Wenje kaongea utumbo sana Wasafi FM leo

Wenje kaongea utumbo sana Wasafi FM leo

Wenje na Lissu wote hawaelewi au wanadharau ukweli kuwa kumtumia Abdul kupata fadhila Lissu alipwe hela ni makosa. Ni influence peddling. This is unethical.

Abdul hayupo katika mchakato wa Lissu kulipwa hela. In fact hata rais hayupo. Lissu alikosea tangu Belgium kumpa Samia kazi ya kumtafutia passport mpya na malipo yake. Hizo si kazi za rais wala mwanawe. Lissu katumia position yake kisiasa kupata personal gain unfairly.

Lissu alitakiwa kukataa rushwa ya pesa na rushwa ya fadhila kutoka kwa Abdul.

Inaonekana Lissu kakataa rushwa ya pesa, lakini kakubali rushwa ya fadhila.
 
Nilidhani wenje ana elimu hata kidogo kumbe ni mweupe kiasi hiki.
Naunga mkono hoja, viongozi wa type hii hawawezi kuisaidia lolote Chadema!. Siku ile akihojiwa kuhusu Abdul, kwanini amtumie kudai malipo ya Lissu, akasema kwasababu alimchangia Lissu fedha nyingi,hivyo anampambania Lissu ili akilipwa na yeye ataponea hapo kwa kupata chochote kitu!。

Angalia hapa 2010 nilisema nini kumhusu Wenje CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
Wanabodi,

Sasa nikiwa hapa Dodoma kwenye hili Bunge jipya, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana nao, sio siri, baadhi yao. kwa kuwaangalia tuu na kuzungumza nao, hawana kabisa any substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na kwa wabunge wa viti maalum ndio kabisa usiseme!, kwa baadhi ya wabunge hawa wa viti maalum, sikuona ni kipi kilichowafanya wateuliwe na vyama vyao kuwa wabunge wa viti maalum!, wengi wao japo wameteuliwa kutimiza hitaji la usawa wa kijinsia, sababu za uteuzi wa baadhi yao ni ile jinsia yao kwa matumizi ya kutoa zile huduma muhimu zile,kama huduma za kibinaadamu kama za michangamano baadhi yao wakiwa ni vidumu vya baadhi ya waheshimiwa sana na sio kwa ajili ya kuchangia mijadala na hoja nzito za bungeni!, na hili litathibitishwa na michango yao bungeni katika mijadala mbalimbali, kuna baadhi mtawashuhudia kazi yao itakuwa ni kuonyesha umaridadi wa mavazi, kuonyeshea mishapes na kuuza tuu sura kule mjengoni! na mwisho wa siku hivi 'vidumu' vitakuja kuwaponza wamiliki wa 'vidumu' hivi kwa kupata mapigo ya karma ya wake wa ndoa wa waheshimiwa hao!.

Nilipoongea na baadhi ya wale makamanda waliokata magogo kule Kanda ya Ziwa, kiukweli nimewaona baadhi yao ni watu wa kawaida sana tuu with nothing special kilichowafanya wachaguliwe na kuibwaga CCM na vigogo wake wenye nguvu, influence na pesa, iliyoota mizizi kwenye kanda hivyo , hivyo nimefikia jibu moja tuu la uhakika, kuwa CCM katika baadhi ya maeneo, imechokwa mpaka basi!, upinzani hata ungesimamisha jiwe, jiwe lingechaguliwa!, nadhani hii ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi wa waliojiandikisha kupiga kura, hawakujitokeza kupiga kura, waliona kujitokeza kupiga kura ni wastage of their valuable time, ni kujisumbua tuu!, hata uchague nini,mwisho wa siku mshindi ni yule yule!。
P
 
