Japhari Shabani (RIP)
R I P
- Jan 16, 2007
- 721
- 178
Mwanzo » Habari
60,000 vyuo vikuu hawatapiga kura
NA WAANDISHI WETU
4th October 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Wako likizo lakini walijiandikisha vyuoni
Havitafunguliwa kabla ya Uchaguzi Mkuu
Kiravu asema hawana la kufanya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imepigilia msumari wa mwisho juu ya hatma ya upigaji kura kwa zaidi ya wanafunzi 60,000 wa vyuo vikuu nchini ambao wako likizo lakini wakiwa wamejiandikisha kwenye vituo vilivyo vyuoni kwao.
Mkurugenzi wa Nec, Rajabu Kiravu, akizungumza na NIPASHE jana alisema hawana cha kufanya juu ya wanafunzi walioko likizo kwa kuwa mchakato wa kuboreshwa kwa daftari la wapigakura ulishafungwa, kwa maana hiyo wanafunzi hao hawatapiga kura.
NIPASHE ilimtafuta Kiravu kuzungumzia habari hizo baada ya kufanyika kwa kongangamamo la wahitimu na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lililofanyika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao walitoa rai kwa serikali kufanya jambo moja kati ya mawili ili kuwapa fursa ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Walitaka ama waruhusiwe kupiga kura wakiwa likizo kwa kuwekewa utaratibu maalum huko waliko, au vyuo vifunguliwe kabla ya Oktoba 31, mwaka huu ili wapate fursa hiyo kwani walijiandisha wakiwa vyuoni.
Wanafunzi hao na wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini, walitoa malalamiko hayo jana kwenye kongamano ambalo lilijadili masuala ya uchaguzi mkuu.
Walisema kama hawatapewa fursa hiyo, watakuwa wananyima haki yao ya msingi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba ya Tanzania ambayo inatoa haki kwa kila raia kuchagua kiongozi anayemtaka.
Kwa kawaida vyuo vya elimu ya juu nchini hufunguliwa kwa muhula wa kwanza wa masomo kati ya Septemba na Oktoba, lakini mwaka huu vyuo hivyo vitafunguliwa Novemba baada ya Uchaguzi Mkuu.
Kiravu alisema Nec ilitoa muda kwa wananchi wote wakiwemo wanafunzi kubadilisha taarifa zao ili kupiga kura katika maeneo yao mapya na kwamba kama hawakufanya hivyo wao hawawezi kutoa muda mwingine kwa kuwa daftari limeshafungwa.
Tuliishatoa nafasi tena kwa kutangaza kwa wananchi wakiwemo wanafunzi kwamba mtu anayetaka kubadilisha taarifa zake wafanye hivyo, lakini kama hata hao wanafunzi walishindwa kufanya hivyo daftari limeishafungwa na sasa tunafanya mambo mengine alisema, Kiravu.
Akizungumza katika kongamano la jana, mgombea wa ubunge Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam kupitia Chadema, John Mnyika, alisema, mwaka huu watawatumia wanafunzi wa vyuo vikuu kama mawakala ili kuhakikisha wanalinda kura zao zisiibwe.
Aidha, alisema chama chake katika jimbo lake kitaweka mawakala ambao ni wafanyakazi pamoja na wale watakaoteuliwa na viongozi wa kata wa Chadema na kwamba watakuwa na mawakala wa aina tatu wakiwemo wafanyakazi.
Kuhusu serikali kufungua vyuo vya elimu ya juu kabla ya uchaguzi mkuu, Mnyika aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuharakisha mpango huo ili kuwawezesha wanafunzi kupiga kura maeneo waliyojiandikishia.
Alidai kuwa serikali imefanya makusudi kuchelewesha kufungua vyuo kwa maagizo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili wanafunzi wasiweze kukipigia kura Chadema na kuongeza kwamba mabadiliko ya kweli katika nchi hii yataletwa na wasomi.
Alisema kama wasomi wasipoleta mabadiliko kwa kuindoa CCM madarakani watakuwa wanawasaliti wananchi hasa waliopo vijijini.
Alijigamba kuwa wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo hawakulipwa posho wala kusafirishwa kwa mabasi kama inavyofanya CCM katika mikutano yao na kwamba walikwenda wenyewe hali inayoonyesha kwamba wana uzalendo wa kweli na mapenzi kwa Chadema.
Mnyika ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema ni vigumu wananchi kuendelea kukiamini CCM kwa kuwa ahadi walizotoa mwaka 2005 wameshindwa kuzitekeleza na badala yake wameendelea kutoa zingine mwaka huu.
Aliwataka vijana hao kuhakikisha kila mmoja anashawishi watu wanne hadi watano ili kukipigia kura Chadema mwaka huu ili kukiwezesha kuingia madarakani na kuunda serikali.
Mnyika aligusa hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wapandwe na jazba baada ya kuwaambia kuwa Chadema ikiingia madarakani kitu cha kwanza itakachofanya ni kuvunja Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) kwa kuwa imeshindwa kukidhi mahitaji wa wanafunzi na kuunda mMamlaka ya kugharamia masomo ya elimu ya juu.
Alisema mamlaka hiyo itakuwa inasomesha wanafunzi wote elimu ya juu bure ambapo wataunda matawi katika kila mkoa ambayo yatakuwa yanashughulikia utoaji wa elimu ya juu bure kwa wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi hao wakichangia mada kwenye kongamano hilo walisema ikiwa serikali haitafungua vyuo itakuwa inawanyima haki yao ya kikatiba.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi kutoka Chuo cha Biashara (CBE), Lutashobya Lutashobya, alisema Nec inatakiwa kuliangalia suala hilo mapema iwezekavyo ili wanafunzi nao wapate haki yao ya kupiga kura.
Tunashangaa kwa nini vyuo havifunguliwi mapema, CCM inataka kuhujumu haki yetu ya kikatiba ya kupiga kura na kumchagua kiongozi bora, lakini hili likishindikana itabidi tuhamasishane sisi kwa sisi ili kuwashawishi wananchi wanaovaa nguo za rangi ya kijani ambao wanaoipenda Chadema, lakini wanaogopa kusema wazi ili wakipigie kura chama hicho, alisema.
Mhitimu mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Docas Mnanga, aliitaka Chadema kutimiza ahadi yao ya kuvunja haraka HELSB na kuunda mamlaka ya kugharimia masomo ya elimu ya juu.
Aliunga mkono hoja ya Chadema ya kuvunja bodi hiyo kwa madai kuwa inachangia kuwepo vitendo vya rushwa na imeshindwa kuonyesha ufanisi tangu ilipoundwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo, alisema Ilani ya chama chochote cha siasa inatakiwa kutoa majibu kwa wananchi kuwa itawafanyia nini.
Nimejaribu kupitia Ilani za vyama vyote, lakini ya CCM inasema itajenga barabara au kuchimba visima hii maana yake ni miradi sio dira, kwa kawaida ilani inatakiwa kubebwa na dira sio miradi, alisema.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na Naibu wake, Gaudensia Kabaka, walipotafutwa kupitia simu zao za mkononi kuelezea madai ya wanafunzi hao hawakupatikana.