Wema uliwahi kukuponza?

Aisee hatari sana maisha yanatufunza mengi
 
Kab
Kabisa unafanya ihsani kwa mtu ili umsaidie alafu anakuchomea
 
Tupo kwenye daladala.
Dada akanyanyuka tupishane kwenye siti, amekalia uchafu, nikamwambia dada samahani jitazame vyema huko nyuma umechafuka
Nikajibiwa wewe choko nini, kanichafua baba yako...
Nikatabasamu tu..
 
Nimecheka hadi michozi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nadhani unawafahamu vizuri
 
Sijaelewa kabisa
Kuna wale wamama wanacheza vikoba siku za marejesho zikifika wanakuja kukukopa kama unafahamiana nae ili warejeshe na wakirejesha hizo hela kwenye kikoba wanakopa tena kwenye kikoba, sasa unakuta ni mama ambaye unaheshimiana nae kwangu alikua ni mwalimu aliyenifundisha na nafahamiana naye hata hela ndogondogo alikua anakuja anakopo analeta, kuna siku ilikua siku ya marejesho hana hela kaja kwangu nimpe kiasi cha hela apeleke kwenye vikoba akanambia wao kawaida yao unaenda na hela wanahesabu kama kweli umerejesha then wanakukopesha mi nikampa hiyo hela mpaka leo haijaisha analipa kidogo kidogo
 
Hizo cha mtoto, Je, ukimsomesha mtoto wa ndugu yako, kaka yako kwa mfano. Baadaye kaka yako na mtoto wake huyo uliyemsomesha waanze kukusema vibaya kuwa ulijipendekeza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…