Wengi msimshangae Ali Kiba, hakuna mtu anayempenda Diamond kama Ali Kiba

Wengi msimshangae Ali Kiba, hakuna mtu anayempenda Diamond kama Ali Kiba

Kiba ni mwimbaji mzuri tu....dai ni mbunifu zaidi ya kiba........
 
Alikiba hamtegemei Diamond hata kidogo na niwaambie tu jambo hakuna kitu rahisi kama mtenda kukubali kusuluhishwa kuliko mtendwa. matatizo yalianzia kwa diamond hili lipo wazi na kama mkisema jambo la kiki mnatakiwa mjue Alikiba ndo msanii wa pili Tanzania kuleta tuzo ya kimataifa nyumbani. msanii wa kwanza ni jay dee,
Fikiria upya
 
Mkafanye PRESS CONFERENCE basi au sio mleta mada ili uma wa watanzania ujue akiwemo nasibu na ali pia ...mana sidhan kama huku jamii forum they can waste their time kufatilia hizi thread
 
Ivi mimi ndio uzee unanikaribia au nawehuka?uyu mtoto Kiba si ndio ambae kaimba Cinderella?tunaposema anamtegemea Diamond tuna maana ipi hasa ni kipi anakifanya sasa ivi au anakipata hakuwahi kukifanya mwanzoni naamini Kiba alikuwepo hapo kitambo sana tena ni kati ya watoto wazembe sana maana anatumia nguvu ndogo sana kujitangaza mpaka hapo alipo ila angekua na juhudi angekua bora zaidi ya hapo na kwa nyimbo anazofanya ni aibu kusema zinategemea agombane na mtu ili zisogee mbona toka zamani watu wanasikiliza ngoma zake ivi aligombana na nani mpaka tukaisikiliza nakshi nakshi au single boy ni upuuzi kuamini wimbo wake wa Aje umefika hapo kisa beef na fulani huko nje ambako wameukubali nako ni wapuuzi kama sisi pia,simply Kiba ana fan base yake kubwa anayo toka kitambo kabla ya Diamond kama kuna mtu anamsikiliza Kiba kisa hampendi Nassibu basi hana akili maana muziki ni burudani ya nafsi na kwa nini waende kwa Kiba sio Timbulo au Barnaba.
Diamond ni kati ya vijana ambao ni talented sana yeye sio mfanyabiashara tu ila amejifanya kua biashara iko wazi kabisa ana mashabiki wake wengi sana kwa sababu zao ni upuuzi aibuke shabiki wa Kiba akatae nguvu ya Diamond kwa muziki wake lazima tukubali haiwezekani awepo msanii mmoja popote pale na hakuna wa kuzui ushindani kwenye muziki hii hali ipo toka enzi hizo,bado natamani mtu ambae hana timu akiwa na akili timamu aniambie kwa nini uwepo wa Kiba unamtegemea Diamond na huo utegemezi umeanza lini.
Jamaa bravo. Good analysis.
 
Nafurahia sana mambo haya...

Mnalazimisha kugombana na kiba halaf yy hana time

Mnatoa nyimbo mnavyotaka lakin yy yupo kimya

Mnamlazimisha aongee halafu yy anaingia studio na kuwaambia Kama vip Aje

Mnatengeneza skendo zenu na mademu wenu yy anacheza gofu gymkana.... Msilazimishe ugomvi maana kiba hana ugomvi na mtu
 
1e9434148d0abd3fe34016daa68a58aa.jpg
.
.....maneno ya domo aka chaijaba ayo Leo kasahau anasema yaishe..kingne kiba anauza mziki wake Sony,dizzer, na blog zingne zaid Ya 750 dunianai kote xo atuwez uza nyimbo zetu kwenye ka blog uchwara ka uko tandale....
 
Sijawah kusikia kiba akiongea maneno ya mipasho juu ya diamond zaid ya jamaa (diamond) kumpaka jamaa,akachuku dancers wake,akampaka jamaa pamoja na familia kwa ujumla!,ndio jamaa anatakiwa kusamehe ila msamaha wa kweli lazma mhusika awe na utayari so lets wait!
 
