wenye elimu nzuri ya islam sharia nisaidieni hili.

wenye elimu nzuri ya islam sharia nisaidieni hili.

Ralphryder

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
5,168
Reaction score
1,549
Hivi hakuna adhabu mbadala kwa mzinifu zaidi ya kupigwa mawe hadi kufa? mods naomba mnielewe vizuri na msiondowe uzi huu nia yangu ni kujifunza tu. NB: KAMA SIO MUISLAM MWENYE ELIMU HII USICHANGIE. MATUSI TAFADHALI SITAKI.
 
Hiyo ni kwa wale walio fanya huo uzinifu wakiwa ndani ya ndoa.Kwa wasio kuwa ndani ya ndoa ni bakora 100
 
Hiyo ni kwa wale walio fanya huo uzinifu wakiwa ndani ya ndoa.Kwa wasio kuwa ndani ya ndoa ni bakora 100

Kwa maana hiyo, adhabu hii ni wazinifu wote wawili au ni mwanamke peke yake?
 
Hivi hakuna adhabu mbadala kwa mzinifu zaidi ya kupigwa mawe hadi kufa? mods naomba mnielewe vizuri na msiondowe uzi huu nia yangu ni kujifunza tu. NB: KAMA SIO MUISLAM MWENYE ELIMU HII USICHANGIE. MATUSI TAFADHALI SITAKI.

Mods toeni ujinga huu kwa huyu jamaa ana ids zaidi ya kumi lengo lake ni kuupaka matope uislam,Shame on you!
 
Kwa wenye ndoa wakifumaniwa wanazini na kukawepo ushahidi wa kutosha kuwa wamefanya tendo hilo adhabu yao ni kupigwa mawe mpaka wafe wote wawili. Lakini mawe hayo yasiwe makubwa sana.
Ama kwa mzinifu wa kiume/kike ambaye hajaoa wala kuolewa sheria inamhukumu kupigwa viboko 100 kila mmoja yani mwanamke na mwanaume. Hakuna sheria ktk uislam ya kumhukumu mmoja kati yao na kumwacha mwingine wakati wote walitenda dhambi moja.
Yesu alipoletewa mwanamke mzinifu aliwaambia kuwa anayejiamini kuwa hajatenda dhambi na awe wakwanza kumpiga mawe. Wote walikimbia kwa sababu walikuwa wakiijua sheria kuwa lazima wawapige mawe wote wawili yani wa kike na wakiume, hivyo wote walikuwa wamefanya kosa kwa kumkamata mwanamke tu bila yule aliyezini naye. Kwa kufanya hivyo wote walikuwa na makosa kwa sababu hakuna mzinifu anayezini yeye pekee. Na hiyo ndiyo ilikuwa hekima ya YESU.
 
Mods toeni ujinga huu kwa huyu jamaa ana ids zaidi ya kumi lengo lake ni kuupaka matope uislam,Shame on you!

Mkuu mimi naupenda uislam na nia yangu sio kuupaka matope uislam, nilitaka elimu kdg juu ya hilo jambo, na nashkuru nimejibiwa vema hapo juu, na nilisema hapo mwanzo mtu kama hujui usichangie na matusi sitaki. Sasa unakurupuka na kuda eti nina ID zaidi ya kumi! Habari hiyo umeiokota wapi! Kuwa mstaarabu ndugu.
 
Kwa wenye ndoa wakifumaniwa wanazini na kukawepo ushahidi wa kutosha kuwa wamefanya tendo hilo adhabu yao ni kupigwa mawe mpaka wafe wote wawili. Lakini mawe hayo yasiwe makubwa sana.
Ama kwa mzinifu wa kiume/kike ambaye hajaoa wala kuolewa sheria inamhukumu kupigwa viboko 100 kila mmoja yani mwanamke na mwanaume. Hakuna sheria ktk uislam ya kumhukumu mmoja kati yao na kumwacha mwingine wakati wote walitenda dhambi moja.
Yesu alipoletewa mwanamke mzinifu aliwaambia kuwa anayejiamini kuwa hajatenda dhambi na awe wakwanza kumpiga mawe. Wote walikimbia kwa sababu walikuwa wakiijua sheria kuwa lazima wawapige mawe wote wawili yani wa kike na wakiume, hivyo wote walikuwa wamefanya kosa kwa kumkamata mwanamke tu bila yule aliyezini naye. Kwa kufanya hivyo wote walikuwa na makosa kwa sababu hakuna mzinifu anayezini yeye pekee. Na hiyo ndiyo ilikuwa hekima ya YESU.

