Wenye elimu ya dini nisaidieni: Ni ipi hekima iliyojificha katika mateso makali wayapatayo wanyama?

Kumbe zile pembe zenye ncha kali huwaga ni mapambo ama ni "mikono" ya kupigania wao kwa wao katika "race" zao kugombea majike!

Likija suala la kujihami ni sifuri, hakuna anayepigania maisha yake kwa jasho akijihami zaidi ya kutimua mbio!

Furaha yangu hurejea ninapoangalia carnivorous anapogeuzwa naye kuwa ni chakula!

Fisi anadhibitiwa na simba na kuliwa huku kakasirika.

Simba anazungukwa na mbwa mwitu na kugawanwa fasta.

Nyoka mla panya, analiwa na kenge huku akitekeleza ukamataji wa panya live.

Yote hayo yamewekwa na muumba ili kubalonce ecosystem.
 
Tatizo wanyama hawana utashi kama binadamu, nyati angekuwa na utashi angemkanyaja simba kifuani wakati wa mapambano, simba akiwa chini mwendo wa kunyonya damu nae simba amkanyage kifuani ila hiyo akili hana. Tuseme Muumba alitaka mambo yawe hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…