Wema uliwahi kukuponza?

Wema uliwahi kukuponza?

mangiTz

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,820
Reaction score
3,062
Habari wana jF, kama heading inavyojieleza share experience je wema uliwahi kukuponza katika harakati za maisha ukamsaidia mtu lakini ile huruma yako ikakupa matokeo hasi

Ndio, katika maisha ya kawaida haya mambo yapo sana mtaani, maofisini n.k

Haya hutokea kwa kuwa wanaosaidiwa huacha kuthamini mchango wa waliowasaidia badala yake ikitokea tofauti na matarajio yake lawama zinakuangukia wewe akidai kubwa ndiye uliyempoteza au kumuingiza mkenge.

Mimi iliwahi kutokea kwa uchache matukio kadhaa kuna jamaa alikosea kufanya malipo sasa nikamsaidia kuwasiliana na kampuni hiyo nilikuwa na namba yao ya WhatsApp , swali nilimpa namba akasema wewe nisaidie mimi sina bando alafu sijui naanzia wapi, alilipa kupitia tigopesa alipiga simu tigo wakamwambia hela ilishaingia kwenye account ya hiyo kampuni hivyo hatuna mamlaka nayo kuweza kuirudisha wasiliana na hiyo kampuni .

Hivyo nikaanza kuwasiliana nao nikachukua na namba ya jamaa na sms ya malipo wakasema tunaofanya kazi unarudisha ndani ya siku7 za kazi. Kwa bahati mbaya zilipita siku saba hazikurudi jamaa akanipiga kwahiyo vipi sasa hela yangu haijarudi , the way alivyouliza nikaona mmh

Isiwe tabu nikamwambia nakupa namba akasema wewe ulishaanza nao ulizia nikasema sawa . Mara ya pili nilipouliza wakasema mpaka siku 14 . Bahati mbaya zilifika haikurudi kwake ila hiyo kampuni wakadai wameshaitoa nilichofanya nikampa namba jamaa awasiliane nao akaambiwa aprint ministatement apeleke jamaa si akaprint akaja kwangu akaanza kung'ang'ania wewe ndio uliwasiliana nao na wewe unajuana nao nilichoka nilimweleza aende makao makuu ya hiyo kampuni nikamwelekeza ila aliondoka anatukana.

Kisa kingine niliwahi panda daladala kondakta alisahau kunicharge nauli nafika mwisho wa kituo ambako ndio gari inaishia nikakumbuka sijalipa nikatoa nauli nalipa tu nipo chini gari ikawekwa gear imegeuza konda chenji jamaa akanipiga mkono kuashiria njoo chukua bana dereva kakanyaga mafuta konda akafunga mlango aisee ilinibidi nicheke😅 nikaona wema gani wa kijinga hivi.

Share hapa nawe wadau tujifunze karibuni
 
Wema uliniponzaa Kuna mdada nilimsaidiaa sana mwisho wacku aliniitia mwizi
emoji120.png
..imenifanyaga niogopege kutoa msaada Kwa wanawakee hataa dada zangu..

Maana hata dadaangu nae nilimpaga mtaji ule mtaji ukawa chanzo Cha ndoa yake kuvunjika maana alifanikiwa kupitiaa ule akaanza dharau Kwa mumewe ndoaa ikafaaa
emoji24.png
 
Wema uliniponzaa Kuna mdada nilimsaidiaa sana mwisho wacku aliniitia mwizi [emoji120]..imenifanyaga niogopege kutoa msaada Kwa wanawakee hataa dada zangu..

Maana hata dadaangu nae nilimpaga mtaji ule mtaji ukawa chanzo Cha ndoa yake kuvunjika maana alifanikiwa kupitiaa ule akaanza dharau Kwa mumewe ndoaa ikafaaa [emoji24]
 
]Wema uliniponzaa Kuna mdada nilimsaidiaa sana mwisho wacku aliniitia mwizi [emoji120]..imenifanyaga niogopege kutoa msaada Kwa wanawakee hataa dada zangu..

Maana hata dadaangu nae nilimpaga mtaji ule mtaji ukawa chanzo Cha ndoa yake kuvunjika maana alifanikiwa kupitiaa ule akaanza dharau Kwa mumewe ndoaa ikafaaa [emoji24]
Pole mkuu
 
Kuna demu nilimsaiidiaga alikuwa jiran yangu kipindi iyo alikuwa nashida sana nilimpag kiasi flan iv cha cash lkn yeye akapeleka tarifa kwa wenzake kwamba nimemuonga namtaka aisee nilichoka ilikuw aibu sana na taarifa zilisambaa mbaka kujieeleza nikawa nashindwa
 
Wale wa mama wa vikoba wanakwambia niazime laki5 naonyesha na kukuletea aisee [emoji119][emoji119]
Nimecheka hadi michozi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna demu nilimsaiidiaga alikuwa jiran yangu kipindi iyo alikuwa nashida sana nilimpag kiasi flan iv cha cash lkn yeye akapeleka tarifa kwa wenzake kwamba nimemuonga namtaka aisee nilichoka ilikuw aibu sana na taarifa zilisambaa mbaka kujieeleza nikawa nashindwa
Pole mkuu😂kuna muda linakukaa vibaya hadi unaona hata nikieleza ukweli watu hawataelewa watahisi unajitetea
 
je wema uliwahi kukuponza katika harakati za maisha ukamsaidia mtu lakini ile huruma yako ikakupa matokeo hasi
Kuna dogo nilimpa msaada mkubwa wakati wa kutafuta chuo na kupata boom kila kitu nikamshughulikia kulipia gharama za stationary kumtafuta mwanasheria kusaini kugonga muhuri mpaka kuzipeleka documents zake Posta nilifanya Mimi, kila kitu kikaenda sawa akapata na boom % nzuri tu nikamweleza hizo Pesa za boom zitumie kwa umakini ukiweza weka akiba ukimaliza Chuo zikusaidie ukiwa unajitafuta dogo akasema sawa,

Aisee cha kushangaza alipopata boom la kwanza tu akaanza tabia za ajabu yaan ni wanawake wanawake na yeye ni anabadirisha Malaya tu kwa Pesa za boom leo kamwingiza huyu kesho kamwingiza yule, mpaka anamaliza mwaka wa 3 tabia yake ni hio boom lake ni linaishia kwenye kununulia Malaya tu

Nilijuta kutoa msaada kwa-kweli unaweza ukamsaidia mtu baadae ukaja kujuta tu kwanini ulimsaidia Bora ungemuacha tu apambane na hali yake
 
#1. Nilimsaidia rafiki yangu kumuonesha mfereji wa Suez tukiwa darasa la 7 (kwenye ramani ya dunia).
Mwalimu alivyorudi ili apatiee jina la mtu wa kwanza kuuona jamaa alinikazia na alipewa zawadi ya daftari yeye kwenye group zima na kumwagiwa sifa kibao.

#2. Wakati nipo secondary, siku moja tumeandaa maji kwenye ndoo masafi ili baadaye tuyatumie.

Kumbe mama mmoja anatoka toilet akapita na kuyanawa yale maji.

Kwa vile sikutaka yawe makubwa, nilimsanua rafiki yangu kwamba ""maji yaliyo kwenye ndoo ile ya wazi usiyatimie ni machafu"".

Alivyo mjinga akamwambia pia yule mama kuwa Lucky Star anasema maji ya kwenye ndoo kubwa ya wazi tusiyatumie ni machafu.

Asee, nilijuta siku hiyo, maana yule mama alikuja na maswali ambayo sikuweza kumjibu kitu. Wema sometimes unamalipo hasi sana.
 
Back
Top Bottom