Wema unaofanya ukiwa Arusha kamwe hautafunika uovu uliofanya ukiwa Dar es Salaam!

Watu wa Kolomije tunasema Amina kwa kila jambo.Kwamba Albert anajaribu kufanya kitubio akiwa Arusha lakini bado toba yake haikubaliki? basi itabidi afanye kuendeleza kufanya matendo mema Mungu atapokea toba yake
 
Ndio unasamehewa lakini matokeo ya ubaya uliotenda lazima uubebe ndio msalaba wako...

Mfano umengonoka ovyo uko ukapata ukimwi afu urudi kuomba toba,, ndio unasamehewa na Mungu but ukimwi utaishi nao mpaka ukuue.
Sio kila baya limpatalo mwanadamu ni matokeo ya dhambi alizotenda.
 
Imeandikwa; dhambi zenu zijapokuwa nyekundu kama damu mkitubu zitasafishwa ziwe nyeupe kama theluji! Muhimu hapo ni toba ya kweli kutoka moyoni.
Sisi wakatoliki tunadundishwa ukimkosea Mungu na wanadamu lazima.utubu kwa Mungu na wanadamu. Kujifanya unacheza mziki eti unapotezea haisaidii utacheza segere zote ila raha hutaipata.

Ni kwa mujibu wa Askofu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu la Tabora.
 
Ndio unasamehewa lakini matokeo ya ubaya uliotenda lazima uubebe ndio msalaba wako...

Mfano umengonoka ovyo uko ukapata ukimwi afu urudi kuomba toba,, ndio unasamehewa na Mungu but ukimwi utaishi nao mpaka ukuue.
We jamaa huu mfano umeeleweka sana.

Kama yule jamaa ambaye amezana kwenda Gym baada ya kufukuliwa kwa miaka mingi. Mungu atamsamehe kwa ushoga wake ila sio kwa madhara yale ataishi nayo milele
 
Ametubu,lakini haisaidia........................mkuu kwani mtu anapotubia kuna sauti inatoka mbinguni kuja duniani kuwambaia kuwa toba yake imekubalika au haijakubalika ?
 
Uzi mzuri sana.
 
Huna tofauti na nyumbu ambao wataona mwenzao analiwa na simba na kuangalia tu kwa kushangaa, kisha wakaendelea kula, kama vile kusema mwacheni simba aendelee kula, na kusahau kuna siku itakuwa zamu yao kuliwa!
Endapo Ni Kweli Alifanya Mabaya (Maana hakuna uthibitisho) na Sasa anafanya Mema, Basi Tuhesabu Mema yake.
Utusamehe kama na sisi tunavyosamehe waliotukosea..

Yona aliona wivu kwa Watu Wa Ninawi kufanya toba na kusameheea mahali alipodhani wangehukumiwa.

Mbinguni malaika wote hufurahi mwenye dhambi mmoja anapotubu.
 
Ametubu,lakini haisaidia........................mkuu kwani mtu anapotubia kuna sauti inatoka mbinguni kuja duniani kuwambaia kuwa toba yake imekubalika au haijakubalika ?
Jamaa anajipa Umungu. Wa kupokea na kukataa toba.Hakuna mwanadamu asiyekosea.Kutubu ni dalili kwamba anayetubu anajua yeye ni mwanadamu na anakosea.Huyu "malaika" anayeendelea kushutumu na kuhukumu aendelee na kazi yake ya kujua wanaosamehewa na wasiosamehewa.
 
Wewe ubaya wake ulikuathiri vipi? Kwa nini uwe mwepesi wa kuongelea kusamehe kwa mambo ambayo hayakukuumiza binafsi? Wewe angekuwa ni mume, au kaka au mtoto aliemdurumu haki ya kuishi ungesema haya unayosema hapa?
 
Acha uongo
 
Hujamwelewa. Anachomaanisha ni kwamba ametubu kwa mapadri, kaomba aombewe na wachungaji na mashehe, nk, lakini haijasaidia kumtuliza akili. Haimwondolei sense ya kuwa guilty na kumwaga damu za watu, ndio maana bado analia lia tu kama mtoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…