T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Maisha ya bongo hayahitaji akili nyingi sana kama tupo Singapore. Wasomi hawathaminiki wala jamii haiwajali, maishq yetu hayategemei sana maarifa. Wabongo hatujengi kwa misingi ya ujenzi kwamba uite wasomi wataalamu, gari tunarekebisha gereji bubu ya walioishia la saba, wanasiasa vilaza wanalangua PhD, matapeli wanatumia dini.Ukiwa unatoka familia mbovu, masikini sana au za uswazi hata kama unashika namba moja darasani nafasi yako ya kufanikiwa baadaye maishani ni finyu ukilinganisha na wanaotoka familia bora hata kama hawafanyi vizuri darasani au ni vilaza.
Jamii kama hiyo hata mtu asiposoma anaishi. Sasa mtu kwao wana assets na mali hata kama kilaza akifungua duka la vipuri vya magari la kama 30M atashindwaje kuhesabu hela. Msomi mwenye akili na hana hela, ajira, mtaji akili zake azitumie wapi kwenye jamii hii.