Umenena Ukweli
huo ndio ukweli halisi!!
Kiba anatembelea kick kwa Diamond
kwanza kiba hana Busara,Hana nidhamu
hajui kujieleza,Malengo Zero
Nimtu asiye kwenda na wakati
Majivuno nizaidi ya Mwanamke!!
Kiukweli hata Mungu anaona wapi ampaishe mtu
laiti kama kiba angelikuwa na Mafanikio kama ya Diamond sijui ingelikuwaje!!

Yote na yote Diamond bado ni kioo cha watanzania
Ukweli ni huu:
Kiba ni kama mwanamke mrembo sana,anayeamini urembo wake unambeba hivyo hana haja ya kujituma sana akiwa na mumewe!Mumewe anaridhika na urembo wake japo kama angejituma kwa juhudi basi ingekuwa balaa!

Diamond ni kama mwanamke ambaye yuko katikati,sio mbaya wala sio mrembo!Hivyo anaamini kuendelea kumuweka mumewe ndani ni kwa kujituma kwa juhudi zote na kuwa mnyenyekevu kwa mumewe!Mumewe anajikuta anaridhika na hilo na kudumisha ndoa maradufu!

Sijui umeelewa???
 
Naanzisha ikiwa ni majibu Kwa Uzi huu hapa.
Kwanini Ali Kiba hataki bifu lake na Diamond liishe?

Wengi wanamshangaa sana allykiba kwann hataki kupatanishwa na Diamond. Jibu ni simple tu..Dogo Ali yupo kwasababu ya kiki ya Diamond. Unamkumbuka kanumba na Ray ( Kigosi). Japo Ray aliaanza tokea zamani kwenye filamu na maigizo but hakuweza kumfikia Kwa nusu kipaji cha kanumba.

Kipind kile watu walikuwa wanawafananisha Ray na Kanumba..!! Kufaninishwa kule kulifanya hata wasanii km JB waonekane hawajui sana Kwa Ray. Japo hawa wawili hawakuwa na bifu but walitengeneza kaushindani ambapo kalikuwa kanambeba sana Ray..!! Leo kanumba hayupo, Ray kapotea sana..Ray hatrend kwenye muvi tena...anatrend Kwa mikorogo tu.

Tuje Kwa kiba.
Kiba anajua kabsa Siku atakayopatana na Diamond basis ndo mwisho wa kutrend. Kwa miziki anayoimba kiba anahitaji promo sana. Ile hata kumuandika hivi ni kumpa promo.

Kuna kipind Fulani nilikutana na abdu kiba( mdogo wa kiba) nilimuuliza mbn mnaweka bifu sana Kwa diamond wakati hana time na nyie..!! Alichojibu abdu alisema ni masuala ya kibiashara tu. Ali hamchukii diamond km watu wanavyodhani, but kuwa na bifu na Diamond kunamfanya anapata attention.

Abdu aliniambia pia hii bifu ilitengenezwa na clouds FM ili wawe wanapata watu kwenye fiesta Kwa uwepo wa alikiba kwakuwa diamond anawazinguaga clouds kwenye shoo za fiesta za mikoani.

Tusimlaumu sana kiba..kiba siyo msanii mzuri, yeye mwenyewe anajijua na hawezi kuwa msanii Mkubwa akikosa attention za diamond...!! Kiba bila diamond hana kitu.

Kwann diamond anamuhitaji kiba kipindi hiki?
Diamond mfanya biashara..na anataka kuwashawishi wasanii wa bongo fleva waingie makubaliano kwenye website yao ya kuuza mziki. Diamond mtoto wa mjini yupo radhi ajijushe ili apate mkwanja. Na Diamond anajua siku akipatana na kiba tu basi kiba Keisha Habari yake.

But kiba utatumia mgongo wa dai mpaka lini. ?

Ushauri Kwa diamond
Hawa wasanii wako wadogo kabla ya kutoa jiridhishe uwezo wao. Walianza vizuri but naona uwezo wao mdogo sana. Angalia kijuso ray/Dada ako sijui hata wameimba nini?

