mangiTz
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,820
- 3,062
Habari wana jF, kama heading inavyojieleza share experience je wema uliwahi kukuponza katika harakati za maisha ukamsaidia mtu lakini ile huruma yako ikakupa matokeo hasi
Ndio, katika maisha ya kawaida haya mambo yapo sana mtaani, maofisini n.k
Haya hutokea kwa kuwa wanaosaidiwa huacha kuthamini mchango wa waliowasaidia badala yake ikitokea tofauti na matarajio yake lawama zinakuangukia wewe akidai kubwa ndiye uliyempoteza au kumuingiza mkenge.
Mimi iliwahi kutokea kwa uchache matukio kadhaa kuna jamaa alikosea kufanya malipo sasa nikamsaidia kuwasiliana na kampuni hiyo nilikuwa na namba yao ya WhatsApp , swali nilimpa namba akasema wewe nisaidie mimi sina bando alafu sijui naanzia wapi, alilipa kupitia tigopesa alipiga simu tigo wakamwambia hela ilishaingia kwenye account ya hiyo kampuni hivyo hatuna mamlaka nayo kuweza kuirudisha wasiliana na hiyo kampuni .
Hivyo nikaanza kuwasiliana nao nikachukua na namba ya jamaa na sms ya malipo wakasema tunaofanya kazi unarudisha ndani ya siku7 za kazi. Kwa bahati mbaya zilipita siku saba hazikurudi jamaa akanipiga kwahiyo vipi sasa hela yangu haijarudi , the way alivyouliza nikaona mmh
Isiwe tabu nikamwambia nakupa namba akasema wewe ulishaanza nao ulizia nikasema sawa . Mara ya pili nilipouliza wakasema mpaka siku 14 . Bahati mbaya zilifika haikurudi kwake ila hiyo kampuni wakadai wameshaitoa nilichofanya nikampa namba jamaa awasiliane nao akaambiwa aprint ministatement apeleke jamaa si akaprint akaja kwangu akaanza kung'ang'ania wewe ndio uliwasiliana nao na wewe unajuana nao nilichoka nilimweleza aende makao makuu ya hiyo kampuni nikamwelekeza ila aliondoka anatukana.
Kisa kingine niliwahi panda daladala kondakta alisahau kunicharge nauli nafika mwisho wa kituo ambako ndio gari inaishia nikakumbuka sijalipa nikatoa nauli nalipa tu nipo chini gari ikawekwa gear imegeuza konda chenji jamaa akanipiga mkono kuashiria njoo chukua bana dereva kakanyaga mafuta konda akafunga mlango aisee ilinibidi nicheke😅 nikaona wema gani wa kijinga hivi.
Share hapa nawe wadau tujifunze karibuni