Wema, Aunty wakwepana Ikulu

Wema, Aunty wakwepana Ikulu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MAHASIMU wawili katika anga la mastaa , Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wiki iliyopita walikwepana na kushindwa kusalimiana, licha ya wote kuwa waalikwa katika hafla maalum ya kujipongeza iliyofanyika Ikulu , jijini Dar es Salaam.

Aunt Ezekiel .

Gazeti hili ambalo pia lilikuwepo kwenye viwanja hivyo vilivyosheheni mastaa wa fani mbalimbali , liliwaona wawili hao ambao awali walikuwa marafiki wakubwa , wakijivinjari kwa tahadhari ili wasikutane , licha ya nyakati tofauti kuzungumza na mastaa wengine .

Wema ambaye katika kampeni za CCM alikuwa pamoja na Makamu wa Rais , aliyekuwa mgombea mwenza Samia Hassan Suluhu , wakiwa na kundi lao maarufu la Mama Ongea na Mwanao , muda mwingi alionekana akiwa na wenzake aliokuwa nao ? Timu moja ? Kwenye kampeni .

Aunt Ezekiel ambaye wakati wa kampeni hizo alikuwa kundi lililopewa jina la Nimestuka , naye alijichanganya na waalikwa wengine lakini jicho lake likiwa makini kuhakikisha hakutani hata sehemu moja na muigizaji huyo wa Filamu ya Madam .

Katika sherehe hiyo pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa kitaifa wa serikali iliyopita , akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mkewe, mama Salma Kikwete na waziri mkuu wa zamani wa Kenya , Raila Odinga na mkewe .

Mastaa wengine waliojumuika katika hafla hiyo iliyochagizwa na muziki kutoka kwa Yamoto Band ni pamoja na mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi , Ally Choki , muigizaji mkongwe , Bi Mwenda , mlezi wa wasanii Mama Loraa na Mbasha.
 
Inabidi muheshimiwa Magufuli aingilie kati.
 
Huyu Wema na Aunty hawana mchango wowote katika nchi hii.. Wameshatumika na ccm na sasa ni makapi.. Warudi wapambane na maisha kupitia papuchi zao...!!
 
hahahaha afanye ziara ya kushtukiza bongo movie
 
Mbona kila mara wananuniana? Mi siwaelewi . Wamekaa kiswahili Swahili, wenyewe kutwa majungu tu. Hadi wamesahau fan Yao ya usanii.
 
Hawa walikuwa wapenzi (Ku. Sa. Ga. .....) sasa kila mmoja anakumbuka mautamu ya mwenzie! Huku akiwa hataki kujiweka wazi!
Mbaffffffff kabisaaaaaaa
 
Ikulu ya Tanzania imepoteza kabisa heshima yake.
 
Back
Top Bottom