Wema amenishangaza kwa kauli ya "yeye na uzungu wake"

Kule Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2016
Posts
3,157
Reaction score
1,894
Habarini Wadau,

Usiku huu katika taarifa ya habari ya TV1, habari ikielezea uhamasishaji wa wasanii kuupa kipaumbele miziki yenye mahadhi ya uswahili kama segere na singeli nimemsikia Wema Sepetu akihojiwa na kuzungumza haya:-

"Mimi pamoja na uzungu wangu lakini huwa napenda nyimbo zenye uswahili kama hizi"

Kwa aliyeelewa vizuri hiyo kauli ya Wema ilimaanisha nini? Wema ni Mzungu?

Nawasilisha.
 
Kungekua na sindano unajidunga phenotype inabadilika na kua mzungu moja kwa moja basi nahisi huyu mdada angekua wa kwanza, akifuatiwa na wadada weusi wengi tu, watu wanafananisha uzungu na pesa.
Elimu ndogo, social media inazidi kuvuruga maana watu kama Wema ndio wanaongoza followers. Tusipoli~solve hili tatizo generation inayofuata itakua inatisha.
 
Lakini mkuu watu weusi wenye kupenda weusi wao ni wachache.
 
Lakini mkuu watu weusi wenye kupenda weusi wao ni wachache.

Ni wachache sana, na kilichopelekea hapo ni pressure, hollywood movies zilianza zamani tu kuonyesha mwanamke mweupe kua ni mzuri kuliko mweusi, society ikaiga, sehemu zote wakaanza kufanya hivyo, siku hizi hata wasanii wa bongo wakifanikiwa tu wanakimbilia kuweka weupe tu kwenye video zao, nyimbo za matatizo ndio watarudi kuchukua wadada weusi. Msichana gani atapenda weusi kwa pressure yote hii?
Binadamu vila.za kazi sana kudeal nao, hili hata hawalioni.
 
Dah, kwakweli watu tumeumbwa tofauti, siitaji kutukanwa tusi kubwa kama huyu dem anavyotukana, angepata fahamu akiwa Muhimbili chumba cha uangalizi maalumu siku ya 3 nahata aulizwe kilitokea nini hatokuwa na kumbukumbu.
 
Ahahahahaaaa yeah right!

Huu ndo 'Uzungu' wake.

Hebu yasikieni hayo matusi ya 'Mzungu'.

'Mzungu' in action...

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Njaa, Ujinga Ushamba na Uigaji unampoza sana Wema pamoja na mabinti wengi kweli wa kibongo.
 
Dah, kwakweli watu tumeumbwa tofauti, siitaji kutukanwa tusi kubwa kama huyu dem anavyotukana, angepata fahamu akiwa Muhimbili chumba cha uangalizi maalumu siku ya 3 nahata aulizwe kilitokea nini hatokuwa na kumbukumbu.
Hao wanaotukanwa pia wanaumia sana ila wanashindwa kureact sana eti kulinda umaarufu wao hapa bongo.
 
Hao wanaotukanwa pia wanaumia sana ila wanashindwa kureact sana eti kulinda umaarufu wao hapa bongo.
Mwanamke akishakutukana matusi mazitomazito kama hayo na ukamuacha salama huna haja ya kuwa maarufu, umaarufu sio kuonyesha kuhimili matusi ya kike ila kuonyesha kuwa mwanaume ni kichwa.
 
Dah, kwakweli watu tumeumbwa tofauti, siitaji kutukanwa tusi kubwa kama huyu dem anavyotukana, angepata fahamu akiwa Muhimbili chumba cha uangalizi maalumu siku ya 3 nahata aulizwe kilitokea nini hatokuwa na kumbukumbu.
Mwanamke apigwi bali anapigwa mkwara w kupigwa na anatulia.
 
Kwanza sikutaka kuamini masikio yangu juu ya kile nilichokisikia. nikamuuliza mwenzangu,
"Eti Wema amesemaje?"
"Amesema yeye pamoja na uzungu wake wote bado anapenda mambo ya uswahili kama yale...."
Nikasema hapana kwa kuwa hii tv ni ya zamani itakuwa imeanza kutupa habari zisizo za kweli.
Sasa saa hizi nimeingia humu nimeikuta tena hii habari, kwanza nikatikisa kichwa kwa dharau halafu ghafla nikakumbuka huyu amewahi kutaka kugombea ubunge kupitia CCM na alipita kila mkoa kumnadi Mr Alcohol... "Sio ajabu hawa ndio tuliochagua kuwakabidhi nchi yetu eti wamesema wataifanya iwe ya viwanda hahahahahah."
 
Konsciouz

Watu wanaohusisha ustaarabu au tabia fulani fulani na Uzungu ni wazi hawajaishi na Wazungu kwa muda mrefu.

Kwa sababu, kwa mtu yeyote aliyeishi na Wazungu kwa muda mrefu basi lazima atakuwa anajua kuwa hata wao wapo wengi tu wenye tabia za ajabu ajabu kama uhasidi, upekepeke, umbeya, uasherati, na kadhalika.

Hebu ona hawa Wazungu wanavyosutana na kurushiana ngumi halafu nambie wana tofauti gani na watu wengine..

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…