Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Huyu bwana ni wazi anasumbuliwa sana na uovu aliofanya Dar es Salaam, ambao ulitia ndani kuteka na kuua watu. Sasa hili linamchanganya sana kiakili, na huenda anapata ndoto na maono yanayomvuruga kichwa kutokana na damu alizomwaga moja kwa moja au kuratibu mipango ya damu hizo kumwaga.
Amejaribu sana kwenda kutubia kwa mapadri, lakini haijamsaidia. Amejaribu sana kuwaomba wachungaji na hata mashehe wamuombee japo yeye si mwislamu, lakini bado haisaidii.
Kuna wakati taswira za uovu aliofanya zikimjia analia kama mtoto. Anajitahidi kwa kila njia kushiriki mambo ya kidini, lakini haisaidii. Damu alizomwaga zinazidi kumwandama tu. Akiona watu ambao ni kama wazazi, wake, au watoto, anakumbuka kuna mtu alishiriki kumwaga damu yake na kuwanyima hao watu huduma na msaada kutoka kwa huyo mtu. Inamchanganya sana, na kutaka kuwasaidia kama namna ya kupunguza uzito wa maumivi ya mambo aliyofanya. Kuna wengine hata ameanza kuwaita rafiki zake, akijua wazi ilikuwa awafutilie mbali.
Sasa amekuwa na fikra kwamba akiwafanyia wema kina baba na kina mama ambao ni kama wazazi wa wale aliomwaga damu zao, au wale ambao ni kama wake wa aliomwaga damu zao, labda atapata unafuu fulani, kwamba wema huo utasaidia kufunika uovu aliofanya akiwa Dar es Salaam. Kuna wakati mambo yalimzidi hadi ikaamuliwa apumzike kwa muda.
Nataka nimwambie wazi, damu alizoshiriki kumwaga akiwa Dar es Salaam zitamwandama siku zote, na hakuna kuombewa na wachungaji wala mashehe kutakakomsaidia. Wala hakuna wingi wa wema atakaofanya utafunika uovu aliotenda huko nyuma. Kuna kila dalili kwamba anavurugikiwa akili, na nimwambie wazi, hizo ni dalili za mwisho mbaya unaomsubiri. Jambo moja tu litakalomtoa katika kuchanganyikiwa aliko nako ni kukiri hadharani na kwa familia alizoziathiri kwa uovu wa aliyotenda na kuomba msamaha, ikibidi hata aende jela. Akifanya hiyo toba ya kweli ndipo Mungu anaemtafuta kwa bidii atakuwa tayari kumpokea. La sivyo tatizo la afya ya akili linamnyemelea, na huenda wengine wakahisi ni bora apotezewe kabla hajaanza kutoa siri.