Wema, Aunty "Kimenuka" kisa Zari

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kugombana baada ya Aunt ' kuposti ' kwenye ukurasa wake wa Instagram tangazo lililohusiana na pati ya mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz ', Zarinah Hassan ' Zari The Boss Lady ' iliyofanyika Mlimani City jijini Dar wikiendi iliyopita.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao wa sinema za Kibongo, baada ya Aunt kuposti tangazo hilo akiwalaumu watu wa mtandao wa huduma za simu waliomtumia ndipo Wema akaona na kuja juu. Ilielezwa kwamba baada ya Aunt kutupia picha ya tangazo hilo, Wema alichukizwa na kitendo hicho huku akimuona Aunt kuwa amemsaliti.

Ilisemekana kwamba katika utetezi wake , Aunt hakupendezwa na tangazo hilo alilotumiwa na mtandao huo wa simu .
"Wema alivyoona alichukia na kusema Aunt alikuwa akimsaliti na alitumia tangazo lile kijanja kwa ajili ya kuwatangazia watu kuhusu pati ya Zari wakati anajua kabisa kuwa Wema hazipandi na Zari kwa sababu anatoka na aliyekuwa mchumba ' ke (Diamond ), " kilisema chanzo hicho .

Wema Isaac Sepetu katika sakata hilo, kuna watu ambao waliona Aunt hakuwa na kosa lakini wapo walioona hakuwa sahihi, jambo ambalo lilichochea ugomvi wao huku wakidaiwa kukesha wakitukanana. Gazeti hili lilipozungumza na Aunt kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea akisema kuwa hakuwa na maana mbaya kuposti tangazo hilo lakini kila mtu ana mtazamo wake .

"Mimi sikumaanisha chochote kibaya kuhusu hilo tangazo na wala sikujua kama kuna mtu anaweza akalichukulia tofauti kabisa na hapo na mimi ndiyo nashindwa cha kuzungumza, " alisema Aunt .Alipopigiwa Wema simu yake iliita bila kupokelewa hadi gazeti hili linakwenda mitamboni .
 
Attachments

  • 1430939045306.jpg
    48.5 KB · Views: 4,251
Hivi ni kweli Aunt alipost hilo tangazo la White Party jamani? Mimi sijamfollow sionagi la maana analopost.Kama ndio hivyo basi lazima wema amind maana angeweza kumalizana na mtandao kimya kimya sio lazima kupost insta.
 
Aunty hana kosa nionavyo alipost msg ya vodacom waliyomtumia sema bi dada anapenda kuabudiwa kama Mungu. hawezi dumu na marafiki.
Hivi ni kweli Aunt alipost
hilo tangazo la White Party jamani? Mimi sijamfollow sionagi la maana
analopost.Kama ndio hivyo basi lazima wema amind maana angeweza
kumalizana na mtandao kimya kimya sio lazima kupost insta.
 
Hivi ni kweli Aunt alipost hilo tangazo la White Party jamani? Mimi sijamfollow sionagi la maana analopost.Kama ndio hivyo basi lazima wema amind maana angeweza kumalizana na mtandao kimya kimya sio lazima kupost insta.

Alipost I saw it kwa macho yang bt watajijua wenyewe!!!
 
Tatizo la Wema anapenda urafiki wa Kizaramo mpaka anapitiliza!madira sare,kusuka sare,viatu sare,pafyumu sare utadhani watoto wadogo!

Na ukiwa naye kwenye urafiki basi ukubali kuwa mtumwa maana utafanya anachopenda yeye na adui yake basi lazima na wewe awe adui yako.hata kama hajakukosea,usimpe hata salam maana ukimpa tu anakuona msaliti.

Ngumu sana kuwa na urafiki na mtu kama Wema maana inatakiwa uwe na moyo malaika usimkosee hata kidogo.

Hata hivyo Wema ni mwepesi wa kusamehe naimani watayamaliza tu na Aunty yake
 
Hivi ni kweli Aunt alipost hilo tangazo la White Party jamani? Mimi sijamfollow sionagi la maana analopost.Kama ndio hivyo basi lazima wema amind maana angeweza kumalizana na mtandao kimya kimya sio lazima kupost insta.

NIliona best, nilishangaa ata mimi, alimtag diamond, ney na shamsa ford, diamond akamuuliza aunty shamsa na ney wamefanyaje? SAsa aunty sijui alikuwa ana maana gan kuwatag hao watu
 
AHahah urafiki wa kizaramo, nimecheka mpaka bas, sijui yupoje mxiuu
 
Aende zake huyo so Aunt asiposti boyfi wake ale wapi...kagombana na kumchukia dada yake Diamond kwa kuposti videos na picha za Zari na kaka yake

Kisa anayefanya nae kazi kamuoa Esma, so atupilie mbali ndugu zake. Akili finyu sana w.
Akaachia makamanda wake wamtukane sana tena sana dada wa watu...hadi ndoa nusu ivunjike na ndio maana petit hakwenda Mwz kubeba pochi.

Eti pia ukaribu wao ulifumaniwa,

Mie msomaji pia
 
Hivi ni kweli Aunt alipost hilo tangazo la White Party jamani? Mimi sijamfollow sionagi la maana analopost.Kama ndio hivyo basi lazima wema amind maana angeweza kumalizana na mtandao kimya kimya sio lazima kupost insta.

Yes kiujanja, Wema anakasirika nini kwa kweli wakati Mr wa aunt shughuli ilimuhusu ni dancer wa Diamond.
 
Hivi ni kweli Aunt alipost hilo tangazo la White Party jamani? Mimi sijamfollow sionagi la maana analopost.Kama ndio hivyo basi lazima wema amind maana angeweza kumalizana na mtandao kimya kimya sio lazima kupost insta.

Aliposti hii
 
Attachments

  • 1430946467207.jpg
    34.6 KB · Views: 1,496
Akaandika hivi nifah
 
Attachments

  • 1430946770057.jpg
    27.6 KB · Views: 1,464
Last edited by a moderator:
Mama ubaya plzz have several sits!!!!! Si umeolewa wewe unapata wapi muda kumpigia mmeo pasi kama kutwa kukimbizana na nani kaposti nini.. ???Wanchoshaa!!
 
Anti anaishi mjini kwa pesa ya Diamond, sidhani kama kakosea.
 
Kweli Uyu si Mwanamke wa Kuoa. Yani anaacha kufanya ya maana anakomalia upuuzi upuuzi tu

Mtazamo wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…