Igweeeeeeee,
Hongera Wema Sepetu kwa kupata muamko wa kugombea ubunge na ni wazo zuri ila kwa maoni yangu kwako ni kwamba usigombee mwaka huu ubunge wa viti maalum hadi 2020 ndio ugombee. Hii ni kwa sababu zifuatazo.
Kwanza mjue kuwa wabunge wa viti maalum hawateuliwi na Rais kama wengi wanavyodhani bali wagombea hufanya kampeni na wanachama tu wa chama husika wenye kadi za vyama ndio hupiga kura na hushiriksha wanawake tu.
Wema bado huna connection nzuri na wanachama wako unaotaka wakakupigie kura, ujue kuwa wanachama wenye kadi tu ndio wataopiga kura ya kukupitisha ndani ya chama na kwa uzoefu wangu hautapita hata kwenye hatua za uteuzi wa chama kwasababu unaokwenda kushindana nao ni watu mashuhuri katka vyama na serikali pia.
Ni wanawake ambao wametumikia vyama vyao katika nafasi mbalimbali,makada,wenyeviti wa vyama nk. Ambapo kwa upande wako hujawahi hata kuwa mwenyekiti wa mtaa wako kupitia chama chochote kile, kitu ambacho kinakupnguzia credit kwani kwa bahati mbaya wanaopiga kura sio wananchi wote bali wanawake wa vyama husika wenye kadi.
Lakini pia vyama hufanya uteuzi wa mtu wa kuwawakilisha jambo ambalo litakuwa sumu kwako kwani kuna watu huandaliwa mapema na vyama husika na wanaaminika zaidi na ni mashuhuri pia.
Anza harakati za kisiasa sasa ili uje ugombee 2020 nawe utapitishwa na chama.
Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu and i can say sorry for you because hutapitishwa na chama kama mgombea.
Chukua ushauri wangu uepuke kupoteza fedha bure na muda. Nakupenda that's why nimekujuza.
La mwsho ni kwamba wananchi bdo hawajawahi kukuona hata katika harakati zozote za kisiasa, umeibuka ghafla sana wakati hata hatujui Wema atatushawishije katika suala la ajira na uchumi wakati hata yeye hatujui kawekeza kwenye nini.