Wengi wanaotoa ushauri wa ndoa humu sio wanandoa, sababu ya upendeleo

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
4,031
Reaction score
6,156
Wengi wanaotoa ushauri wa ndoa huku JF si wanandoa. Unaona kabisa huyu hajaoa wala kuolewa.

Neno kuoa ni kuwa na mke unayempata kihalali—iwe kidini, kimila au kiserikali—na unatambuliwa rasmi kama mume wa mtu. Neno kuolewa ni kuwa chini ya mamlaka ya aliyekuoa, yaani unakuwa mke halali wa mwoaji.

Katika ndoa, kuna kiongozi mkuu—yaani mume au yule aliyeoa. Kama umeolewa na mwanamke, hiyo sijui itakuwaje. Ila sasa hapa chini nitaeleza kwa kifupi lile tatizo.

Hapa JF, mwanamume akitoka nje ya ndoa, basi anaendelea kushutumiwa mwanamke. Hii si maana ya kuoa au kuolewa. Katika ndoa haimaanishi mume anapokosea awe juu tu na mamlaka yake.

Eti anampiga mwingi? Hapana. Mke ana haki ya kusamehe au kutosamehe endapo atagundua kudanganywa na mume—na kinyume chake pia.

Lakini mke anamwambiaje mme wake kuwa amekosea? Hapa ndipo JF wanashauri mke kuendelea kukaa kimya na kuvumilia, hata kama amecheat. Yaani, madhara ya kucheat ni sawa na kupiga punyeto au kujichua—utaendelea na kuendelea, mwisho wa siku utaleta magonjwa ya kuambukiza kwa mke au mume.

Sasa wana JF hawa, wanapotoa ushauri, wanafosi sana upande mmoja—hasa kwa mwanamke.

Inamaana mwanamke yeye akicheat anafukuzwa, lakini wewe ukicheat unataka kumkumbatia mkeo huku ukimnyima uhuru wake wa kujitetea. Yaani mke avumilie ila mume amtimuze.

Member amekuta mumewe kapanga kupiga miti na mchepuko. Hapo unaona wanaume wa JF wanamtetea mwanaume mwenzao. What if ingekuwa mwanamke ndo kacheat? Cheki nyuzi nyingi, utaona wanasema: “Timua huyo!”

Kitu muhimu kwa wote ni hiki: kwa dini ya Kikristo, mume au mke akizini—ndoa inakufa. Mume au mke akifa—ndoa inakufa. Ndivyo ilivyo. Katika uzinzi, Mwenyezi Mungu katupa option hizi: mkishindwa kusameheana, basi ndoa ife ikiwa tatizo ni kuzini.

Je, member wa JF uko kwenye ndoa? Kwa asilimia nyingi mbona wengi watoa hukumu kwa kupendelea?

Mod nisaidie kufomat uzi ukae vyema, sijui kuandika vizuri kwa simu.
 
Tunakosea sana kuzilinganisha sawa sawa hizi jinsia mbili. Linapokuja suala la sex mwanaume yupo tayari muda wowote siku yoyote, hii ni tofauti na mwanamke ambae ana visababu na changamoto nyingi.

Mara kachoka, mara yupo period, sometimes anaweza kumnyima tu mumewe kwa kisingizio kwamba akimpa kila siku atamchoka. Hapo hapo kumbuka akijifungua anahitaji almost miezi mitatu hili kushiriki tendo vizuri. Sasa changamoto zote hizo mwanaume atamaliza haja zake wapi?

Biology haitambui hayo masuala ya dini. Wanawake waache kutumia sex kama silaha ya kuwa-control na kuwaadhibu waume zao uko ndoani au ili kuepusha suala la wanaume kuchepuka na kupelekea kuvunja familia basi kama jamii turudishe utamaduni wa mwanaune kuoa wake wengi.

Tutalazimisha sana hizi tamaduni za mke mmoja tulizoletewa na wazungu lakini ukweli ni kwamba mwanamke mmoja hawezi kutosheleza haja za mwanaume. You can't wrestle nature.

Suala la mume kufanya makosa lipo, lakini ndani ya nyumba mume ni kama baba. Hata wewe nyumbani kwenu baba akikosea hauwezi kum-face kama unavyofanya kwa wadogo zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…