Wengine hili janga la derby ya leo tuliliona linakuja kitambo

Mimi shahidi wako, uliwahi kuleta uzi wa mapungufu ya Shabalala nikakuubga mkono lakini wengi walikushambulia, wengine walikuita yanga, wengine walikuuliza umetoa pesa gani za usajili Simba na kejeli nyingine zinazofanana na hizo.
Washabiki tumetofautiana, wapo walipoingia ushabiki kwa kufata Mkumbo, wapo wamefata umaarufu Kama kina mwijaku na wachambuzi wengi, wapo ambao hawataki kusikia lolote baya linalohusu timu yao, wapo mashabiki machawa ambao wanashabikia mtu badala ya timu mfano machawa wa no na wapo ambao pamoja na kuipenda timu wanaikosoa na kuzungumzia mapungufu yake.
 
Uko sawa kabisa. Mwanzoni mwa msimu huu nilikuja na uzi nikisema Yanga itakuwa na mafanikio zaidi ya Simba msimu huu. Na ni juzi juzi tu hapa nilisema kwa maujinga yanayoendelea pale Simba, inaweza isivuke hata hatua ya makundi safari hii. Kama unavyosema, kuna mashabiki mandazi wanadhani ukisema hivyo wewe ni upande wa pili.

Haya nimekuwa nayasema kwa sababu naangalia maeneo mengi yanayoiathiri timu lakini kikubwa ni kile ninachokiona mazoezini. Tunataka umakini wa wachezaji katika mechi wakati umakini huo unakosekana hadi mazoezini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…