Nilidhani wenje ana elimu hata kidogo kumbe ni mweupe kiasi hiki. Contents nzima zililuwa zimejikita kwenye hisani ya ccm kuisaidi chadema au hisani kwa namna yoyote. Lisu anataka principals of administration weqe unazungumza hisani? Borq asingeenda wasafi fm amejidharilisha
Kisa kaongea usichotaka kusikia? Lissu achangie chama aache perepeche mpaka ute ute unamtoka mdomoni kwa umbea..... apeleke tumbo huko....atoe mchango kwa chama!!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Naunga mkono hoja, viongozi wa type hii hawawezi kuisaidia lolote Chadema!. Siku ile akihojiwa kuhusu Abdul, kwanini amtumie kudai malipo ya Lissu, akasema kwasababu alimchangia Lissu fedha nyingi,hivyo anampambania Lissu ili akilipwa na yeye ataponea hapo kwa kupata chochote kitu!。

Angalia hapa 2010 nilisema nini kumhusu Wenje CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
P
Hili sakata limesaidia kuwajua wapambanaji hasa wa CHADEMA!! LISSU si miongoni mwao bora hela yangu nimpe Mbowe sio Lissu!!

Lissu na Magufuli akili zao ni sawa sawa tofauti ni taaluma zao tu!
 
Nilidhani wenje ana elimu hata kidogo kumbe ni mweupe kiasi hiki. Contents nzima zililuwa zimejikita kwenye hisani ya ccm kuisaidi chadema au hisani kwa namna yoyote. Lisu anataka principals of administration weqe unazungumza hisani? Borq asingeenda wasafi fm amejidharilisha
Mbona mimi nimeona zaidi ya hayo? Kuna gharama za uchaguzi huu na namna walivyokubaliana kufanya fund raising na jinsi ambavyo Mbowe amepewa jukumu la kutafuta 250M. Au wewe umeangalia kipande tu?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hili sakata limesaidia kuwajua wapambanaji hasa wa CHADEMA!! LISSU si miongoni mwao bora hela yangu nimpe Mbowe sio Lissu!!
Hakika! Kuna watu wanaenda na upepo tu, lakini ukisikia hoja za pande mbili, Lissu ana kasoro nyingi hasa katika ujenzi wa chama
 
Naunga mkono hoja, viongozi wa type hii hawawezi kuisaidia lolote Chadema!. Siku ile akihojiwa kuhusu Abdul, kwanini amtumie kudai malipo ya Lissu, akasema kwasababu alimchangia Lissu fedha nyingi,hivyo anampambania Lissu ili akilipwa na yeye ataponea hapo kwa kupata chochote kitu!。

Angalia hapa 2010 nilisema nini kumhusu Wenje CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
P
To the contrary. Kuna clip ya Lissu akikiri kuwa Abdul aliongozana na mtu mwingine ( Wenje) na alimpa ushahidi kuwa hajalipwa madai yake. Na kuwa alimuambia Abdul kuwa akifanikisha hilo atakuwa rafiki yake wa maisha. Kama ni kweli Abdul alienda kumhonga itakuwaje amuambie mtu corrupt kama yule kuwa anaweza kuwa rafiki yake wa kudumu? Ni ama hio hongo haikuwepo au aliona sio tatizo. Kuna kitu gani cha ajabu kwa Wenje kufanya jitihada Lissu alipwe ile ili amrudishie pesa alizomkopesha? Amezungumzia pia jinsi Lissu alivyomzushia Mwenyekiti tuhuma za kuhongwa gari wakati Mwenyekiti alitoa ushahidi kuwa alinunua kwa pesa zake kwenye mnada. Au hamuamini kuwa Mbowe anaweza kuwa na pesa za kununua magari used mpaka ahongwe na CCM? Au mtu anaetaka kugombea uenyekiti anashindwa kuchangia hata thumni? Na kumbuka alisema kuwa alichangiwa na watu wengi pesa za kulipia fomu ya uchaguzi lakini fomu ililipiwa na Sativa. Mbona hajasema ile michango imetumika wapi?