Asante sana mkuu,, Mwenyezi Mungu akuzidishie hekima.
 
Kuna mzinifu wakati wa Mtume alipewa adhabu zote mbili kwa pamoja...mikwaju 100 na kupigwa mawe...kwa sababu bakora imetajwa Qur-ani...mawe ni Sunna ya Mtume kwa mtu aliezini akiwa ana mke au mume....au Mtu aliewahikuoa au kuolewa...ndo kusema hata wajane wa Kike au wakiume wapigwe mawe tu....
 
Ni katika ushahidi upi huo sheikh wangu?
 
nitakuletea Qisa Kizima Jina la huyu mtu aliepitishiwa adhabu hii..kuwa na Subra kesho nikienda Darsa nitamuuliza mwalim wangu Insha-Allah
 
Ila kwa kujazia tu hapo unaweza ku refer suratul nuur 24:1-5 shukran jazakallahu khair
 
Asalaam aleiku mkuu...ok Jana nilimuuliza mwalimu wangu kuhusu hukmu ya Mzinifu....aliniambia kua ni Sayyidna Ali Khalifa wa nne baada kufa Mtume yeye ndie alimsimamishia hukmu 2 kwa wakati mmoja...Yeye alisema nakupiga mikwaju 100 kwa kufuata maandiko ya Kur-ani...na nakupiga mawe kwa kufuata Khadithi (Sunna) ya Mtume....Kuna Khadithi Sahihi ya Mtume Muhammad inayosema..

"La yahillu Lidammi mri-i illa bithalaatha...

1.Atthayib Zani
2.Waqatlu Nafsi lati harama-Allah ila bil-haqi.
3 Wataariqu lidinihi.

Kiswahili chake. Si halali damu ya mtu yoyote kumwagwa ila kwa mambo ma 3
1.Athayyibu Zani(mzinifu aliekua ndani ya ndoa au aliewahi kuoa au kulewa)
2.Mwenye kuiuwa nafsi bila ya haki ya kuuliwa.
3.Na mtu atakaeihama dini yake ya uislamu.

Khadithi hii ni sahihi kwa sababu hainde kinyume na aya ilioko katika surat-Furqani.25:68-70

Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu(kama unavyojua ukiacha uislamu utaanza ushirika na hapa ndio tunapata hukmu ya mtu Kurtaddi), wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara,

Ukiangalia Ayya hii hawa ni watu watakaokaa Motoni milele....nao wametajwa pamoja na hukmu yao hapa duniani ni ya aina moja

Qur-ani 25:69
Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka.

Qur-ani 25:70
Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Maelezo:

Toba ya Mtu alieuwa ni kwenda kwa jamaa ya mtu aliemua...ama wasimamishe kisasi(auliwe) au waamue kusamehe kwa kumtoza fidia...au kusamehe moja kwa moja.

Toba ya Mtu aliehama dini...Ni kwamba baadhi ya wanazuoni wanasema apewe vipindi vi 5 vya sala vikimaliza hajarudi kwenye dini...auliwe...wengine wanasema apewe siku tatu...wengine ni kwamba baada ya kurdani anatakiwa anasihiwe palepale na akitakataa auliwe...

Toba ya Mzinifu ni kwamba ukipatikana ushahidi wa watu wanne wakithibitisha kua amezini apigwe mawe.....

Qiswa cha UMMU JUHAINA.

Huyu ni mwanamke Mzuri sannna ambae alikwenda kwa Mtume kwa hiari yake na kutaka kusimamishiwa hukmu ya Zinaa..yeye alikau amebeba Mimba ya zinaa...Mtume alimuamuru aje na Mzee wake...akamwambia kakae na Binti yako bila kumtukana wala kumnyanyasa...na uniletee miezi mitatu baada ya kujifungua....Mtume aliamrisha achimbiwe shimo na apigwe mawe....Baada kuuliwa aliamrisha akaoshwe asaliwe na akazikwe.....Sayyidna Omar Bin Khatwaabi alikataa kumsalia mwanamke huyu....Mtume alimwambia kuwa unatakiwa umsalie.....kwani Msamaha wa mwanamke huyu kama utagaiwa kwa watu 70 watakwenda peponi wote.....
 
Back
Top Bottom