Alikamatwa mtu mmoja anaitwa Shkuba, huyu alikuwa bwana unga ambaye hata FBI walimfahamu. Na alipokamatwa alikabidhiwa haraka kwa FBI. Ilikuwa vita kati ya Polisi dhidi ya Polisi. Ni tukio la mwaka mmoja tu uliopita.
Unaweza kusema hiyo ilikuwa hatua kubwa kwa kikosi kazi kilichoongozwa na kamanda mstaafu Nzowa. Lakini kazi ilikuwa bado sana.
Wapo watu wamezuiliwa kungia katika ardhi ya Marekani kwa kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya. Majina yao hayakutajwa na mtu yeyote na hakuna kiumbe chochote kinachoweza kuthubutu kuwataja ndani ya ardhi ya Tz. Kikwete hakuwataja, Magufuli hatawataja. Hakuna wa kuwataja.
Vita hii inahitaji akili nyingi kuliko tulizonazo sio lopolopo za kisiasa.
Wema, Chid benz ambaye sasa hv amekuwa Chid paso, Babuu wa kitaa nk! hawa ni Mules tu! Hawa ni wanapunda tu wanaotumiwa na watu. Ukute wanaowatumia hawa, na wenyewe wanatumiwa vilevile. Na unaweza kutumiwa na mtu usiyemjua vilevile. Huhitaji sana kuwahoji hawa kwa sababu ni 'Mules' wanaotumiwa na 'Mules'. Wapo watu huko magerezani na vichochoroni wana taarifa za biashara ya dawa za kulevya kuliko vyombo vya intelijensia. Ukiwapata hawa utapata taarifa ambazo bila shaka, utakaa nazo mwenyewe. Hutathubutu kunyanyua kinywa chako. Vita dhidi ya dawa ya kulevya inapiganwa kimya kimya, ukinyanyua kinywa chako basi iwe ni kuelimisha jamii kuhusu madhara na mabaya ya biashara hii, lakini 'The batle' should be silence. Ukikurupuka hautafanikiwa kwa sababu wana nguvu ya pesa na madaraka, wana akili, ni wajanja na wajuvi wa mambo kuliko wengi wetu. Wameshikilia sehemu kubwa ya uchumi wetu. Na mtandao wao ni wa kidunia, unahitaji jeshi kupambana na hawa watu, na unaweza kukuta ndani ya jeshi wamo vilevile.