Rugaijamu
JF-Expert Member
- Jul 10, 2010
- 2,942
- 1,298
NEC na Prof. Maghembe bado wanaharalisha kuwanyima wanafunzi karibu 60,000 wa elimu ya juu kutokupiga kura kitu ambacho ni haki yao kikatiba. Madai ni kwamba wakati wa kurekebisha daftari la kudumu la wapiga kura hawakufanya hivyo na kujikuta vituo vyao vya kupigia kura ni vyuoni na vyuo vitafunguliwa baada ya uchaguzi (HabariLeo, 5/10/2010).
Hivi wangewezaje kubadili vituo hivyo wakati walikuwa madarasani na mikoa ilikuwa na tarehe tofauti? Hivi gharama za kwenda huko kubadili vituo wangepewa na nani? Kama ni ngumu wao kusafiri kwenda kupiga kura kwenye vyuo vyao basi ingekuwa ngumu vile vile kwenda kubadili taarifa zao?
Lakini si kwamba wanaweza kumchagua Rais lakini si madiwani na wabunge? Basi wapeni fursa ya kumchagua Rais wamtakaye, la sivyo huo ni uvivu wa kufikiri na kuchambua mambo!
Pia wakati huo ratiba/karenda za vyuo zilionesha siku ya kupiga kura vyuo vingekuwa vimefunguliwa.Hizi ni mbinu zao!