Wekeza Milioni 7 upate Milioni 20 ndani ya miezi 6

Wekeza Milioni 7 upate Milioni 20 ndani ya miezi 6

Unajisikia unachozungumza ivj huamini kam kwa sasa sokoni gunia ni 30k au huamini kama gunia la mpunga linaweza kufika 100k au unaona faida ya mil 20 kubwa sana kwako?

Ngoja nisave hii post tukutane mwakani January panapo majaliwa
 
Wanaouliza ni wapi gunia 30,000 nawasaidia tu Tabora yote, Shinyanga yote, Mwanza maeneo baadhi kwa vijijini bei ni hiyo kwa msimu huu wa mavuno, debe ni 3000-5000 huko vijijini, sio mpunga tu hata karanga na mahindi bei ni hiyo
 
Umemaliza mkuu 3k to 5k maana ake ata 18k gunia unapata
 
Mazao ya kusafirisha yapo mengi, usikomae na mazao ya chakula ambayo bei zake hazikai juu muda mwingi.

Iliki,karafuu,mdalasini,pilipili zilizokaushwa unaweza ukasafirisha nje ya nchi na ukapata pesa kubwa zaidi
Ni pilipili gani hasa mkuu?
 
hawa watoto wa 2000 yaan wanachukulia maisha ni note book kuna umuhimu sasa wa kua na filter maada za msingi , uhalisia na Makadirio kuwekwa wazi

uko mbali ungekua karibu ningekuchalaza bakora 6M = 20M kwa miezi 6M
😂😂😂
 
Wanaouliza ni wapi gunia 30,000 nawasaidia tu Tabora yote, Shinyanga yote, Mwanza maeneo baadhi kwa vijijini bei ni hiyo kwa msimu huu wa mavuno, debe ni 3000-5000 huko vijijini, sio mpunga tu hata karanga na mahindi bei ni hiyo
Huu ni uogo kaka makini unaibiwa.
 
Mazao ya kusafirisha yapo mengi, usikomae na mazao ya chakula ambayo bei zake hazikai juu muda mwingi.

Iliki,karafuu,mdalasini,pilipili zilizokaushwa unaweza ukasafirisha nje ya nchi na ukapata pesa kubwa zaidi
Hizo uwe na mtaji kiasi gani unachukulia wapi
 
Watz kwa kupenda kutoa ushauri ambao wao hawauishi? Kama ni kweli uza/weka dhamana kibanda chako upate mtaji si utapata hela kubwa ya faida ununue au ujenge kubwa zaidi? Za kuambiwa changanya na za kwako!
Mkuu Mpunga na vitunguu ni mazao ambayo timing ya kuuza ni ya msimu yaani seasonal. Mfano kuanzia mwezi wa 10 hadi mwezi wa 5 wa mwaka unaofuata mpunga na vitunguu huadimika sana. Hivyo, ukitunza mazao hayo na kuuza katika msimu ambao ni adimu unapiga fedha ndefu. Mathalan mwaka juzi mchele uliuzwa hadi sh 5,000 kwa kilo moja kwa kipindi hicho na mwaka huu gunia la vitunguu maji limeuzwa zaidi ya sh 400,000 kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa 10 hadi mwezi wa 4.
 
Umemaliza mkuu 3k to 5k maana ake ata 18k gunia unapata
Ila ndo huko Bush kweli gharama ya kulitoa huko ukafike town unakuta debe lishafika 6000-7000,
5000-6000 hii bei uhakika na vijiji husika haviko mbali na barabara
 
Mpunga wa gunia la sh 30000 sijui itakuwa ni wapi! Kahama ambayo ni moja ya sehemu inaayozalisha Michele kwa wingi, Kwa sasa inalishwa Michele wa kutokea Dar.
Labda kama tunaongelea mpunga ya Tunduru ambayo ni tasteless na aifanyi vizuri sokoni.
 
Mazao ya kusafirisha yapo mengi, usikomae na mazao ya chakula ambayo bei zake hazikai juu muda mwingi.

Iliki,karafuu,mdalasini,pilipili zilizokaushwa unaweza ukasafirisha nje ya nchi na ukapata pesa kubwa zaidi
Changamoto watu wengi hatujui namna ya kusafirisha plus gharama zake pia... Iliki ,karafuu bei ya chini hupatikana wapi kwa hapa tz kwetu na nchi gan hununua mazao haya kwa wingi ?
 
Iliki inapatikana turian/matombo/amani tanga

Karafuu inapatikana amani/matombo/zanzibar

Masoko ni wahindi, waarabu na wachina

Usafirishaji ni the same na mazao mengine
Changamoto watu wengi hatujui namna ya kusafirisha plus gharama zake pia... Iliki ,karafuu bei ya chini hupatikana wapi kwa hapa tz kwetu na nchi gan hununua mazao haya kwa wingi ?
 
Salamaleko,

Shalom. Kama tunavojua kipindi hiki kwa maeneo ya vijijini ni kipindi cha kuvuna mazao na kuna niliko mimi kwa sasa debe la mahindi lina 7000 na debe la mpunga lina 5000. Maana yake gunia la debe sita la mpunga ni 30000. Na gunia la mahindi la debe sita linasoma 42,000.

Kama una mtaji wa kununua mpunga kwa kipindi cha mavuno basi una uhakika wa kuingiza mil 20 kwa mtaji wa mil 6 kwa muda wa miezi 5 (UHAKIKA)

MCHANGANUO
Gunia la mpunga 30,000 unanunua gunia 200 jumla inakuja 6,000,000 kwenye million 7 inakua imebaki million 1 kwa ajili ya kukava gharama za ukusanyaji na mambo mengine madogo madogo.

Huu tupo mwezi wa 5 ikifika mwezi wa 10/11/12 gunia la mpunga linafika 100,000l= kutoka 30k ya sasa.

Sasa una gunia 200 stoo zidisha 100,000 kwa kila gunia mzigo utasoma 20,000,000/= ukitoa mil 7 uliyowekeza UNABAKI NA 13,000,000/=KAMA FAIDA KWA MIEZI SITA (6) WOOW

NB: Ni bora kununua mpunga kuliko mahindi sababu mpunga hauna gharama sana kwenye kutunza kama mahindi

UKITAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI UKU NILIKO KUNA FURSA NJOO TUWEKEZE

Ushauri maoni kurekebishana ruksa, nawakaribisha.
Utapeli huanza poooole pole
 
Iliki inapatikana turian/matombo/amani tanga

Karafuu inapatikana amani/matombo/zanzibar

Masoko ni wahindi, waarabu na wachina

Usafirishaji ni the same na mazao mengine
Oooky amani napapata vzur ngoja nkafanye utafit wa bei ya huko na bei ya soko . Thanks
 
Nimenunua gunia 20 za debe sita kwa 6000@ natest zali ikinipendeza nitaendelea nayo mwakani
Matumizi yake
1 .gunia tupu 20=12000
2.usafiri 2000= 40000
3.mpunga gunia 20*36000= 720000
4. Gharama ndogo ndogo = 50000

JUMLA 822000
TUKUTANE JANUARY
 
Mimi nauliza wapi wanafanya kilimo cha umwagiliaji hususani mpunga?
Nataka kufahamu sehemu yenye mto wa uhakika ambapo watu wanalitumia kumwagilia mpunga,
 
Back
Top Bottom