Wengi wanamkubali Bob Marley ila Mfalme wa Reggae duniani ni Lucky Dube

Wengi wanamkubali Bob Marley ila Mfalme wa Reggae duniani ni Lucky Dube

Hizi mada achana nazo ndugu hujui kitu!!! Wewe fuatilia ndoa ya haji manara ndio level yako
 
Lucky dube alikuwa vizuri kwenye aina yake ya mziki ambao yeye alituaminisha kuwa ni rege sababu aliimba na kucheza kwa kurukaruka. Ni kwaito flaan hivi yenye vibe ya rege.
Boby huyu aachwe tu Kama alivyo na sidhani Kama ni busara kulinganisha Boby na mtu mwenye viwango vya Senzo
Naunga mkono hoja
 
Bob kwa lucky ni mchumba tu, hakuna nyimbo ya bob naipenda ila za lucky mbaya ni kidogo sana tena moja tu inaitwa drakula huwa siipendi kabisa
Nyie ndio matoa tuzo ya msanii bora wa hip hop kwa Bil Nas
 
Sio kama simpendi Lucky Dube ila muziki wake nilianza kuupotezea pale alipohusishwa na kifo cha Senzo

"Cᵒᵃᶜᵏʳᵒᵃᶜʰ ⁿᵘʰ ᵇᵘˢˢⁱⁿᵉˢˢ ⁱⁿⁿᵃ ᶠᵒʷˡ ᶠⁱᵍʰT"
Ila senzo ni Mzima, mambo haya
 
Dunia yote inamtukuza na kumuhusudu Bob Marley (Culture?) kama mfalme wa muziki rege, sijui wanatumia vigezo gani hasa. Wanamshusha na kumchukulia poa Lucky Dube sijui kwakua Bob aliuawa ndio wanakua na sympathy naye.

Kwa upande wangu japo Dube alimuheshimu Bob ila kwangu dube ndio mfalme wa muziki wa rege duniani. Nyimbo safi zenye ujumbe mwanana, beats zilizoenda shule performance za hadhi ya nyota 15 alizofanya! Nina uhakika Bob angekuwepo wakati Dube Anatoa Album zake 3 za mwanazo (hasa Slave) angempigia magoti Dube na kumsujudu kwa nyimbo bora alizotoa.

Huyu jamaa anajua hasa sikiliza nyimbo zake zote 80% lazima uzipende tu, ukutaka ujue ukali wa huyu mtu angalia Live performance zake utadata.

Najua mtanipinga humu na kunipopoa ila kwangu huyu ndio nishampitisha kua Mfalme wa Rege Duniani, hakuna mwingine.

Ninauhakika huko alipo kapumzika kwa amani maana katimiza kile kilichomleta duniani (Kuhamasisha watu waamke) japo alikua na mapungufu yake kama mtu yoyote yule ila naamini huyu mtu mbingu ni yake na tunaweza mwita mtakatifu kwa kazi yake nzuri.

Sikiliza hizi



Hujui reggae
 
Lucky dube uki sikiliza ngoma zake au skip.. sio kama bob ngoma nayo ikubali ni moja ..uko juu naona watu wana komaa na bob ili waonekane wana jua
 
Dunia yote inamtukuza na kumuhusudu Bob Marley (Culture?) kama mfalme wa muziki rege, sijui wanatumia vigezo gani hasa. Wanamshusha na kumchukulia poa Lucky Dube sijui kwakua Bob aliuawa ndio wanakua na sympathy naye.
Pale machawa wa wasafi wanapojikuta wanaijua raggae
 
Lucky dube uki sikiliza ngoma zake au skip.. sio kama bob ngoma nayo ikubali ni moja ..uko juu naona watu wana komaa na bob ili waonekane wana jua
hiyo ni kwa ladha yako ya mziki, mziki ni vibe kwakua vibe zako haziendani na Root Reggae Music haikupi uhalali wa kumfananisha Bob na muimba kwaya dube, we endelea kukomaa na kwaya root reggae waachie baba zako
 
Mwanamuziki kutambulika kama Mfalme wa aina fulani ya Muziki, ni kutakana na kazi zake kutambulika na kuufanya muziki huo ukibalike duniani kote na yeye kwa kiasi kikubwa kuwa alama ya Muziki huo

James Brown ndiye aliyeupa umaarufu mkubwa duniani Muziki wa Soul, na ndio maana ulimwengu humtambua kuwa Mfalme wa Soul. Michael Jackson na Muziki wa Pop au jinsi Franco anavyotambulika kama Mfalme wa Rhumba kwani ni yeye ndiye aliyeupeleka muziki huo na kuufanya ukibalike sana Duniani.

Bob Marley, ndiye anayetajwa popote pale duniani kuwa ni alama ya Muziki wa Reggae. Dube alifahamika zaidi afrika. Tembelea site yoyote nchi yeyote duniani, Bob Marley hutambulika hivyo.
 
Back
Top Bottom