Wenje anakisaidia sana chama chake kuwaonyesha kuwa huyo wanaodhani ni mtu wa dhahabu, miguu yake ni ya udongo. Lissu wa majukwani sio Lissu wa nyuma ya pazia. Na bado yatatoka mengi ambayo yatatushangaza.

Mwenyekiti Lissu atakuwa zawadi kwa CCM.

Amandla...
 
Hakika! Kuna watu wanaenda na upepo tu, lakini ukisikia hoja za pande mbili, Lissu ana kasoro nyingi hasa katika ujenzi wa chama
Lissu hakua mtu wa kumgeuka mkewe kwa ile hali mkewe alivyopambana nae vile...ujuaji mwingi mbele giza......

Kwa facts tu ukiacha ushabiki Lissu anaeweza torokea uhamishoni akitishiwa Bunduki Chama amuachie nani?

Kisiasa Lissu hayko well matured kama wengi tunavyofikiri!!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Tuachane na hilo jamani kama kuna mtu ana laki moja anikopeshe nitarejesha tarehe 20 mwezi wa kwanza 2025 angalau familia na mimi ifurahi kichwa kinawaka moto wadau
Nenda tu Arusha hizi siku 3 nikujiachia tu mitaani
 
Kwahiyo kwako ukweli ndio utumbo na utumbo kwako ukweli kaa kwa kutulia mtoto kayataka ....
 
Wenje amesema walikuwa watu 4, A,W,TL na msaidizi wa TL, A, hana msaidizi ila dereva wake ni wale jamaa zetu, 1st family wanalindwa na SS wetu!。
P
Sijakuelewa. Kwangu mimi ha msingi ni kuwa Lissu alikiri kuwa suala la malipo yake lilizungumzwa kama alivyodai Wenje. Halafu alipobanwa kuhusu ushahidi Lissu anasema kuwa aliyempa taarifa hizo amekufa! Huyu sio wa kumuamini kabisa.

Amandla...
 
Hakusema alimkopesha,amesema alimchangia!。Mtu ukimchangia unapigania alipwe ili ku recover mchango wako?!。
P
Hizo ni semantics. Hatujui alimpa kwa makubaliano gani maana walikuwa marafiki sana. Unaweza kumsaidia mtu kwa maelewano kuwa akiwa vizuri atakurudishia pesa hizo. Ni kawaida sana ingawa watu wengi hawapendi kulipa kwa dhana hiyo hiyo ya utamkopeshaji rafiki yako?

Amandla....
 
Lissu hakua mtu wa kumgeuka mkewe kwa ile hali mkewe alivyopambana nae vile...ujuaji mwingi mbele giza......

Kwa facts tu ukiacha ushabiki Lissu anaeweza torokea uhamishoni akitishiwa Bunduki Chama amuachie nani?

Kisiasa Lissu hayko well matured kama wengi tunavyofikiri!!
Kamgeuka vipi mke wake?

Amandla...
 
Hizo ni semantics. Hatujui alimpa kwa makubaliano gani maana walikuwa marafiki sana. Unaweza kumsaidia mtu kwa maelewano kuwa akiwa vizuri atakurudishia pesa hizo. Ni kawaida sana ingawa watu wengi hawapendi kulipa kwa dhana hiyo hiyo ya utamkopeshaji rafiki yako?

Amandla....
naunga mkono hoja!。Much respect
P
 
Nilidhani wenje ana elimu hata kidogo kumbe ni mweupe kiasi hiki. Contents nzima zililuwa zimejikita kwenye hisani ya ccm kuisaidi chadema au hisani kwa namna yoyote. Lisu anataka principals of administration weqe unazungumza hisani? Borq asingeenda wasafi fm amejidharilisha
Naunga mkono hoja.
 
Hakusema alimkopesha,amesema alimchangia!。Mtu ukimchangia unapigania alipwe ili ku recover mchango wako?!。
P
Kuna Ile interview Wenje alijifanya na Odemba, alisema wazi kuwa ana hela yake katika hizi ambao Lissu atalipwa, ukiacha mchango
 
Back
Top Bottom