Ubaya Ubwela
JF-Expert Member
- Jul 24, 2024
- 1,353
- 3,060
Na wenje anayafanya yotr hayo kwa baraka za FAM
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni muhimu zaidi,
kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi akaweka wazi video footage za CCTV camera zikimuonyesha akiingiza maburungutu ya pesa chumbani kwake kutoka sebuleni alikokua ameketi pamoja na wageni wake bila kuhesabu ni kiasi gani pesa anaingiza chumbani kwake,
hii itasaidia sana kuondoa hii kasumba ya kubwekabweka na kusingiziana mambo ambayo wahusika walikua pamoja ndani ya chumba kimoja. atoe video tumuone alivyokua akitabasamu wakati wa kupokea mlungula ili usafi wa rushwa zake ujulikane
Tulia wewe watu wamekwepa sheria ya mtandao, ukiwashtaki wanampeleka Abdul michanoAbdul hana fedha, fedha yote ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
unless otherwise urekebishe usemi: Hongo kutoka kwa Abdul (na ueleze Abdul ni nani maana sio jina la Pekee kama Yesu au mtume Muhammad S.A.W)
Shubammit..
Watu aina ya Wenje ni wale ambao tunaambiwa wanawatoa ndugu zao kafara ili wapate utajiri. Watu wa namna hii ni hatari sana.Siasa kuielewa ni vigumu sana. 2020 kaka yake Wenje aliuwawa kule Rolya kwa ushindani wa vyama pinzani na CCM.. Leo Wenje huyo huyo anaowaona wazuri hadi anachukua pesa zao. Bora nikae hivi hivi bila ushabiki wa siasa nibaki na Yesu wangu tu.
Kwa Lissu kuacha kugombea Umakamu Mwenyekiti na kugombea Uwenyekiti ni sawa, ila kwa Wenje kugombea uwenyekiti wa Kanda na baadae Umakamu Mwenyekiti sio sawa. Uko sawa kweli?Huyu Wenje amejidhihirisha kuwa ana kazi Maalum ndani ya CHADEMA.
Kwanza yeye ndiye kamleta Abdul CHADEMA. Mivurugano yote unayoiona kwa Sasa imeletwa na Wenje baada ya pesa za Abdul kuingia kwenye chama. Leo kiburi Cha Kambi ya Wenje ni kwamba Kuna pesa walizonazo ndizo Kinga yao. Na pesa za Abdul ndizo zitakazo saidia kuwashawishi wajumbe wa mpigie kura Wenje na Mwenyekiti wake. Wenje asingemleta Abdul kwenye chama yote haya yasingetokea.
Pili, Wenje alitaka kumuingiza Lissu kwenye mtego wa Abdul. Tukumbuke ya kwamba Wenje ndiye aliyempeleka Abdul kwa Lissu. Maana nyingine ni kwamba, Lissu angekubali kuchukua pesa za Abdul Leo hii akina Wenje wangeitumia Kama silaha ya kummaliza kisiasa Lissu. Jiulize Kama kweli Wenje hajui protocali za serikali kuhusu malipo mpaka akaongee na mtoto wa Rais?. Tuwe wakweli. Cha msingi ni kwamba Lissu aliepuka huo mtego la sivyo Leo akina Wenje wangekuja Hadi na video za maongezi au stakabadhi za malipo. Yani Lissu alitumia akili Sana la sivyo wangemmaliza.
Tatu, Wenje yupo kumtoa Lissu kwenye reli. Baada tu ya kuchafuliwa kuwa mwenyekiti ya Kanda ya Victoria , ni Wenje huyo huyo alitangaza kugombea Umakamu Wenyekiti wa CHADEMA. Pamoja kwamba ni haki yake ya kichama, ila ilizua swali kwanini asijielekeze kwanza kwenye Kanda aliyochaguliwa ila anakimbilia kwenye umakamu uenyekiti?. Je ametumwa ili atumie fedha za Abdul kuhonga wajumbe ili afanikiwe kumtoa Lissu. Lissu kwa kujuaa mipango ya Wenje akajitoa kugombea umakamu uenyekiti na kugombea Uenyekiti. Sasa hapo ndipo kelele zikaanza.
Mwisho, Wenje anatumika kumtoa Pambalu kwenye reli. Pambalu alipotangaza kugombea Uenyekiti wa Kanda ya Victoria , Wenje akaibuka naye kutaka kugombea. Kama haitoshi, Wenje kamvamia Pambalu Nyamagana kutaka kugombea ubunge mwaka 2025. Yote ni kumtoa Pambalu kwenye reli na amefanikiwa kwa hilo.
Niwe mkweli, kitendo Cha WanaCHADEMA kuogopa kuchukua fomu za umakamu uenyekiti kisa kumuogopa Wenje na pesa Abdul, kinaonesha jinsi CHADEMA inavyoharibiwa na vibaraka wa CCM.