Niambie ya harmonise nyimbo ya kawaida sana. Mlianza vyema naona wenzako watakuangusha soon.hata producer laizer naye angalia kiwango chake.

mm nlijua we mtu mzima na akili zako kumbe naz tupu
 
Ivi mimi ndio uzee unanikaribia au nawehuka?uyu mtoto Kiba si ndio ambae kaimba Cinderella?tunaposema anamtegemea Diamond tuna maana ipi hasa ni kipi anakifanya sasa ivi au anakipata hakuwahi kukifanya mwanzoni naamini Kiba alikuwepo hapo kitambo sana tena ni kati ya watoto wazembe sana maana anatumia nguvu ndogo sana kujitangaza mpaka hapo alipo ila angekua na juhudi angekua bora zaidi ya hapo na kwa nyimbo anazofanya ni aibu kusema zinategemea agombane na mtu ili zisogee mbona toka zamani watu wanasikiliza ngoma zake ivi aligombana na nani mpaka tukaisikiliza nakshi nakshi au single boy ni upuuzi kuamini wimbo wake wa Aje umefika hapo kisa beef na fulani huko nje ambako wameukubali nako ni wapuuzi kama sisi pia,simply Kiba ana fan base yake kubwa anayo toka kitambo kabla ya Diamond kama kuna mtu anamsikiliza Kiba kisa hampendi Nassibu basi hana akili maana muziki ni burudani ya nafsi na kwa nini waende kwa Kiba sio Timbulo au Barnaba.
Diamond ni kati ya vijana ambao ni talented sana yeye sio mfanyabiashara tu ila amejifanya kua biashara iko wazi kabisa ana mashabiki wake wengi sana kwa sababu zao ni upuuzi aibuke shabiki wa Kiba akatae nguvu ya Diamond kwa muziki wake lazima tukubali haiwezekani awepo msanii mmoja popote pale na hakuna wa kuzui ushindani kwenye muziki hii hali ipo toka enzi hizo,bado natamani mtu ambae hana timu akiwa na akili timamu aniambie kwa nini uwepo wa Kiba unamtegemea Diamond na huo utegemezi umeanza lini.
Mkuu umeongea vizur mno...
 
Mkuu unajua kiba akifanya show dk 40 analipwaje? Ni hela ambayo wengi wetu humu tunaitafuta kwa miezi kadhaa kama sio miaka, kwahiyo ushaur wangu kwako jitahidi utafute njia na wewe kama hizo za kiba ili utengeneze mtonyo, pambana m
inakula sh ngap?
 
Samahani mkuu naomba unieleweshe sasa utegemezi wa Kiba kwa Diamond na ingekua vema ukaniambia kaanza lini utegemezi huo.
Itakuwa kwel uzee unakunyemelea mkuu pole San a kama hutamvui umuhimu Wa chibu kwa kiba na kiba kwa chibu

Nimesoma vizuri post ila ninachoelewa Kiba yupo muda sasa tena ameshafanya hit song kibao kabla hata hajaanza uyu Diamond na Alli ana fan base yake hata alipopumzika kufanya ngoma bado fan base yake ilikua pale naomba unipe kwa kina nini ambacho Kiba anakifanya kwa msaada wa Diamond na hakuwahi kukifanya.
Soma vizuri post
 
Endelea kuota ndoto huku umechutama mwenzio anapiga shoo chalinze ya marekani na watoto wake wanaenda chooni sasa wewe unaeandika ukiwa tumbo wazi komaza vidole kwa kuchangia JF
 
Samahani mkuu naomba unieleweshe sasa utegemezi wa Kiba kwa Diamond na ingekua vema ukaniambia kaanza lini utegemezi huo.

Nimesoma vizuri post ila ninachoelewa Kiba yupo muda sasa tena ameshafanya hit song kibao kabla hata hajaanza uyu Diamond na Alli ana fan base yake hata alipopumzika kufanya ngoma bado fan base yake ilikua pale naomba unipe kwa kina nini ambacho Kiba anakifanya kwa msaada wa Diamond na hakuwahi kukifanya.
Usijibizane na hao watoto wanaotumia mgongo wa Diamond kutangaza biashara zao za vest na suruali Instagram kila siku wanatusumbua
 
Back
Top Bottom