kwenda upande wa Zambia na Malawi Kwa Kasi.
Ruvuma Mahindi Yao yatavushwa sana kuingia Msumbiji na Malawi
Mahindi ya Kiteto, kondoa, Babati, mbulu na Karatu yayakwenda sana upande wa Kenya kupitia namanga ma Tarakea.
Piya mwaka huu wengi wa Mvua umeathiri sana kiimo Cha mahindi kwenye Mashamba ya kichanga na udongo mwepesi Mahindi ya metitia chini, kwenye maeneo ya mbuga na udongo wa mfinyazi ndio watavuna vizuri.