Wema aachiwa, akamatwa tena, azua kizaa zaa mahakamani

Hapa ndio nashindwa kuielewa tasnia ya sheria, kwani huyo hakimu hana smatfoni? Single web pendwa atakuta ushahidi upo kweupe
 
Mkuu anashitakiwa kwa kosa la kusambaza siyo kupiga picha. Ushahidi wa kusambaza ndiyo unaotakiwa
 
Sasa zilifikaje kwenye jamii bila kusambazwa? Yeye ndio anaonekana kwenye hayo maudhui sasa atuambie kama si yeye ni nani aliyesambaza?
 
I didn't expect wakili Msomi Albert Msando kutumia hicho kifungu 225(5) wakati anajua madhara yake ni yapi.

Anyhow, let us wait & see.

Je kifungu hicho kinawezesha mtu kukamatwa tena, kama ilivyotokea au?
 
Mzazi yule mama? [emoji87][emoji87][emoji87][emoji144][emoji144]
HIVI KATIKA NDOA YA HUYU MAMA NA BALOZI SEPETU SI WALIKUWA WANANDOA KABLA YA KUACHANA?? NA WASIWASI PIA KUWA HUYU DADA ALIKOSA MALEZI YA BABA TANGU AWALI AU KWA WINGI WA KIASI CHAKE!!
 
Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amezua kizaa zaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akigoma kukamatwa na polisi baada ya mahakama hiyo kumwachia huru na kisha kumkamata tena na kumuweka mahabusu ya mahakama hiyo.

Wakati askari wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati askari na mawakili wake, Albert Msando na Reuben Simwanza.

Hata hivyo, askari hao walifanikiwa kumkamata msanii huyo aliyetoka Mahabusu ya Gereza la Segerea Juni 24, mwaka huu ambapo alifika mahakamani asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayoendelea mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai hana shahidi baada ya shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi kudai ni mgonjwa.

Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Wema, Albert Msando kwa madai kwamba haina mashiko, mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho hivyo hawawezi kuahirisha tena.

“Mheshimiwa shauri lipo zaidi ya siku 60, upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru,” alidai.

Wakili Mwenda alipinga akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Hakimu Kasonde alisema anakubaliana na maombi ya upande wa utetezi, sheria hiyo inatumika wakati wowote hivyo mahakama inamuachia huru mshtakiwa.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.
Kama wamemkamata labda wanatamani wakamuambarudi usiku waleo
 
HIVI KATIKA NDOA YA HUYU MAMA NA BALOZI SEPETU SI WALIKUWA WANANDOA KABLA YA KUACHANA?? NA WASIWASI PIA KUWA HUYU DADA ALIKOSA MALEZI YA BABA TANGU AWALI AU KWA WINGI WA KIASI CHAKE!!
Hapana nasikia huyu mama alikuwa msaidizi wa ndani
 
I didn't expect wakili Msomi Albert Msando kutumia hicho kifungu 225(5) wakati anajua madhara yake ni yapi.

Anyhow, let us wait & see.
Msando Kachemka Sana Leo Hata Mm Nimeshangaa Sana, Halafu Wema Ana Bahati Leo Msando Kaja, Yule Dogo Wakili Wake analamba Midomo Mda Wote
 
Yule dogo mlaini sana. Nahisi alikosewa kuumbwa mwanaume hahahahah.
 
Sasa zilifikaje kwenye jamii bila kusambazwa? Yeye ndio anaonekana kwenye hayo maudhui sasa atuambie kama si yeye ni nani aliyesambaza?
Hapo ndipo kwenye kasi yenyewe. Waendashamashitaka wanatakiwa kudhibitisha kuwa ni Wema ndiyo kasambaza na watetezi kuja na hoja kuwa hakuna ushahidi wa yeye kusambaza.
 
Wengine wakifutiwa kesi wanatoka wanakimbia breki ya kwanza nyumbani.
Yeye amefutiwa kesi katoka anapiga selfie.
Halafu kweli[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hivu ukifika nyumbani hukamatwi tena kama kuna lolote?
 
Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amezua kizaa zaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akigoma kukamatwa na polisi baada ya mahakama hiyo kumwachia huru na kisha kumkamata tena na kumuweka mahabusu ya mahakama hiyo.

Wakati askari wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati askari na mawakili wake, Albert Msando na Reuben Simwanza.

Hata hivyo, askari hao walifanikiwa kumkamata msanii huyo aliyetoka Mahabusu ya Gereza la Segerea Juni 24, mwaka huu ambapo alifika mahakamani asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayoendelea mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai hana shahidi baada ya shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi kudai ni mgonjwa.

Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Wema, Albert Msando kwa madai kwamba haina mashiko, mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho hivyo hawawezi kuahirisha tena.

“Mheshimiwa shauri lipo zaidi ya siku 60, upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru,” alidai.

Wakili Mwenda alipinga akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Hakimu Kasonde alisema anakubaliana na maombi ya upande wa utetezi, sheria hiyo inatumika wakati wowote hivyo mahakama inamuachia huru mshtakiwa.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.
HUYU DADA ANA SHIDA KIMAADILI SANA. NI JUU YAKE KUTUBU KWA MOLA WAKE, NA KISHA KUOMBA WATANZANIA WOTE MSAMAHA KWA DHATI KUTOKA MOYONI. KISHA ASIKUTWE TENA NA KASHFA MFANO WA HIZO.

WAZAZI WASIOZINGATIA MAADILI KWA WATOTO, NAWAKUMBUSHA KUCHUKUA SOMO KWA MAMA WA BINTI HUYU. MAANA SIDHANII KAMA ANAPENDA KUONEKANA KTK VYOMBO VYA HABARI AKIMSINDIKIZA BINTI YAKE KTK MASHTAKA AMBAYO KIMSINGI NI YENYE KUFEDHEHESHA.
 
Kuzuia polisi kukukamata ni sawa na kuzuia polisi kufanya kazi yake,ni kosa la jinai
Huyo wakili msomi nae alikunbwa na mihemko tu,alichofanya ni obstruction of justice,tena akiwa bado kwenye viunga vya mahakama,anaweza hata kupokwa leseni yake
 
Rahisi Sana kutamka mnayotamka ila omba Mungu akupe watoto wasikivu kinyume chake ni maumivu Sana kwa mzazi. Wema badilika jamani kila siku wewe tu mamaa muonee huruma mamaako mabezo yote haya ni radhi tosha sio mpaka akutamkie
 
Back
Top Bottom