Kwa mtizamo wangu zoezi la sensa limekuwa na "poor planning"
Mitaani watu wengi inaonekana hawajafikiwa na zoezi hili katika siku ya kwanza ya 23/08/2022.
Siku hii ndiyo ya mapumziko, watu wameshinda nyumbani na makarani hawakuonekana. kuanzia tarehe 24, kila mtu atakuwa kwenye shughuli zake na nyumbani zipo nyumba hakuna anayebaki nyumbani, nyingine wanabaki watoto au mtu wa kazi na nyingine anaweza kuwepo mzazi mmoja.
Tumeambiwa zoezi linaendelea kwa siku 7,
Je, tunafuatwa wapi? nyumbani au kwenye shughuli zetu?
Karani akimkuta mtoto mdogo au mfanyakazi atafanikisha sensa kweli?
Kama tunataka zoezi lipate takwimu halisi na si watu kufikia hatua wakaanza kuandika chochote ilimradi waonekane wamefanya kazi, basi ni lazima tufanye tathmini ya zoezi lilivyoanza na kutoa dira ya nini kifanyike