Uchaguzi wa TLS umekuwa na mafunzo mengi, baadhi yakiwa wazi. Kwa mfano, juhudi kubwa zilizofanywa kumzuia mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo asiwemo kwenye kinyang'anyio.
Kampeni zilipoanza ilionekana nguvu za ziada zikielekezwa kwa mgombea aliyetakiwa kushika nafasi hiyo. Lakini juhudi hizo bado hazikutosha.
Ilipokuja kwenye kupiga kura; pamoja na upiga kura huo kuwa wa wazi na haki, kama ilivyoelezwa na baadhi ya washiriki; bado kuna maswali ambayo yanahitaji majibu.
Kwa mfano: Kama kura zilizopigwa hazikuzidi elfu nne (4,000); itakuwaje kuhesabu kura hizo ichukue muda zaidi ya saa kadhaa kabla ya kutangazwa mshindi?
Msingi wa swali hili upo wazi, hasa kutokana na uzoefu. Ucheleweshaji wa kutangaza mshindi ni njia mojawapo ya kuiba ushindi.
Sasa naomba mwenye kujua, atoe dukuduku hili kwamba ucheleweshaji huo haukuwa njia ya kutaka kubadili matokeo ya uchaguzi huu! Baada ya kupima upepo ulivyo kuwa ukivuma, wenye mamlaka ya kutoa amri wakaamua matokeo yatangazwe kama ylivyo kuwa.
Je, huko kwenye chaguzi kubwa zinazofuata nako haki hii itakuwepo au yale mazoea ya siku zote yataachwa yatumike!?
Pia soma > News Alert: - Uchaguzi wa TLS 2024: Boniface Mwabukusi ashinda Urais, apata kura 1274