Wenye akili kubwa na walioshiba njooni mnisaidie kupata jibu

Wenye akili kubwa na walioshiba njooni mnisaidie kupata jibu

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Wana JF nisaidien kupata jibu la swala hili mfano, wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga, mambo yamegoma ukalimbikiza deni la kodi ya miezi 3 sawa na Tsh 300,000/= .

Mwenye nyumba akakupa siku tatu uwe umemlipa hiyo pesa ukishindwa anakuondoa kwake,,,, Basi kesho yake ukaamkia kuitafuta hiyo pesa, sasa imefika saa 7 mchana hujapata na unahisi njaa, wakati uko mtaani unajikuta umekatiza karibu na restaurant( hoteli iayouza chakula) ,mara ukasikia mtu anakuita pale restaurant.

Ukaenda ile umefika ukamuona yule mwenye nyumba ndo anakuita, akakuagizia chakula na kukulipia ukaanza kula muda ule ule yeye akaondoka,,,ukahamia kwenye kiti alichokuwa amekalia, ukakuta wallet imejaa noti za elfu 10, ukaichukua na kuiweka mfukoni.

Dakika 3 baadae yule mwenye nyumba akarudi pale akakukuta umekalia kile kiti akakuuliza vipi ndugu umeniokotea waleti yangu hapo kwenye kiti ila sina uhakika kama nimeidondosha hapa ina Tsh Milioni1

Je, UTAKUBALI au UTAKATAA??
 
naona kama hadithi za esopo,alfulela ulela,wagagagigikoko,sindbad baharia..yaani ni mambo ya kusadikika ambayo kwa kipindi hiki sidhani kama hicho unachokiwaza kinaweza kutokea..pambana mkuu tafuta pesaaa.
 
Kutuita kote kule!!!! Mbona jibu jepesi halihitaj akili nyingi
 
Sijawahi kufikiria kama pesa inaweza kuniweka majaribuni hata kama sina pesa kwa wakati huo nikiokota pesa ya mtu na nikamjua huwa namrudishia.

Fikiria shida zako ulizonazo kuna wengine pia wanazo tena zaidi yako.
Kumbe una roho nzuri hivo Viatu. Safiii
 
Rudisha pesa ya watu..uaminifu unalipa
 
Hadithi ya kufikirika. Hakuna mtupa pesa siku Izi.
 
Alalaaaa, hapo kwakweli muujiza utokee tuu, nirudishe 90%[emoji15] [emoji15] nibakiwe na 10% no noo[emoji3] [emoji3]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Unaona ulivyokuwa na imani haba.

Mwanzoni mwa mwaka huu kuna siku nilikuwa nina shida na hela kweli ila mambo yalikuwa bila bila siku hiyo. Majira ya saa 4 usiku nikapokea shilingi laki 1 kwenye M pesa yangu, nikawa nimekaa nawaza nani kanitumia hii pesa wakati sikuwa na miadi na mtu.

Saa tano ananipigia mama mmoja analia kuwa alikuwa anamtumia Mwl ada ya mwanae anaomba nirudishie hela yake. Nikamtumia hela yake.

Kumbe ulikuwa mtego nilianza kupata dili za hovyo hovyo nikapata pesa mara 3000 ya ile [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125].
 
3000X100000
Sawa na

300,000,000

Chai ya malimao hii.
 
Back
Top Bottom