KERO Wembamba wa barabara za kutoka Jiji la Arusha huleta foleni kubwa mida ya jioni

KERO Wembamba wa barabara za kutoka Jiji la Arusha huleta foleni kubwa mida ya jioni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Hassanjk

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2023
Posts
333
Reaction score
689
Kwanza nimpongeze sana mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa jitihada zake za kusaidia wananchi;
Naamini na hili lipo kwenye mpango kazi wake ila kwa kuchangia tu;
Kuna vipande vitatu vya Barabara VIFUPI KABISA ila vina sababisha jiji la ARUSHA lisimame Asubuhi na jioni...

1. Ukitoka mnara wa Saa (Clock tower) Kwenda round about ya Kijenge, takriban meta 800, jioni unaweza kutumia nusu saa hadi lisaa na zaidi (Barabara hujifunga) Na hii ni kwa sababu kipande hicho kinaunganisha mitaa maarufu ya Kijenge juu, kijenge chini, Njiro, Moshono, by pass ya Chuo cha Mandela, na pia ni by pass ya kuingia Barabara ya moshi Arusha. Naona ipo haja ya kukipanua kwa haraka kiwe njia nne na kupanua round about ili iendane na maboresho hayo.

2. Kuna kipande kingine kama km 1.2kms kutoka Shoppers hadi Majengo ya chini (Kwa sefu) Hiki kinaunganisha mitaa maarufu ya Mbauda, Kisongo, Monduli, Majengo ya chini na majengo ya juu. Hiki walianza kupanua ziwe Barabara nne ila wakaishia njiani; natamani wamalizie;

3. Kuna kipande kingine cha kufilter magari yasipite mjini kati kama cha meta 350 (kutoka Faya Kwenda round about ya Unga ltd); hako ka kipande kapo busy asubuhi hadi jioni, unaweza kuendesha hapo kwa dkk 15 hadi nusu saa? Nashauri napo wapanue pawe njia nne

Nafikiri tunasumbua Traffic bure kwani hata kwa akili ya kawaida, mitaa yote hiyo haiwezi kuunganishwa na kipande kimoja cha barabara ya njia mbili ikapitika

4. Mipango itakayofuata; wapanue Barabara ya Njiro kwani inatumiwa na watu wanaopitia by pass kuingia mjini na hivyo kuifanya iwe busy sana hasa muda wa Asubuhi na jioni.
 
Mji kama kiberiti izo barabara ulizo taja zita panuliwaje nafasi hamna . Barabara ya Njiro haina foleni. Ya moshono haina .ya Phillips haina labda ukitoa jam zinazo sababishwa na round about za ayo maeneo ...uko kwingine barabara ni finyu hazina nyama ya kuongezea bila kuvunja vibanda vya watu .

Mabus na magari makubwa yana jitahidi sana kukatisha kwenye vibarabara vya Arusha mjini
 
Bypass uwa ipo tupu kabisa lkn mnavimba huko kwenye daladala
 
Barabara mfano ya kutoka clock tower hadi round about ya kijenge haiwezi kutanuliwa kuwa njia nne sababu hakuna nafasi kabisa, kuna hospital ya icc, hoteli kubwa kubwa kama kibo palace, Golden rose, The Arusha hotel, shule ya kimataifa ya brebun hizo zote zipo pembeni kabisa ya barabara
 
Barabara nyembamba hapo hapo pongezi. Nchi inapitia kipindi kigumu sana.
 
Kuna barabara ipo Ungalimited Ile ya mwisho wa reli.... Inapopita hosp. Ya darajambili na shule ya Felix mrema.... Inaweza kutumika kama mchepuko kuelekea njiro Ile naamini ingepunguza mno msongamano sijui kwnn sirikali hailioni hili..... Hili jengine nalo mkalitizameni,,.
 
Bypass uwa ipo tupu kabisa lkn mnavimba huko kwenye daladala
By Pass inatoa watu USA RIVER kuwapeleka Kisongo, sasa inahusiana nini na watu wanao ingia na kutoka mjini ?
Hata hivyo nimeandika hapo kuwa, long term plan wapanue barabara ya Njiro kwani kwa sasa inatumiwa sana na magari yanayotokea by pass kuingia mjini na hivyo kuleta msongamano mkubwa kuanzia Njiro nanenane ambapo watu wanaotumia magari ni wengi
 
Kuna barabara nyingine nilipita hapo Arusha iliniacha hoi kabisa.
Inatokea maeneo ya National Milling kuelekea lilipo 'dampo'.

Hapo katikati kuna sehemu nguzo za umeme ziko katikati kabisa ya eneo la barabara jambo ambalo limesababisha kuwe na vibarabara viwili (kimoja kushoto ya hizo nguzo na kingine kulia)ambavyo ni size ya gari moja tu.
Eneo hilo huwa na jam ya kutisha haswa nyakati za jioni.
 
By Pass inatoa watu USA RIVER kuwapeleka Kisongo, sasa inahusiana nini na watu wanao ingia na kutoka mjini ?
Hata hivyo nimeandika hapo kuwa, long term plan wapanue barabara ya Njiro kwani kwa sasa inatumiwa sana na magari yanayotokea by pass kuingia mjini na hivyo kuleta msongamano mkubwa kuanzia Njiro nanenane ambapo watu wanaotumia magari ni wengi
Mmh Kaka kwakweli bypass haifik mjin mkuu
 
Back
Top Bottom