PoaKutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam muda huu, leo (Ijumaa, Novemba 07.2025) washtakiwa wengine 95 wamefikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka mawili ya uhaini
Shtaka la kwanza ni kupanga njama za kutenda la uhaini ambapo inaelezwa kuwa kati ya Aprili hadi Oktoba 29 mwaka huu washtakiwa walikuwa wanakula njama za kutenda kosa hilo, shtaka la pili ni kutenda kosa la uhaini kwa kuitishia serikali na kufanya vurugu kwa lengo la kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025, na hivyo washtakiwa walifanya vurugu zilizosababisha pia uhalibifu wa mali
Kwa ujumla, watuhumiwa 240 wamefikishwa Mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka ya uhaini.
Itakua mahakama ya uhainiItafika wakati mahakama nayo itaonekana ni adui wa haki. Tukifika hapo itakuwa patamu sana.
Nimeona walau vijana wawili wanashuka kwenye hayo magari huku wanacheka. Tupo karibu sana kufika wanapotaka tufike. Jela na mahakamani itakuwa si sehemu ya kuogopa tena.Itakua mahakama ya uhaini
07 November 2025Kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam muda huu, leo (Ijumaa, Novemba 07.2025) washtakiwa wengine 95 wamefikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka mawili ya uhaini
Shtaka la kwanza ni kupanga njama za kutenda la uhaini ambapo inaelezwa kuwa kati ya Aprili hadi Oktoba 29 mwaka huu washtakiwa walikuwa wanakula njama za kutenda kosa hilo, shtaka la pili ni kutenda kosa la uhaini kwa kuitishia serikali na kufanya vurugu kwa lengo la kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025, na hivyo washtakiwa walifanya vurugu zilizosababisha pia uhalibifu wa mali
Kwa ujumla, watuhumiwa 240 wamefikishwa Mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka ya uhaini.
Pia soma GE2025 - Watu 9 washtakiwa kwa Uhaini Makambako, idadi yafikia watuhumiwa 196 nchi nzima
View attachment 3498690
Itafika wakati mahakama nayo itaonekana ni adui wa haki. Tukifika hapo itakuwa patamu sana.
Naelewa ila naongelea hatua ambayo mtu anapelekwa mahakamani, anakataa wakili, bila kupepesa macho anakubali anachotuhumiwa hapohapo halafu anamwambia hakimu au jaji, nipe hukumu yangu mambo mengine yaendelee. Tutafika huko.Hatua hiyo tumeshafika
Cha kushangaza wanaoiba kura na kujitangaza wameshinda kihuni ndiyo wanakuwa wametenda uhaini ila msala anaenda kupewa yule anayekemea kitendo hicho.
Tumefanya siasa kuwa ni jinai. Kuna mtu aliwahi kusema "Ukweli ni uhaini katika himaya ya uongo"