Wema uliwahi kukuponza?

Wema uliwahi kukuponza?

Katika maisha ya kutafuta nilikuwa nchi tofauti na TZ. Alikuja dogo ni ndugu wa rafiki yangu wa karibu sana ambae alinipokea mimi katika hiyo nchi na baadae akahama.

Kama kulipa fadhila na mimi nikampokea mdogo wake.

Huyo dogo alikuwa ni zaidi ya mshenzi. Kipindi nipo kazini analeta kwangu washkaji aliookota huko. Anapika chakula kwa fujo, anaacha vyombo vichafu, akageuza nyumba danguro kipindi sipo.
Kwa kipindi kifupi tu ikawa ni kama adhabu kuishi nae.

Ukimkanya dogo anapiga simu kwa kaka yake kuwa namtesa. Mshkaji nae bila kuuliza akawa anamuamini mdogo wake. Mwisho wa siku akamtafutia hifadhi kwingine na mimi akanichunia kabisa.

Dogo alinichafua mji mzima kwa wabongo kuwa nilikuwa namtesa.
Sikuwahi kujielezea kwa mtu yeyote ila nilijisemea mwenyewe kuwa anaejua ukweli ni Mungu tu na namuachia yeye.

Mwenye asili yake haachi, dogo akaendeleza upuuzi wake mpaka huko kwingine. Taratibu watu wakajua tabia zake na habari kumfikia ndugu yake.
Mwisho wa siku watu wakaanza kunifuata kunambia kumbe dogo ndio mshenzi. Kaka yake nae akaja kuomba msamaha.

Sasa hivi dogo ni teja la kufa mtu ametelekezwa Pakistani kawekwa poni na wauza waunga baada ya kuchukua mzigo kwa mali kauli.
Aisee hatari sana maisha yanatufunza mengi
 
Kab
#1. Nilimsaidia rafiki yangu kumuonesha mfereji wa Suez tukiwa darasa la 7 (kwenye ramani ya dunia).
Mwalimu alivyorudi ili apatiee jina la mtu wa kwanza kuuona jamaa alinikazia na alipewa zawadi ya daftari yeye kwenye group zima na kumwagiwa sifa kibao.

#2. Wakati nipo secondary, siku moja tumeandaa maji kwenye ndoo masafi ili baadaye tuyatumie.

Kumbe mama mmoja anatoka toilet akapita na kuyanawa yale maji.

Kwa vile sikutaka yawe makubwa, nilimsanua rafiki yangu kwamba ""maji yaliyo kwenye ndoo ile ya wazi usiyatimie ni machafu"".

Alivyo mjinga akamwambia pia yule mama kuwa Lucky Star anasema maji ya kwenye ndoo kubwa ya wazi tusiyatumie ni machafu.

Asee, nilijuta siku hiyo, maana yule mama alikuja na maswali ambayo sikuweza kumjibu kitu. Wema sometimes unamalipo hasi sana.
Kabisa unafanya ihsani kwa mtu ili umsaidie alafu anakuchomea
 
Tupo kwenye daladala.
Dada akanyanyuka tupishane kwenye siti, amekalia uchafu, nikamwambia dada samahani jitazame vyema huko nyuma umechafuka
Nikajibiwa wewe choko nini, kanichafua baba yako...
Nikatabasamu tu..
 
Nimecheka hadi michozi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nadhani unawafahamu vizuri
 
Sijaelewa kabisa
Kuna wale wamama wanacheza vikoba siku za marejesho zikifika wanakuja kukukopa kama unafahamiana nae ili warejeshe na wakirejesha hizo hela kwenye kikoba wanakopa tena kwenye kikoba, sasa unakuta ni mama ambaye unaheshimiana nae kwangu alikua ni mwalimu aliyenifundisha na nafahamiana naye hata hela ndogondogo alikua anakuja anakopo analeta, kuna siku ilikua siku ya marejesho hana hela kaja kwangu nimpe kiasi cha hela apeleke kwenye vikoba akanambia wao kawaida yao unaenda na hela wanahesabu kama kweli umerejesha then wanakukopesha mi nikampa hiyo hela mpaka leo haijaisha analipa kidogo kidogo
 
Habari wana jF, kama heading inavyojieleza share experience je wema uliwahi kukuponza katika harakati za maisha ukamsaidia mtu lakini ile huruma yako ikakupa matokeo hasi

Ndio, katika maisha ya kawaida haya mambo yapo sana mtaani, maofisini n.k

Haya hutokea kwa kuwa wanaosaidiwa huacha kuthamini mchango wa waliowasaidia badala yake ikitokea tofauti na matarajio yake lawama zinakuangukia wewe akidai kubwa ndiye uliyempoteza au kumuingiza mkenge.

Mimi iliwahi kutokea kwa uchache matukio kadhaa kuna jamaa alikosea kufanya malipo sasa nikamsaidia kuwasiliana na kampuni hiyo nilikuwa na namba yao ya WhatsApp , swali nilimpa namba akasema wewe nisaidie mimi sina bando alafu sijui naanzia wapi, alilipa kupitia tigopesa alipiga simu tigo wakamwambia hela ilishaingia kwenye account ya hiyo kampuni hivyo hatuna mamlaka nayo kuweza kuirudisha wasiliana na hiyo kampuni .

Hivyo nikaanza kuwasiliana nao nikachukua na namba ya jamaa na sms ya malipo wakasema tunaofanya kazi unarudisha ndani ya siku7 za kazi. Kwa bahati mbaya zilipita siku saba hazikurudi jamaa akanipiga kwahiyo vipi sasa hela yangu haijarudi , the way alivyouliza nikaona mmh

Isiwe tabu nikamwambia nakupa namba akasema wewe ulishaanza nao ulizia nikasema sawa . Mara ya pili nilipouliza wakasema mpaka siku 14 . Bahati mbaya zilifika haikurudi kwake ila hiyo kampuni wakadai wameshaitoa nilichofanya nikampa namba jamaa awasiliane nao akaambiwa aprint ministatement apeleke jamaa si akaprint akaja kwangu akaanza kung'ang'ania wewe ndio uliwasiliana nao na wewe unajuana nao nilichoka nilimweleza aende makao makuu ya hiyo kampuni nikamwelekeza ila aliondoka anatukana.

Kisa kingine niliwahi panda daladala kondakta alisahau kunicharge nauli nafika mwisho wa kituo ambako ndio gari inaishia nikakumbuka sijalipa nikatoa nauli nalipa tu nipo chini gari ikawekwa gear imegeuza konda chenji jamaa akanipiga mkono kuashiria njoo chukua bana dereva kakanyaga mafuta konda akafunga mlango aisee ilinibidi nicheke😅 nikaona wema gani wa kijinga hivi.

Share hapa nawe wadau tujifunze karibuni
Hizo cha mtoto, Je, ukimsomesha mtoto wa ndugu yako, kaka yako kwa mfano. Baadaye kaka yako na mtoto wake huyo uliyemsomesha waanze kukusema vibaya kuwa ulijipendekeza?
 
Back
Top Bottom