Kwanza kabisa nimefurahishwa na uamuzi muliouchukua wa kuikomalia serikali ihakikishwe mnapewa haki yenu ya kikatiba ya kupiga kura, mimi naamini siku zote vuguvugu la mapinduzi ya kuiondoa serikali ya kidhalimu madarakani kwa njia ya kidemokrasia huwa inaanzia vyuo vikuu.
Sababu kuu ikiwa ni kwamba wasomi huwa wanauelewa mkubwa jinsi nchi inavyoendeshwa kwa wakati huo, na huweza kutambua ndivyo sivyo kirahisi zaidi kutokana na uelewa mkubwa wa kuchambua mambo pamoja na kufanya ulinganishi wa utendaji kazi wa serikali za nchi zilizoendelea.
Dr. Wilbrod Silaa anahitaji kura ya
'NDIO' kutoka kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu vya umma na vya private pia, na sababu zipo kama zilivoainishwa hapo chini:
- Mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi unahitaji marekebisho, tunahitaji mfumo utakaozingatia mahitajia haliasia ya mwanafunzi. Na hivo kutoa fursa kwa wanafunzi wasio nauwezo ( walio wengi ndani ya taifa letu ) kunufaika kwa kupata elimu ya juu ambayo ni haki yao.
- Board ya mikopo inahitaji restructuring ili iwe na ufanisi katika utendaji kazi, kwani wanafunzi wanahitaji pesa zao za kujikimu ziwafikie kwa muda muafaka wawapo vyuoni na mafunzoni. Tofauti na sasa ambapo wanafunzi wengi wanateseka na kuishia ombaomba ati sababu board haina pesa, wengine wanaishiwa kupewa pesa baada ya semester kuisha. Hapa tusitegemee kutoa wasomi waliobobea.....elimu ya juu inahitaji investment ya kutosha sio lele mama tu!!!
- Board ya mikopo inahitaji kuwa na strategy endelevu kwenye loans recovery, tofauti na sasa hatuoni efforts zozote zinazofanywa na board ya mikopo katika kudai wale waliokwisha neemeka na mikopo. Mimi nikiwa ni mmoja wapo! na ninatamani nilipe mkopo wote ili wadogo zangu nao waneemeke na hizi pesa.
- Tume ya vyuo vikuu (TCU) na aibu; anahitajika mtu makini sehemu hii pia aishauri serikali mikakati endelevu....na sio hawa wanaojiita ma-profesa wachumia tumboni! wanaowakosesha watanzania haki yao ya kujiunga na vyuo vikuu kutokana na makosa ya kiufundi ambayo inadhihirisha zaidi wamekurupuka. .....ati mtu anajisifu kwa kuanzisha online application portal ....huku akijua wazi hajatoa elimu ya kutosha kwa umma ni jinsi gani ina-work, hakuna facilities za kutosha kufanikisha...shame on you prof!!!!!!!! Naomba nieleweke kuwa sipingi teknolojia hii...lakini sio realistic kivile kwa mazingira mabovu ya Tanzania jamani.
Mwisho kabisa napenda kuwaambia wanafunzi wa vyuo vikuu, esp. university of Dodoma ya kwamba acheni
"UNAFIKI" wa kujifanya mnapesa zilizowazidia hadi kumdhamini kikwete. Nani asiyejua mnawasumbua ndugu, wazazi, walezi au wafadhili wenu wengine wawatumie pesa ya kuwasukuma siku mbili tatu ati sababu board imechelewa kuwapa mikopo au wakati mwingine mnakuwa mmeishiwa kabla hata ya semester kuisha. Si vibaya kusaidiana, lakini sisi ndugu, wazazi wenu, walezi wenu, wafadhili wenu tuna hali ngumu sana ambayo mnaijua kutokana na gharama za maisha kupanda kila kukicha. Sasa sisi tunasema tumeamua mwaka huu hatumpi kura huyo JK wenu.....Tuone nani ni Msomi wa kweli......................sisi au ninyi!!!
2010 Hatudanganyiki; KURA ZETU ZOTE ZA NDIO NI KWA Dr. WILBROAD SLAA