Asalaam aleiku mkuu...ok Jana nilimuuliza mwalimu wangu kuhusu hukmu ya Mzinifu....aliniambia kua ni Sayyidna Ali Khalifa wa nne baada kufa Mtume yeye ndie alimsimamishia hukmu 2 kwa wakati mmoja...Yeye alisema nakupiga mikwaju 100 kwa kufuata maandiko ya Kur-ani...na nakupiga mawe kwa kufuata Khadithi (Sunna) ya Mtume....Kuna Khadithi Sahihi ya Mtume Muhammad inayosema..
"La yahillu Lidammi mri-i illa bithalaatha...
1.Atthayib Zani
2.Waqatlu Nafsi lati harama-Allah ila bil-haqi.
3 Wataariqu lidinihi.
Kiswahili chake. Si halali damu ya mtu yoyote kumwagwa ila kwa mambo ma 3
1.Athayyibu Zani(mzinifu aliekua ndani ya ndoa au aliewahi kuoa au kulewa)
2.Mwenye kuiuwa nafsi bila ya haki ya kuuliwa.
3.Na mtu atakaeihama dini yake ya uislamu.
Khadithi hii ni sahihi kwa sababu hainde kinyume na aya ilioko katika surat-Furqani.25:68-70
Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu(kama unavyojua ukiacha uislamu utaanza ushirika na hapa ndio tunapata hukmu ya mtu Kurtaddi), wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara,
Ukiangalia Ayya hii hawa ni watu watakaokaa Motoni milele....nao wametajwa pamoja na hukmu yao hapa duniani ni ya aina moja
Qur-ani 25:69
Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka.
Qur-ani 25:70
Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maelezo:
Toba ya Mtu alieuwa ni kwenda kwa jamaa ya mtu aliemua...ama wasimamishe kisasi(auliwe) au waamue kusamehe kwa kumtoza fidia...au kusamehe moja kwa moja.
Toba ya Mtu aliehama dini...Ni kwamba baadhi ya wanazuoni wanasema apewe vipindi vi 5 vya sala vikimaliza hajarudi kwenye dini...auliwe...wengine wanasema apewe siku tatu...wengine ni kwamba baada ya kurdani anatakiwa anasihiwe palepale na akitakataa auliwe...
Toba ya Mzinifu ni kwamba ukipatikana ushahidi wa watu wanne wakithibitisha kua amezini apigwe mawe.....
Qiswa cha UMMU JUHAINA.
Huyu ni mwanamke Mzuri sannna ambae alikwenda kwa Mtume kwa hiari yake na kutaka kusimamishiwa hukmu ya Zinaa..yeye alikau amebeba Mimba ya zinaa...Mtume alimuamuru aje na Mzee wake...akamwambia kakae na Binti yako bila kumtukana wala kumnyanyasa...na uniletee miezi mitatu baada ya kujifungua....Mtume aliamrisha achimbiwe shimo na apigwe mawe....Baada kuuliwa aliamrisha akaoshwe asaliwe na akazikwe.....Sayyidna Omar Bin Khatwaabi alikataa kumsalia mwanamke huyu....Mtume alimwambia kuwa unatakiwa umsalie.....kwani Msamaha wa mwanamke huyu kama utagaiwa kwa watu 70 watakwenda peponi wote.....