Wema Sepetu, Mr. Blue, TID, Recho wahusishwa na Dawa za Kulevya. Watakiwa kuripoti kituo cha Polisi

Wema Sepetu, Mr. Blue, TID, Recho wahusishwa na Dawa za Kulevya. Watakiwa kuripoti kituo cha Polisi

NApata mashaka kama vita ya mtandao wa madawa ya kulevya inapaganwa kwa style hii.Kunapaswa kuwe na uchunguzi wa muda mrefu na wa kina juu ya mitandao hii hata kama itachukua miaka lakini mwisho wa siku uje na ushahidi wa uhakika.Ikienda inavyokwenda sasa itakuwa kama hili suala la mnyama mkubwa wa juzijuzi.
 
CCM hawana fadhira leo hii wamemuubua wema sepetu na alivyojifanya lumpe lumpe ss kasalitiwa mchana kweupe ,ss kaubuliwa ndo utajua CCM siyo watu wa spot spot
 
Mwenge..kituo cha itv kuna bar inaitwa Maryland. Sasa nyuma ya Maryland bar..mtaa wa kwanza kushoto..hapo ndiyo kitivo cha mateja dar es salaam.

Kuna jamaa mmoja white hivi anavaa Sana pensi..huyo ndiyo pusha wao hapo tangu Mimi nasoma Mwenge primary .
Pale nilikuwa nikipita naogopa sana maana wale mateja wanatisha vibaya sana. Tumuombee Mhe. Makonda akifanikiwa itakuwa habari njema kwa jamii
 
Kuna wale wapakistan walikamatwa na kilo za kutosha tu as ushahidi, na wakaachiwa hadi leo hakuna aliyewajibishwa.Ukimkamata TID ukawaachia wapakistani walioingiza hapo hupambani na unga.Na hadi leo hakuna mtu aliyetiwa hatiani kwa uzembe ule wa wale wapakistani KUTOROSHWA,hawakupaa angani wale wamepita kwenye entry ya kawaida tu
Kuna watu waliwachezea faulo ili watoke

Ova
 
CCM hawana fadhira leo hii wamemuubua wema sepetu na alivyojifanya lumpe lumpe ss kasalitiwa mchana kweupe ,ss kaubuliwa ndo utajua CCM siyo watu wa spot spot
Ngoja watoto wako wale unga ndo utamtetea wema vizuri Zaidi;
 
Alhamis hii kwenye mitandao ya kijamii
kulikuwepo na habari za kushtua kuhusiana
na orodha iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda ya watu
wanaotuhumiwa kuuza unga, kutumia na
polisi wanaojihusha na wafanyabiashara wa
unga.
Kwenye orodha ya watu wanaoshukiwa
kuwemo kwenye biashara hiyo, yumo
Ahmed Hashim Ngahemela maarufu kama
Petit Man ambaye tayari yupo mikononi
mwa polisi. Petit ni bosi wake na rapper Bill
Nas ambaye amedai kuhuzunishwa na
taarifa hizo.
“Ukizungumzia suala la Petit, hili suala
linaniumiza sana na siwezi kuzungumzia
kitu chochote kwa sasa,” ameiambia Dizzim
Online.
 
dah huyu makonda bana
hivi VITA YA MASHOGA ZAKE SI ILIMSHINDA ITAKUA YA KINA ELCHAPO?MAPOUDA BEIBE?
THATS A JOKE MWAMBIENI MAIGIZO AWAACHIE WAKINA WEMA SEPETUNGA
 
Naam hii ni asubuhi, kama mambo yakiendelea kuna watu walikuwa wakiabudiwa kwamba wana mafanikio makubwa sana asije shangaa nao wamo na wanahusika na hii haramu
 
Kifupi ni kwamba mameneja wengi wa wasanii ndio ma drug dealer wa kati. Wanawachukua wasanii wanakuwa karibu nao wanawageuza punda. Sasa baadhi ya wasanii wanawauzia watu wenye hela zao na wataona it's okay hata Wao kujiingiza. Wanajaribu wanakuwa Sasa wameguka na kuwa Ray C na kina chid benzi. Ndo maana bongo movies na na bongo FLEVA kazi zao zinahamasisha vijana kujidunga. Anajifanya kuhuzunishwa Ila ukweli wengi wanajua wasanii ndio wapitishaji wa madawa. Utaskia show nje ya Nchi kumbe wanarudi na sembe.. Kiama Chao kimeanza kunukia. NIDHAMU inarudi mdogo mdogo. Watanzania tuache uwoga tupige kelele Njooni tujitoe ufahamu tuwataje ma dealer.. Watu wanaogopa kupotezwa. Wasanii hii awamu nyingine. Acheni kuishi Kwa Hisia fikirieni.
 
Skendo kumbe huwa ni kweli. Unganisha maisha ya wasanii kazi zao na tatizo LA madawa alafu angalia mitaa wanayokaa Sana hasa kinondoni magomeni Mbezi utagundua wasanii ndio madawa tunayoyazungumzia. Wafanyiwe uchunguzi wote ni kwa Nia njema
 
Wilaya ya kinondoni mbona sio kubwa yakifukuliwa Mapapa hata matano tu biashara itapungua Sana. Kuna WATU wanaamini huu MTANDAO ni hatari Sana wanafananisha na marekani.. Hapana Kwa tanzania ni RAHIS Sana kuudhibiti. USHIRIKIANO ukitolewa. Makonda Jana kasomeka
 
Back
Top Bottom